Wimbo Na. 153
Wewe Unahisije?
Makala Iliyochapishwa
We’ unahisije
kuhubiri kwa bidii,
kuwafikia watu
wanaopendezwa?
Unapofahamu
umetimiza mgawo;
Naye Mungu afanye
kazi kuwavuta.
(KORASI)
Twafurahi kutumia
akili na moyo wote
Tutatoa dhabihu ya sifa
siku zote.
We’ unahisije
wanapoukubali
ujumbe wetu wa uzima
wa milele?
Wasipokubali
bado twauhubiri
Tunafurahi kubeba
jina la Mungu.
(KORASI)
Twafurahi kutumia
akili na moyo wote
Tutatoa dhabihu ya sifa
siku zote.
We’ unahisije
kujua Mungu ndiye
ametukabidhi kazi
tunayofanya?
Tunajivunia
kazi ya kuhubiri.
Tutaendelea
hadi kazi iishe.
(KORASI)
Twafurahi kutumia
akili na moyo wote
Tutatoa dhabihu ya sifa
siku zote.
(Ona pia Mdo. 13:48; 1 The. 2:4; 1 Tim. 1:11.)