Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • ll seh. ya 4 kur. 10-11
  • Kumsikiliza Shetani Kulikuwa na Matokeo Gani?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kumsikiliza Shetani Kulikuwa na Matokeo Gani?
  • Msikilize Mungu Uishi Milele
  • Habari Zinazolingana
  • Maisha Yalikuwaje Katika Paradiso?
    Msikilize Mungu Uishi Milele
  • Sehemu ya 4
    Msikilize Mungu
  • Wafu Wako Wapi?
    Biblia Inafundisha Nini Hasa?
  • Kwa Nini Tunazeeka na Kufa?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Toleo la Watu Wote)—2019
Pata Habari Zaidi
Msikilize Mungu Uishi Milele
ll seh. ya 4 kur. 10-11

SEHEMU YA 4

Kumsikiliza Shetani Kulikuwa na Matokeo Gani?

Adamu na Hawa hawakumtii Mungu, basi wakafa. Mwanzo 3:6, 23

Hawa ala tunda lililokatazwa na anampa Adamu pia

Hawa alimsikiliza nyoka na akala tunda lililokatazwa. Baadaye, alimpa Adamu, naye akala.

Adamu na Hawa wanaondoka katika Paradiso iliyokuwa makao yao

Kwa kufanya hivyo, walifanya dhambi ya kutotii. Mungu akawaondoa katika makao yao ya Paradiso.

Adamu na Hawa wanazeeka na kisha wanakufa

Maisha yakawa magumu kwao na kwa watoto wao. Wakazeeka na kufa. Hawakwenda katika ulimwengu wa roho; walikoma kuwapo.

Wafu hawana uhai kama vile mavumbi yasivyo na uhai. Mwanzo 3:19

Watu wa tamaduni mbalimbali katika nyakati mbalimbali

Tunakufa kwa sababu sote ni wazao wa Adamu na Hawa. Wafu hawawezi kuona au kusikia au kufanya jambo lolote.—Mhubiri 9:5, 10.

Msichana anakufa na familia yake inaomboleza

Yehova hakukusudia watu wafe. Hivi karibuni, atawafufua wale wanaolala katika kifo. Iwapo watamsikiliza, wataishi milele.

  • Kwa nini tunakufa?​—Waroma 5:12.

  • Kifo hakitakuwapo tena.—1 Wakorintho 15:26.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki