Wimbo Na. 76
Yehova, Mungu wa Amani
Makala Iliyochapishwa
1. Mungu wa amani,
Yehova Mungu wetu,
Tunakuomba amani,
Sifa ya roho yako.
Ulitununua;
Kwa damu ya Mwanao.
Twaomba amani yako
Iwe pamoja nasi.
2. Hakuna amani,
Katika ulimwengu.
Hata hivyo watu wako
Wana amani tele.
Tunapotimiza
Nadhiri zetu kwako,
Twaomba utubariki
Kwa kutupa amani.
3. Twapata nuru ya
Neno na roho yako.
Twaongozwa na kulindwa,
Katika ulimwengu.
Na kama umande,
Twapata utulivu,
Mioyo nayo akili
Zetu ziwe salama.
(Ona pia Zab. 4:8; Flp. 4:6, 7; 1 The. 5:23.)