Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • ypq swali 5 kur. 15-17
  • Nifanye Nini Ninapoonewa Shuleni?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Nifanye Nini Ninapoonewa Shuleni?
  • Majibu Ya Maswali 10 Ambayo Vijana Huuliza
  • Habari Zinazolingana
  • Nifanye Nini Ninapoonewa?
    Vijana Huuliza
  • Kuacha Udhalimu
    Amkeni!—2003
  • Dhuluma Baadhi ya Visababishi na Matokeo
    Amkeni!—2003
  • Dhuluma Tatizo la Ulimwenguni Pote
    Amkeni!—2003
Pata Habari Zaidi
Majibu Ya Maswali 10 Ambayo Vijana Huuliza
ypq swali 5 kur. 15-17
Mvulana akisumbuliwa na mwoneaji mbele ya wanafunzi wenzake

SWALI LA 5

Nifanye Nini Ninapoonewa Shuleni?

KWA NINI NI MUHIMU

Jinsi unavyotenda huenda kukapunguza au kuongeza uonevu huo.

WEWE UNGEFANYA NINI?

Fikiria hali hii: Thomas hataki tena kwenda shuleni. Si leo, si kesho. Hataki kamwe kurudi shuleni. Tatizo lilianza miezi mitatu iliyopita wanafunzi wenzake walipoeneza porojo mbaya sana kumhusu. Kisha akaanza kupewa majina ya utani. Nyakati nyingine, vijana wenzake huangusha vitabu alivyobeba na kujifanya kana kwamba jambo hilo limetukia bila kukusudia, au kijana mmoja nyuma yake anamsukuma, na kufikia wakati ambapo Thomas anageuka hawezi kutambua ni nani aliyefanya hivyo. Jana, uonevu huo uligeuka ukawa mbaya hata zaidi wakati ambapo Thomas alitishwa kupitia mtandao . . .

Ikiwa ungekuwa Thomas, ungetendaje?

TUA NA UFIKIRI!

Usifikiri kwamba huna uwezo wowote! Kwa kweli, unaweza kukabiliana na mnyanyasaji bila kutumia ngumi. Jinsi gani?

  • USIONYESHE UMECHOKOZEKA. Biblia inasema hivi: “Mtu mjinga huiachilia roho yake yote, lakini mwenye hekima huituliza mpaka mwisho.” (Methali 29:11) Ukitulia, bila kuonyesha umechokozeka, wanaokuonea watachoka.

  • USILIPIZE KISASI. Biblia inasema hivi: “Msimlipe yeyote uovu kwa uovu.” (Waroma 12:17) Kulipiza kisasi kutazidisha tu tatizo, hakutalitatua.

  • JIHADHARI. Biblia inasema hivi: “Mtu mwerevu ni yule ambaye ameona msiba na kujificha.” (Methali 22:3) Kwa kadiri unayoweza, waepuke watu wanaoweza kukuonea au maeneo ambayo unaweza kuonewa.

  • TOA JIBU LISILOTAZAMIWA. Biblia inasema hivi: “Jibu, linapokuwa la upole, hugeuza ghadhabu.” (Methali 15:1) Unaweza hata kutumia ucheshi. Kwa mfano, mwoneaji anaposema kwamba umenenepa kupita kiasi, lipuuze jambo hilo na useme: “Inaonekana ninapaswa kupunguza kilo kadhaa!”

  • ONDOKA. “Kunyamaza kunaonyesha kwamba wewe ni mkomavu na una nguvu kuliko yule mtu anayekusumbua,” anasema Nora mwenye umri wa miaka 19. “Kufanya hivyo kunaonyesha kwamba una uwezo wa kujizuia, lakini yule anayekuonea hana uwezo huo.”—2 Timotheo 2:24.

  • JITAHIDI KUJIAMINI. Mara nyingi, watu wanaowaonea wengine hutambua iwapo mtu hajiamini au hatajitetea. Lakini waoneaji wengi watakuacha wakitambua kwamba huwaruhusu wakuhangaishe.

  • MWELEZE MTU. Mtu mmoja aliyekuwa mwalimu zamani anasema: “Ningemsihi mtu yeyote anayeonewa aseme. Hilo ndilo jambo linalofaa, na huenda likazuia mtu mwingine asionewe.”

Kijana akikabiliana na mwoneaji akiwa na uhakika

Kujiamini kutakupa nguvu ambazo anayekuonea hana

JE, WAJUA?

Mbali na kuumizwa kimwili, kuonewa kunaweza kutia ndani:

  • Maneno yanatoka kama moto kwenye kinywa cha mwoneaji

    Kushambuliwa kwa maneno. “Siwezi kusahau majina waliyoniita au mambo waliyosema. Walinifanya nijihisi sifai, sipendwi, na nihisi kuwa bure kabisa. Afadhali wangenipiga badala ya kuniambia maneno hayo.” —Celine, mwenye umri wa miaka 20.

  • Kijana ameketi peke yake baada ya kutengwa na vijana wenzake

    Kutengwa. “Wanafunzi walianza kuniepuka. Wangenizuia nisiketi nao wakati wa chakula cha mchana kwa kuonyesha kana kwamba meza imejaa. Kwa mwaka mzima, nililia sana na nilikula peke yangu.” —Haley, mwenye umri wa miaka 18.

  • Msichana anasogea kutoka kwenye kompyuta baada ya kuonewa kupitia mtandao

    Kupitia Mtandao. “Kwa kuandika mambo machache tu kwenye kompyuta, unaweza kumharibia mtu sifa kabisa—au hata kuharibu maisha yake. Huenda ukafikiri ninatia chumvi, lakini hilo linaweza kutukia!” —Daniel, mwenye umri wa miaka 14.

MASWALI YANAYOHUSU UONEVU

KWELI AU SI KWELI

MAJIBU

1 Watu wamekuwa wakiwaonea wengine kwa maelfu ya miaka.

1 Kweli. Kwa mfano, Biblia inawataja Wanefili—watu ambao jina lao linamaanisha “Wale Wanaowaangusha Wengine.”—Mwanzo 6:4.

2 Kuwaonea wengine hakuna madhara. Ni mzaha tu.

2 Si kweli. Kuonewa kumechangia vijana wengi sana wajiue.

3 Njia bora ya kumfanya mwoneaji aache kukuonea ni kupambana naye.

3 Si kweli. Mara nyingi, waoneaji huwa na nguvu kuliko wale wanaoonewa, kwa hiyo ni kazi bure kujaribu kupambana naye.

4 Ukiona mtu akionewa, ni vizuri kupuuza jambo hilo.

4 Si kweli. Ukimtazama mtu akionewa bila kusema lolote, una hatia, huenda ukawa unachangia tatizo badala ya kusaidia kulitatua.

5 Mara nyingi waoneaji hawajiamini ingawa wanazungumza kwa majivuno.

5 Kweli. Ingawa waoneaji fulani wana ujasiri, wengi wao hawajiamini nao huwashushia wengine heshima ili kuficha hali hiyo.

6 Waoneaji wanaweza kubadilika.

6 Kweli. Wanapopata msaada, waoneaji wanaweza kubadili njia yao ya kufikiri na tabia yao.

HATUA ZA KUCHUKUA

  • Nitakaposumbuliwa na mwoneaji, nitafanya au kusema nini?

JIFUNZE ZAIDI!

Mshinde Mnyanyasaji Bila Kutumia Ngumi

Tazama kibonzo kwenye ubao chenye kichwa Mshinde Mnyanyasaji Bila Kutumia Ngumi kwenye www.jw.org/sw. (Tafuta kwenye MAFUNDISHO YA BIBLIA > MATINEJA)

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki