Wimbo Na. 6
Sala ya Mtumishi wa Mungu
Makala Iliyochapishwa
1. Baba, Bwana Mwenye Enzi Kuu,
Jina lako litukuzwe milele;
Rehema zako zitadumu,
U Mwaminifu, wategemeka.
U Mwaminifu sana,
Rehema zitadumu.
2. Tusaidie tupende kweli,
Tuyafanye mapenzi yako wewe.
Amuri zako tuzishike,
Na tuwalishe kondoo wako.
Tuwalishe kondoo,
Amuri tuzishike.
3. Utupatie hekima yako,
Jaza upendo mioyoni mwetu.
Ili tuonyeshe rehema,
Tufunze watu ukuu wako.
Tufunze watu wako,
Tuonyeshe rehema.
(Ona pia Zab. 143:10; Yoh. 21:15-17; Yak. 1:5.)