WIMBO NA. 112
Yehova, Mungu wa Amani
Makala Iliyochapishwa
1. Mungu wa upendo,
Yehova Mungu wetu,
Twakuomba roho yako,
Tukuze sifa zako.
Ulitununua,
Kwa damu ya Mwanao.
Twaomba utukubali
Tupe amani Yako.
2. Roho yako wewe,
Yatupa ufahamu.
Twaongozwa na kulindwa
Katika ulimwengu.
Tunatazamia
Mwisho wa matatizo.
Tupe roho takatifu,
Tuishi kwa amani.
3. Umewakusanya
Wale uwapendao.
Tumependelewa sana,
Kukuabudu wewe.
Utawala wako,
Utaleta baraka.
Kisha watumishi wako,
Waishi kwa amani.
(Ona pia Zab. 4:8; Flp. 4:6, 7; 1 The. 5:23.)