Wimbo Na. 33
Msiwaogope!
1. Watu wangu musisite,
Ufalme tangazeni.
Musihofu adui.
Wote hubirieni.
Mwana wangu, Kristo Yesu,
Katimua Shetani,
Atamfunga karibuni,
Kisha kuwe amani.
(KORASI)
Watu wangu musihofu.
Nitawapa wokovu.
Nitalinda wenye kicho,
Kama mboni ya jicho.
2. Japo adui ni wengi,
Japo wanawatisha,
Japo wanawacheka,
Ili kuwapotosha,
Musihofu watu wangu;
Pigeni moyo konde.
Nitatunza wa’minifu,
Adui wamushinde.
(KORASI)
Watu wangu musihofu.
Nitawapa wokovu.
Nitalinda wenye kicho,
Kama mboni ya jicho.
3. Sitawasahau kamwe;
Nitawapa ulinzi.
Hata mufe shambani,
Kifo kitanitii.
Hata wakiua mwili;
Nafsi hawataweza.
Iweni waaminifu,
Nami nitawakweza.
(KORASI)
Watu wangu musihofu.
Nitawapa wokovu.
Nitalinda wenye kicho,
Kama mboni ya jicho.
(Ona pia Kum. 32:10; Neh. 4:14; Zab. 59:1; 83:2, 3.)