Wimbo Na. 143
Nuru Katika Ulimwengu Wenye Giza
Makala Iliyochapishwa
Ni siku, zenye uovu,
Nuru inang’aa.
Ni nuru, kama ya jua
Siku ianzapo.
(KORASI)
Ujumbe mwangavu,
Watoa tumaini.
Tunapohubiri—
Giza latoweka,
Nuru yaonekana—
Siku mpya.
Twamushe wanaolala
Muda umekwisha.
Twasali. Twatia moyo.
Nyuma wasirudi.
(KORASI)
Ujumbe mwangavu,
Watoa tumaini.
Tunapohubiri—
Giza latoweka,
Nuru yaonekana—
Siku mpya.
(Ona pia Yoh 3:19; 8:12; Rom. 13:11, 12; 1 Pet. 2:9.)