Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • lfb somo la 72 uku. 170-uku. 171 fu. 2
  • Yesu Akiwa Kijana

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Yesu Akiwa Kijana
  • Masomo Unayoweza Kujifunza Katika Biblia
  • Habari Zinazolingana
  • Alikubali Mwelekezo wa Kimungu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1995
  • Alikuwa Baba na Mume Aliyemwogopa Mungu
    Igeni Imani Yao
  • Aliilinda Familia Yake, Akawaandalia, na Akavumilia
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2012
  • Maisha ya Utotoni Huko Nazareti
    Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
Pata Habari Zaidi
Masomo Unayoweza Kujifunza Katika Biblia
lfb somo la 72 uku. 170-uku. 171 fu. 2
Yesu akiwa na umri wa miaka kumi na miwili ameketi katikati ya walimu hekaluni

SOMO LA 72

Yesu Akiwa Kijana

Yosefu na Maria waliishi Nazareti pamoja na Yesu na wana na binti zao wengine. Yosefu aliitegemeza familia yake kwa kufanya kazi ya useremala, na aliwafundisha kumhusu Yehova na Sheria yake. Familia hiyo ilienda katika sinagogi kwa ukawaida ili kuabudu, na pia jijini Yerusalemu kila mwaka ili kusherehekea Pasaka.

Yesu alipokuwa na umri wa miaka 12, kama ilivyokuwa kawaida yao, familia yao ilifunga safari ndefu kuelekea Yerusalemu. Jiji hilo lilikuwa limejaa watu waliokuwa wamekuja kusherehekea Pasaka. Baadaye, Yosefu na Maria wakaanza safari ya kurudi nyumbani, wakifikiri kwamba Yesu alikuwa akisafiri katika kikundi chao. Lakini walipomtafuta kati ya watu wao wa ukoo, hawakumpata.

Wakarudi Yerusalemu na kumtafuta mwana wao kwa siku tatu. Hatimaye, wakaenda hekaluni. Wakampata hekaluni, akiwa ameketi katikati ya walimu, akiwasikiliza kwa makini na kuwauliza maswali. Walimu hao walipendezwa sana na Yesu hivi kwamba wakaanza kumuuliza maswali. Nao walishangazwa na majibu yake. Waliona kwamba alielewa Sheria ya Yehova.

Yosefu na Maria walipatwa na wasiwasi sana. Maria akasema hivi: ‘Mwanangu, tumekuwa tukikutafuta kila mahali! Ulikuwa wapi?’ Yesu akajibu hivi: ‘Je, hamkujua kwamba ni lazima niwe hapa katika nyumba ya Baba yangu?’

Yesu akaenda nyumbani Nazareti pamoja na wazazi wake. Yosefu alimfundisha Yesu kazi ya useremala. Unafikiri Yesu alikuwa mtu wa aina gani alipokuwa kijana? Alipoendelea kukua, Yesu alifanya maendeleo katika hekima akizidi kupata kibali kwa Mungu na wanadamu.

Yosefu na Maria wakiwa mezani pamoja na Yesu na baadhi ya ndugu na dada zake

“Ee Mungu wangu, ninafurahia kufanya mapenzi yako, na sheria yako imo ndani yangu kabisa.”​—Zaburi 40:8

Maswali: Yosefu na Maria walimkuta wapi Yesu? Kwa nini alikuwa hapo?

Mathayo 13:55, 56; Marko 6:3; Luka 2:40-52; 4:16; Kumbukumbu la Torati 16:15, 16

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki