Wimbo Na. 148
Ulitoa Mwana Wako Mzaliwa-Pekee
Makala Iliyochapishwa
Yehova, Ee Baba,
ulitukomboa.
Fidia imetupa
tumaini!
Twajitoa kwako,
tutangaze kote.
Wajue mapenzi,
utayatimiza.
(KORASI)
Mwana ulitoa,
Nasi twashukuru,
Tutaimba milele,
Ulitoa mwana wako.
Fadhili, rehema,
Zako zatuvuta.
Twapenda, jinako,
na urafiki.
Ulitoa mwana
wako wa pekee
uzima tupate.
Ni zawadi kubwa.
(KORASI)
Mwana ulitoa,
Nasi twashukuru,
Tutaimba milele,
Ulitoa mwana wako.
(MWISHO)
Yehova, Ee Baba, Twatoa shukrani.
Twasema asante, kutoa mwana wako.
(Ona pia Yoh. 3:16; 1 Yoh. 4:9.)