Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • T-35 kur. 1-4
  • Je, Kweli Wafu Wataishi Tena?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je, Kweli Wafu Wataishi Tena?
  • Je, Kweli Wafu Wataishi Tena?
  • Habari Zinazolingana
  • Una Maoni Gani Kuhusu Wakati Ujao?
    Una Maoni Gani Kuhusu Wakati Ujao?
  • Je, Kuteseka Kutaisha?
    Je, Kuteseka Kutaisha?
  • Ni Nani Hasa Anayeuongoza Ulimwengu?
    Ni Nani Hasa Anayeuongoza Ulimwengu?
  • Ufalme wa Mungu Ni Nini?
    Ufalme wa Mungu Ni Nini?
Pata Habari Zaidi
Je, Kweli Wafu Wataishi Tena?
T-35 kur. 1-4
Wazazi wakitazama picha za msichana wao mdogo aliyekufa
Wazazi wakitazama picha za msichana wao mdogo aliyekufa

Je, Kweli Wafu Wataishi Tena?

Ungejibuje swali hilo . . .

  • ndiyo?

  • hapana?

  • labda?

BIBLIA HUSEMA HIVI

“Kutakuwa na ufufuo.”—Matendo 24:15, Tafsiri ya Ulimwengu Mpya.

FAIDA ZA KUAMINI JAMBO HILO

Utapata faraja wapendwa wako wanapokufa.—2 Wakorintho 1:3, 4.

Utaacha kuogopa kufa.—Waebrania 2:15.

Utakuwa na tumaini la kukutana tena na wapendwa wako waliokufa.—Yohana 5:28, 29.

Familia na mjane wakifarijiwa na tumaini la ufufuo
Familia na mjane wakifarijiwa na tumaini la ufufuo

JE, KWELI TUNAWEZA KUAMINI KILE AMBACHO BIBLIA INASEMA?

Ndiyo, kwa angalau sababu tatu:

  • Mungu ndiye aliyeumba uhai. Biblia inasema kwamba Yehova Mungu ndiye “huwapa watu wote uhai.” (Matendo 17:24, 25; Zaburi 36:9) Bila shaka, yule aliyewapa viumbe wote uhai ana uwezo wa kumfanya mtu aliyekufa awe hai tena.

  • Mungu aliwahi kuwafufua wanadamu wakati uliopita. Biblia inataja visa vinane vya watu—vijana kwa wazee, wa kiume na wa kike—ambao walifufuliwa hapa duniani. Wengine walikuwa wamekufa kwa muda mfupi, lakini mmoja alikuwa kaburini kwa siku nne!—Yohana 11:39-44.

  • Mungu anatamani kufanya hivyo tena. Yehova anachukia kifo; anakiona kuwa adui. (1 Wakorintho 15:26) ‘Anatamani’ kumshinda adui huyo na kukomesha kifo kupitia ufufuo. Anatamani sana kuwafufua wale walio katika kumbukumbu lake na kuwaona wakiishi duniani tena.—Ayubu 14:14, 15.

JAMBO LA KUFIKIRIA

Mvuolana mdogo akikua na kuwa mwanamume mzee
Mvuolana mdogo akikua na kuwa mwanamume mzee

Kwa nini tunazeeka na kufa?

Biblia inajibu swali hilo kwenye MWANZO 3:17-19 na WAROMA 5:12.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki