Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • yc somo la 2 kur. 6-7
  • Rebeka alitaka kumfurahisha Yehova

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Rebeka alitaka kumfurahisha Yehova
  • Wafundishe Watoto Wako
  • Habari Zinazolingana
  • Rebeka Alikuwa Tayari Kumpendeza Yehova
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2010
  • “Mimi Niko Tayari Kwenda”
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Toleo la Watu wote)—2016
  • Kumtafutia Isaka Mke
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1997
  • Rebeka—Mwanamke Mwenye Bidii Aliyemwogopa Mungu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2004
Pata Habari Zaidi
Wafundishe Watoto Wako
yc somo la 2 kur. 6-7
Eliezeri, Rebeka, watumishi, na ngamia kumi, wakisafiri kuelekea Kanaani

SOMO LA 2

Rebeka Alitaka Kumfurahisha Yehova

Rebeka alikuwa mwanamke aliyempenda Yehova. Mume wake aliitwa Isaka, yeye pia alimpenda Yehova. Rebeka alikutanaje na Isaka? Rebeka alifanya nini ili kuonyesha kwamba alitaka kumfurahisha Yehova? Sasa, ngoja tujifunze mambo fulani yanayomhusu Rebeka.

Wazazi wa Isaka walikuwa Abrahamu na Sara. Waliishi katika nchi ya Kanaani, mahali ambapo watu hawakumwabudu Yehova. Lakini Abrahamu alitaka mtoto wake aoe mwanamke ambaye alimwabudu Yehova. Kwa hiyo, akamtuma mtumishi wake mahali palipoitwa Harani, ambako baadhi ya watu wa ukoo wa Abrahamu waliishi, ili akamtafutie Isaka mke. Inawezekana mtumishi huyo alikuwa Eliezeri.

Rebeka akimimina maji ili ngamia wa Eleazari wanywe

Rebeka alikuwa tayari kufanya kazi ngumu ili kuwachotea ngamia maji

Eliezeri alisafiri pamoja na baadhi ya watumishi wengine wa Abrahamu. Ilikuwa safari ndefu sana. Walisafiri wakiwa na ngamia kumi waliobeba chakula na zawadi. Eliezeri angemjuaje mwanamke ambaye angemfaa Isaka? Eliezeri na watumishi wengine walipofika Harani, walisimama kwenye kisima kwa sababu Eliezeri alijua kwamba baada ya muda fulani watu wangeanza kuja kuchota maji. Eliezeri alisali kwa Yehova akisema: ‘Ikiwa nitamwomba msichana anipe maji mimi na ngamia zangu, nitajua kwamba huyo ndiye mwanamke uliyemchagua.’

Kisha msichana Rebeka akaja kisimani. Biblia inasema kwamba alikuwa mrembo sana. Eliezeri akamwomba Rebeka maji ya kunywa, naye akajibu: ‘Bila shaka nitakupa. Nitachota maji kwa ajili yako na kwa ajili ya ngamia zako pia.’ Hebu fikiria jambo hilo! Ngamia wenye kiu hunywa maji mengi sana, hivyo Rebeka alihitaji kukimbia kisimani tena na tena ili kwenda kuwachotea maji. Je, unamwona jinsi anavyofanya kazi kwa bidii?— Eliezeri alishangazwa na jinsi ambavyo Yehova alijibu sala yake.

Eliezeri akampa Rebeka zawadi nyingi nzuri. Rebeka akamkaribisha Eliezeri na wale watumishi wengine nyumbani kwao. Eliezeri akawaeleza sababu iliyomfanya Abrahamu amtume na jinsi ambavyo Yehova alijibu sala yake. Familia ya Rebeka ilifurahi kwamba hatimaye Rebeka ataolewa na Isaka.

Rebeka aliena Kanaani pamoja na Eliezeri na kisha akaolewa na Isaka

Je, unafikiri Rebeka alitaka kuolewa na Isaka?— Rebeka alijua kwamba Yehova ndiye aliyemwongoza Eliezeri hadi Harani. Hivyo, familia yake ilipomuuliza ikiwa alitaka kwenda Kanaani ili akaolewe na Isaka, Rebeka akajibu: ‘Ndiyo, ninataka kwenda.’ Mara moja, akaondoka na Eliezeri. Walipofika Kanaani akaolewa na Isaka.

Kwa kuwa Rebeka alifanya yale ambayo Yehova alitaka afanye, Yehova alimbariki. Miaka mingi baadaye, Yesu alizaliwa katika ukoo wa Isaka na Rebeka! Ikiwa utakuwa kama Rebeka na kumfurahisha Yehova, basi wewe pia atakubariki.

SOMA KATIKA BIBLIA YAKO

  • Mwanzo 12:4, 5; 24:1-58, 67

MASWALI:

  • Rebeka alikuwa nani?

  • Kwa nini Abrahamu hakutaka Isaka aoe mwanamke wa Kanaani?

  • Eliezeri alijuaje kwamba Rebeka ndiye mwanamke anayefaa kuolewa na Isaka?

  • Tunaweza kufanya nini ili tuwe kama Rebeka?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki