Wimbo Na. 60
Atakupa Nguvu
Makala Iliyochapishwa
1. Kweli yake Mungu amekufundisha,
Amekuleta katika nuru.
Aliona moyo wako watamani,
Kufanya mambo yaliyo mema.
Kwa sala, ulijiweka wakfu;
Daima atakuimarisha.
(KORASI)
Kwa damu ya Mwanaye, alikununua.
Hukuimarisha, na kukupa nguvu.
Atakulinda na kukuongoza wewe.
Hukuimarisha, na kukupa nguvu.
2. Kamutoa Yesu Mwana wake afe;
Hivyo, ataka ufanikiwe.
Basi kama Mungu alifanya hivyo,
Bila shaka atakupa nguvu.
Imani yako hatasahau;
Walio wake atawatunza.
(KORASI)
Kwa damu ya Mwanaye, alikununua.
Hukuimarisha, na kukupa nguvu.
Atakulinda na kukuongoza wewe.
Hukuimarisha, na kukupa nguvu.
(Ona pia Rom. 8:32; 14:8, 9; Ebr. 6:10; 1 Pet. 2:9.)