Wimbo Na. 12
Uzima wa Milele Umeahidiwa
Makala Iliyochapishwa
1. Mungu ametuahidi,
Uzima wa milele.
Wapole watairithi,
Dunia milele.
(KORASI)
Inawezekana,
Kuishi milele.
Ahadi za Mungu,
Zitatimia.
2. Paradiso duniani,
Kukiwa na uhuru.
Mungu atatuongoza,
Tuwe na amani.
(KORASI)
Inawezekana,
Kuishi milele.
Ahadi za Mungu,
Zitatimia.
3. Wafu watafufuliwa,
Kusiwe na huzuni.
Wakati Yehova Mungu,
Atafuta chozi.
(KORASI)
Inawezekana,
Kuishi milele.
Ahadi za Mungu,
Zitatimia.
(Ona pia Isa. 25:8; Luka 23:43; Yoh. 11:25; Ufu. 21:4.)