Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • lfb somo la 92 uku. 214-uku. 215 fu. 1
  • Yesu Awatokea Wavuvi

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Yesu Awatokea Wavuvi
  • Masomo Unayoweza Kujifunza Katika Biblia
  • Habari Zinazolingana
  • Kwenye Ufuo wa Bahari ya Galilaya
    Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
  • Kwenye Bahari ya Galilaya
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1991
  • Kwenye Bahari ya Galilaya
    Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
  • Kutumika Tukiwa Wavuvi wa Watu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1992
Pata Habari Zaidi
Masomo Unayoweza Kujifunza Katika Biblia
lfb somo la 92 uku. 214-uku. 215 fu. 1
Yesu anazungumza na wanafunzi wake huku samaki wakiiva kwenye moto

SOMO LA 92

Yesu Awatokea Wavuvi

Muda fulani baada ya Yesu kuwatokea mitume, Petro aliamua kwenda kuvua samaki katika Bahari ya Galilaya. Tomasi, Yakobo, Yohana, na baadhi ya wanafunzi wengine wakaenda pamoja naye. Walijaribu kuvua samaki usiku kucha lakini hawakupata chochote.

Mapema asubuhi iliyofuata, walimwona mwanamume akiwa amesimama ufuoni. Akawauliza hivi akiwa ufuoni: ‘Je, mmepata samaki wowote?’ Wakamwambia, “Hapana!” Mwanamume huyo akasema, “Utupeni wavu upande wa kulia wa mashua.” Walipofanya hivyo, wavu ukajaa samaki wengi sana hivi kwamba hawakuweza kuuvuta. Mara moja Yohana akatambua kwamba mwanamume huyo alikuwa Yesu, naye akasema: “Ni Bwana!” Papo hapo, Petro akajitumbukiza ndani ya maji na kuogelea hadi ufuoni. Wanafunzi wengine wakamfuata kwa mashua.

Walipofika ufuoni, wakaona mkate na samaki vikipikwa juu ya moto. Yesu akawaambia walete baadhi ya samaki waliowavua wawaongezee kwenye mlo wao. Kisha akawaambia hivi: “Njooni, mpate kiamshakinywa.”

Petro anamfikia Yesu ufuoni na wanafunzi wengine wanamfuata kwa mashua

Baada ya kula kiamshakinywa, Yesu akamuuliza hivi Petro: ‘Je, unanipenda kuliko unavyopenda kuvua samaki?’ Petro akasema, “Ndiyo, Bwana, unajua ninakupenda.” Yesu akamwambia, ‘Basi walishe wanakondoo wangu.’ Yesu akamuuliza tena: ‘Petro, unanipenda?’ Petro akasema, ‘Bwana, unajua ninakupenda.’ Yesu akamwambia, “Chunga kondoo wangu wadogo.” Yesu akauliza mara ya tatu. Petro akahuzunika sana. Akasema, “Bwana, wewe unajua mambo yote; unajua kwamba ninakupenda.” Yesu akasema, “Lisha kondoo wangu wadogo.” Kisha akamwambia Petro hivi: “Endelea kunifuata.”

“[Yesu] akawaambia: ‘Nifuateni, nami nitawafanya muwe wavuvi wa watu.’ Mara moja wakaziacha nyavu zao na kumfuata.”​—Mathayo 4:19, 20

Maswali: Yesu aliwafanyia wavuvi muujiza gani? Unafikiri kwa nini Yesu alimwuliza Petro hivi mara tatu, “Je, unanipenda?”

Yohana 21:1-19, 25; Matendo 1:1-3

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki