Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • lfb somo la 99 uku. 230-uku. 231 fu. 4
  • Mlinzi wa Jela Ajifunza Kweli

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mlinzi wa Jela Ajifunza Kweli
  • Masomo Unayoweza Kujifunza Katika Biblia
  • Habari Zinazolingana
  • “Vuka Uingie Makedonia”
    “Kutoa Ushahidi Kamili” Kuhusu Ufalme wa Mungu
  • Sila—Chanzo cha Kitia-Moyo
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1999
  • “Ni Lazima Mimi Nifanye Nini Nipate Kuokoka?”
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1989
  • ‘Amani ya Mungu Ni Yenye Ubora Unaozidi Fikira Zote’
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2017
Pata Habari Zaidi
Masomo Unayoweza Kujifunza Katika Biblia
lfb somo la 99 uku. 230-uku. 231 fu. 4
Mlinzi wa jela kule Filipi anakuta milango ya gereza ikiwa wazi na wafungwa wakiwa bado ndani

SOMO LA 99

Mlinzi wa Jela Ajifunza Kweli

Huko Filipi, kulikuwa na kijakazi aliyekuwa na roho mwovu. Roho huyo mwovu alimtumia msichana huyo kufanya ubashiri, na msichana huyo alikuwa akiwapatia mabwana zake faida nyingi kwa kufanya kazi hiyo. Paulo na Sila walipofika Filipi, msichana huyo aliendelea kuwafuata kwa siku nyingi. Roho huyo mwovu alimfanya apaze sauti akisema: “Watu hawa ni watumwa wa Mungu Aliye Juu Zaidi.” Mwishowe, Paulo akamwambia huyo roho mwovu: ‘Katika jina la Yesu, ninakuamuru umtoke!’ Roho huyo mwovu akamtoka msichana huyo.

Basi, mabwana zake walipoona kwamba hawawezi tena kupata pesa kupitia msichana huyo, wakakasirika sana. Wakawakokota Paulo na Sila mpaka kwa mahakimu wa raia, wakisema: ‘Watu hawa wanavunja sheria na wanasumbua sana jiji lote!’ Mahakimu hao wakaamuru kwamba Paulo na Sila wapigwe na kutupwa gerezani. Mlinzi wa jela akawatupa katika gereza la ndani zaidi, lenye giza zaidi, na kuifunga miguu yao katika mikatale.

Huku wafungwa wengine wakiwasikiliza, Paulo na Sila walimsifu Yehova kwa wimbo. Ghafla, katikati ya usiku, tetemeko kubwa la ardhi likatokea na kutikisa misingi ya gereza hilo. Milango ya gereza ikafunguka na minyororo na mikatale waliyokuwa wamefungwa ikafunguka. Mlinzi wa jela akaingia haraka ndani ya gereza na kuona kwamba milango ya gereza ilikuwa imefunguka. Akiwazia kwamba wafungwa wote walikuwa wametoroka, akauchomoa upanga ili ajiue.

Wakati huohuo, Paulo akapaza sauti kubwa, akisema: ‘Usijiumize! Sisi sote tupo hapa!’ Mlinzi huyo akaingia ndani na kuanguka chini mbele ya Paulo na Sila. Naye akawauliza: “Nifanye nini ili niokolewe?” Nao wakamwambia: ‘Wewe na watu wa nyumba yako mnahitaji kumwamini Yesu.’ Basi, Paulo na Sila wakawafundisha neno la Yehova, na mlinzi huyo wa jela pamoja na watu wa nyumba yake wakabatizwa.

“Watu watawakamata ninyi na kuwatesa na kuwakabidhi kwenye masinagogi na magereza. Mtapelekwa mbele ya wafalme na magavana kwa sababu ya jina langu. Hivyo, mtapata nafasi ya kutoa ushahidi.”​—Luka 21:12, 13

Maswali: Kwa nini Paulo na Sila walitupwa gerezani? Mlinzi wa jela alipataje kweli?

Matendo 16:16-34

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki