Wimbo Na. 15
Uumbaji Unatangaza Utukufu wa Yehova
Makala Iliyochapishwa
1. Ee Yehova, mimi ninajua.
Mbingu zako zinakutukuza.
Muchana na usiku zasema
Zatangaza kazi zako njema.
Muchana na usiku zasema
Zatangaza kazi zako njema.
2. Mwezi, jua, nyota umeumba.
Nayo bahari ukaiumba.
Mbingu zako tuzitazamapo.
Twajiona duni mbele zako.
Mbingu zako tuzitazamapo.
Twajiona duni mbele zako.
3. Vikumbusho vyako si hafifu.
Sheria zako ni kamilifu.
Zatufanya tuwe na hekima.
Tuzishike, tupate uzima.
Zatufanya tuwe na hekima.
Tuzishike, tupate uzima.
(Ona pia Zab. 12:6; 89:7; 144:3; Rom. 1:20.)