Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • my hadithi 4
  • Sababu Walipoteza Makao Yao

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Sababu Walipoteza Makao Yao
  • Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia
  • Habari Zinazolingana
  • Adamu na Hawa Hawakumtii Mungu
    Masomo Unayoweza Kujifunza Katika Biblia
  • Maisha Yalikuwaje Katika Paradiso?
    Msikilize Mungu Uishi Milele
  • Yuko Aliye Juu Zaidi
    Kumsikiliza Mwalimu Mkuu
  • Mungu Anaweza Kuhuzunika—Jinsi Tunavyoweza Kumfurahisha
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2013
Pata Habari Zaidi
Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia
my hadithi 4
Adamu na Hawa wanafukuzwa katika bustani ya Edeni

HADITHI YA 4

Sababu Walipoteza Makao Yao

TAZAMA yanayotendeka sasa. Adamu na Hawa wanafukuzwa katika bustani nzuri ya Edeni. Unajua sababu?

Walifanya jambo baya sana. Yehova anawaadhibu. Unajua jambo baya ambalo Adamu na Hawa walifanya?

Ni jambo ambalo Mungu aliwakataza. Mungu aliwaambia wale chakula cha miti ya bustani. Lakini si cha mti ambao Mungu aliwakataza, ili wasife. Huo ulikuwa mti wake peke yake. Tunajua ni makosa kuchuka kitu cha mtu mwingine, sivyo? Basi, kulitokea nini?

Siku moja Hawa alipokuwa peke yake katika bustani, nyoka alisema naye. Ajabu! Akamwambia hawa ale tunda la mti ambao Mungu aliwakataza. Yehova hakuumba nyoka waseme. Mtu fulani alifanya nyoka aseme. Ni nani?

Si Adamu. Ni mmoja wa watu ambao Yehova alikuwa ameumba zamani kabla ya dunia. Ni malaika ambao hatuwezi kuona. Malaika huyo mmoja akawa na kiburi sana. Alianza kuwaza kwamba ingefaa atawale kama Mungu. Alitaka watu wamtii yeye kuliko Yehova. Huyo ndiye malaika aliyemfanya nyoka aseme.

Malaika huyo alimdanganya Hawa. Alipomwambia watafanana na Mungu wakila tunda hilo, Hawa alimwamini. Hawa akala, hata Adamu. Adamu na Hawa hawakumtii Mungu. Ndiyo sababu walipoteza makao yao mazuri.

Lakini siku moja Mungu ataifanya dunia nzima iwe nzuri kama bustani ya Edeni. Tutajifunza namna wewe unaweza kushiriki kuifanya hivyo. Lakini sasa, tuchunguze yaliyowapata Adamu na Hawa.

Mwanzo 2:16, 17; 3:1-13, 24; Ufunuo 12:9.

Maswali ya Funzo

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki