Wimbo Na. 78
Ustahimilivu
Makala Iliyochapishwa
1. Yehova, Baba yetu,
Hulipenda jina lake.
Ataka litakaswe,
Na suto kuondolewa.
Kavumilia mengi,
Tena muda murefu;
Ni mustahimilivu,
Hajachoka kamwe.
Ataka watu wote,
Wapate kuokolewa.
Astahimili yote,
Kwa faida yetu sote.
2. Nasi tunahitaji
Kuwa wastahimilivu.
Ghadhabu tuepuke.
Tukae kwa utulivu.
Tuzingatie mema,
Wafanyayo wengine.
Tutumaini mema,
Japo matatizo.
Na sifa za Kikristo,
Tuonyeshe sikuzote.
Na kwa kufanya hivyo,
Tumuige Mungu wetu.
(Ona pia Kut. 34:14; Isa. 40:28; 1 Kor. 13:4, 7; 1 Tim. 2:4.)