Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • ll seh. ya 7 kur. 16-17
  • Yesu Alikuwa Nani?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Yesu Alikuwa Nani?
  • Msikilize Mungu Uishi Milele
  • Habari Zinazolingana
  • Sehemu ya 7
    Msikilize Mungu
  • Yesu Kristo Ni Nani?
    Biblia Inatufundisha Nini?
  • Majibu ya Maswali ya Biblia
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2013
  • Yesu Kristo Ni Nani?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2005
Pata Habari Zaidi
Msikilize Mungu Uishi Milele
ll seh. ya 7 kur. 16-17

SEHEMU YA 7

Yesu Alikuwa Nani?

Yehova alimtuma Yesu duniani. 1 Yohana 4:9

Yesu akiwa kwenye mkono wa kuume wa Mungu huko mbinguni

Ikiwa tunataka kumpendeza Yehova, ni lazima tumsikilize mtu mwingine wa maana sana. Muda mrefu kabla ya kumuumba Adamu, Yehova alimuumba kiumbe wa roho mwenye nguvu sana mbinguni.

Maria akiwa na mimba na baadaye Yesu anazaliwa

Baadaye, Yehova alimtuma azaliwe huko Bethlehemu na bikira aliyeitwa Maria. Mtoto huyo akapewa jina, Yesu.—Yohana 6:38.

Yesu anawafundisha wengine kumhusu Yehova

Akiwa mwanadamu duniani, Yesu alionyesha sifa za Mungu kikamili. Alikuwa mwenye fadhili, upendo, na mwenye kufikika. Aliwafundisha wengine kweli kumhusu Yehova bila woga.

Yesu alitenda mema lakini alichukiwa. 1 Petro 2:21-24

Yesu amfufua msichana na kumponya mwanamume

Yesu pia aliponya wagonjwa na akawafufua wafu.

Viongozi wa kidini walimchukia Yesu kwa sababu alifunua mafundisho yao ya uwongo na njia zao mbovu.

Yesu anapigwa kisha anauawa

Viongozi wa kidini waliwachochea Waroma wampige Yesu na kumuua.

  • Kwa nini ni muhimu kumjua Yesu?—Yohana 17:3.

  • Yesu alifanya nini mbinguni kabla ya kuja duniani?—Wakolosai 1:15-17.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki