Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • lfb somo la 37 uku. 90-uku. 91 fu. 1
  • Yehova Azungumza na Samweli

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Yehova Azungumza na Samweli
  • Masomo Unayoweza Kujifunza Katika Biblia
  • Habari Zinazolingana
  • Samweli Alifanya Yaliyo Sawa
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2008
  • ‘Aliendelea Kukua Akiwa na Yehova’
    Igeni Imani Yao
  • ‘Aliendelea Kukua Akiwa na Yehova’
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2010
  • Samweli aliendelea kufanya mambo mazuri
    Wafundishe Watoto Wako
Pata Habari Zaidi
Masomo Unayoweza Kujifunza Katika Biblia
lfb somo la 37 uku. 90-uku. 91 fu. 1
Samweli akifungua milango ya maskani

SOMO LA 37

Yehova Azungumza na Samweli

Kuhani Mkuu Eli alikuwa na wana wawili ambao walitumikia wakiwa makuhani katika maskani. Mmoja aliitwa Hofni na mwingine Finehasi. Hawakutii amri za Yehova, na waliwatendea watu vibaya sana. Waisraeli walipokuja kumtolea Yehova dhabihu, Hofni na Finehasi walijichukulia nyama bora zaidi. Eli alipata habari kuhusu yale ambayo wanawe walikuwa wakifanya, lakini hakuchukua hatua yoyote. Je, Yehova angeruhusu hali hiyo iendelee?

Ingawa Samweli alikuwa na umri mdogo kuliko Hofni na Finehasi, hakuwaiga. Yehova alipendezwa na Samweli. Usiku mmoja, Samweli akiwa amelala alisikia akiitwa. Aliamka, akakimbia kwa Eli na kumwambia: ‘Mimi hapa!’ Lakini Eli akamwambia: ‘Sikukuita. Rudi ukalale.’ Samweli akarudi kulala. Kisha, akasikia akiitwa tena. Samweli alipoitwa mara ya tatu, Eli alitambua kwamba Yehova ndiye alikuwa akimwita. Alimwambia Samweli kwamba akiitwa tena ajibu hivi: ‘Sema, Yehova. Mtumishi wako anakusikiliza.’

Samweli akimweleza Eli ujumbe kutoka kwa Yehova

Samweli akarudi tena kulala. Kisha, akasikia sauti ikiita: ‘Samweli! Samweli!’ Akajibu: ‘Sema, kwa maana mtumishi wako anakusikiliza.’ Yehova akasema hivi: ‘Mwambie Eli kwamba nitamwadhibu yeye na familia yake. Anajua kwamba wanawe wanafanya mambo mabaya kwenye maskani yangu, lakini hajachukua hatua yoyote.’ Asubuhi iliyofuata, Samweli alifungua malango ya maskani kama ilivyokuwa kawaida yake. Hata hivyo, aliogopa kumweleza kuhani mkuu mambo ambayo Yehova alimwambia. Lakini Eli alimwita na kumuuliza: ‘Mwanangu, Yehova alikwambia nini? Nieleze mambo yote.’ Ndipo Samweli akamweleza kila kitu.

Kadiri alivyoendelea kukua, Yehova aliendelea kuwa pamoja na Samweli. Kutoka mwisho mmoja wa nchi hadi ule mwingine, Waisraeli walijua kwamba Yehova amemchagua Samweli kuwa nabii na mwamuzi.

“Basi, mkumbuke Muumba wako Mkuu katika siku za ujana wako.”​—Mhubiri 12:1

Maswali: Samweli alitofautianaje na Hofni na Finehasi? Yehova alimpa Samweli ujumbe gani?

1 Samweli 2:12-17, 22-26; 3:1-21; 7:6

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki