Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • ll seh. ya 3 kur. 8-9
  • Maisha Yalikuwaje Katika Paradiso?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Maisha Yalikuwaje Katika Paradiso?
  • Msikilize Mungu Uishi Milele
  • Habari Zinazolingana
  • Yuko Aliye Juu Zaidi
    Kumsikiliza Mwalimu Mkuu
  • Wengine Wana Mamlaka Kuliko Sisi
    Jifunze Kutoka kwa Mwalimu Mkuu
  • Sababu Walipoteza Makao Yao
    Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia
  • Kumsikiliza Shetani Kulikuwa na Matokeo Gani?
    Msikilize Mungu Uishi Milele
Pata Habari Zaidi
Msikilize Mungu Uishi Milele
ll seh. ya 3 kur. 8-9

SEHEMU YA 3

Maisha Yalikuwaje Katika Paradiso?

Yehova aliwapa Adamu na Hawa vitu vingi vizuri. Mwanzo 1:28

Baada ya Yehova kuumba Hawa, anampeleka kwa Adamu

Yehova alimuumba mwanamke wa kwanza, Hawa, na akampa Adamu mwanamke huyo awe mke wake.—Mwanzo 2:21, 22.

Yehova aliwaumba wakiwa na akili na miili mikamilifu, bila kasoro yoyote.

Adamu na Hawa wanatazama Paradiso ambayo ni makao yao

Waliishi katika bustani ya Edeni iliyokuwa Paradiso, bustani hiyo maridadi sana ilikuwa na mto, miti ya matunda, na wanyama.

Yehova alizungumza nao; akawafundisha. Ikiwa wangemsikiliza, wangeishi milele katika Paradiso duniani.

Mungu aliwaambia wasile matunda ya mti mmoja. Mwanzo 2:16, 17

Mti ulio katika bustani ambao Yehova aliwaambia Adamu na Hawa wasile matunda yake

Yehova aliwaonyesha Adamu na Hawa mti mmoja wa matunda katika bustani na kuwaambia kwamba kama wangekula matunda ya mti huo, wangekufa.

Malaika mwovu Shetani Ibilisi anatumia nyoka kuzungumza na Hawa

Malaika mmoja alimwasi Mungu. Malaika huyo mwovu anaitwa Shetani Ibilisi.

Shetani hakutaka Adamu na Hawa wamtii Yehova. Hivyo, akatumia nyoka kumwambia Hawa kwamba akila matunda ya mti huo, hatakufa, bali atakuwa kama Mungu. Lakini huo ulikuwa uwongo mtupu.—Mwanzo 3:1-5.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki