Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • lfb somo la 3 uku. 14-uku. 15 fu. 3
  • Adamu na Hawa Hawakumtii Mungu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Adamu na Hawa Hawakumtii Mungu
  • Masomo Unayoweza Kujifunza Katika Biblia
  • Habari Zinazolingana
  • Sababu Walipoteza Makao Yao
    Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia
  • Wengine Wana Mamlaka Kuliko Sisi
    Jifunze Kutoka kwa Mwalimu Mkuu
  • Maisha Yalikuwaje Katika Paradiso?
    Msikilize Mungu Uishi Milele
  • Yuko Aliye Juu Zaidi
    Kumsikiliza Mwalimu Mkuu
Pata Habari Zaidi
Masomo Unayoweza Kujifunza Katika Biblia
lfb somo la 3 uku. 14-uku. 15 fu. 3
Adamu na Hawa wakiondoka katika bustani ya Edeni

SOMO LA 3

Adamu na Hawa hawakumtii Mungu

Adamu akiwa ameshika tunda walilokatazwa ambalo alipewa na Hawa

Siku moja Hawa alipokuwa peke yake, nyoka alizungumza naye. Alimwuliza hivi: ‘Je, ni kweli kwamba Mungu amewakataza kula matunda ya miti yote?’ Hawa akajibu hivi: ‘Tunaweza kula matunda ya miti yote, isipokuwa mti mmoja. Tukila matunda ya mti huo, tutakufa.’ Nyoka akamwambia: ‘Hamtakufa. Kwa kweli, mkila matunda ya mti huo, mtakuwa kama Mungu.’ Je, nyoka alisema kweli? Hapana, huo ulikuwa uwongo. Lakini Hawa aliamini maneno hayo. Kadiri Hawa alivyoendelea kuyatazama matunda ya mti huo, ndivyo alivyozidi kutamani kuchuma na kula. Alikula tunda hilo na kisha akampatia Adamu. Adamu alijua kwamba wangekufa ikiwa wangemwasi Mungu. Hata hivyo, Adamu aliamua kula tunda hilo.

Adamu na Hawa wakiondoka katika bustani ya Edeni, malaika na upanga unaowaka moto wakilinda mwingilio wa bustani

Baadaye siku hiyo, Yehova alizungumza na Adamu na Hawa. Aliwauliza kwa nini wamemwasi. Hawa alimlaumu nyoka, na Adamu akamlaumu Hawa. Kwa kuwa Adamu na Hawa hawakumtii Yehova, aliwafukuza katika bustani. Ili kuwazuia wasirudi katika bustani, Mungu aliwaweka malaika na upanga uliowaka moto ili kulinda mwingilio wa bustani.

Yehova aliahidi kumwadhibu kiumbe aliyemdanganya Hawa. Si nyoka halisi aliyezungumza na Hawa. Yehova hakuwaumba nyoka wakiwa na uwezo wa kuzungumza. Malaika mbaya alimfanya nyoka azungumze. Alifanya hivyo ili kumdanganya Hawa. Malaika huyo anaitwa Shetani Ibilisi. Wakati ujao, Yehova atamharibu Shetani ili asiendelee kuwashawishi watu wafanye mambo mabaya.

“Ibilisi . . . alikuwa muuaji alipoanza, naye hakusimama imara katika kweli, kwa sababu kweli haimo ndani yake.”​—Yohana 8:44

Maswali: Kwa nini Hawa alikula tunda? Ni nini kilichotokea baada ya Adamu na Hawa kumwasi Yehova? Shetani Ibilisi ni nani?

Mwanzo 3:1-24; Yohana 8:44; 1 Yohana 3:8; Ufunuo 12:9

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki