Wimbo Na. 17
Songeni Mbele, Enyi Mashahidi!
1. Watu wa Mungu wameazimia,
Kazi ya kuhubiri itatimia.
Shetani akiwavamia,
Kwa nguvu za Mungu wavumilia.
(KORASI)
Haya tusonge mbele Ee Mashahidi!
Kufanya kazi ya Mungu na tuzidi!
Yaja Paradiso aliyoahidi,
Yehova Mungu tumuhimidi.
2. Askari wa Yehova wanakesha.
Ulimwengu hautawatetemesha.
Na madoa wajiepusha.
Utimilifu wetu twadumisha.
(KORASI)
Haya tusonge mbele Ee Mashahidi!
Kufanya kazi ya Mungu na tuzidi!
Yaja Paradiso aliyoahidi,
Yehova Mungu tumuhimidi.
3. Enzi ya Mungu yadharauliwa.
Jina lake kuu limechafuliwa.
Karibuni litasifiwa.
Mbele za wote litatambulishwa.
(KORASI)
Haya tusonge mbele Ee Mashahidi!
Kufanya kazi ya Mungu na tuzidi!
Yaja Paradiso aliyoahidi,
Yehova Mungu tumuhimidi.
(Ona pia Flp. 1:7; 2 Tim. 2:3, 4; Yak. 1:27.)