Wimbo Na. 20
Bariki Kukutana Kwetu
Makala Iliyochapishwa
1. Ee Yehova tubariki,
Katika mikutano.
Twakuomba uwe nasi;
Utupe roho yako.
2. Kubali ibada yetu;
Utufundishe Neno.
Tuzoeze kuhubiri;
Na kuwa na upendo.
3. Ewe Baba twakuomba
Umoja na amani.
Nayo enzi yako kuu,
Tutie maanani.
(Ona pia Zab. 22:22; 34:3; Isa. 50:4.)