Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w89 9/15 kur. 3-4
  • “Ni Lazima Mimi Nifanye Nini Nipate Kuokoka?”

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • “Ni Lazima Mimi Nifanye Nini Nipate Kuokoka?”
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1989
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • “Mwamini Bwana Yesu”
  • Jambo Ambalo Ni Lazima Tufanye Ili Tuokolewe
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1989
  • Mlinzi wa Jela Ajifunza Kweli
    Masomo Unayoweza Kujifunza Katika Biblia
  • Wokovu—Inachomaanisha kwa Kweli
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1997
  • “Mwamini Yesu”—Je, Kumwamini Yesu Kunatosha Kupata Wokovu?
    Maswali ya Biblia Yajibiwa
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1989
w89 9/15 kur. 3-4

“Ni Lazima Mimi Nifanye Nini Nipate Kuokoka?”

“NI LAZIMA mimi nifanye nini nipate kuokoka?” Swali hili liliulizwa huko nyuma katika mwaka wa 50 W.K. na mlinda-gereza mmoja katika Filipi, Makedonia. Kulikuwa sasa hivi kumetokea tetemeko kubwa la dunia, na milango yote ya gereza alilokuwa akisimamia ilikuwa imevunjika na kufunguka. Akidhani kwamba wafungwa walikuwa wametoroka, yule mlinda-gereza alikuwa karibu kujiua. Lakini mmoja wa wafungwa wale, mtume Paulo, akapaaza sauti: “Usijiumize, kwa maana sisi sote tupo hapa!”—Matendo 16:25-30, NW.

Paulo na mfungwa mwenzake, Sila, walikuwa wamekuja Filipi ili wahubiri ujumbe wa wokovu, nao walikuwa gerezani kwa sababu ya mashtaka bandia yaliyofanywa dhidi yao. Akishukuru kwamba wafungwa hawakutoroka, yule mlinda-gereza alitaka kusikia ujumbe wa Paulo na Sila. Yeye angepaswa kufanya nini ili ashangilie wokovu uliokuwa ukihubiriwa na wamisionari hawa wawili Wakristo?

Leo watu wangali wanahitaji wokovu ambao Paulo na Sila walikuwa wakihubiri. Ingawa hivyo, jambo lisilofurahisha ni kwamba watu wengi wanatilia mashaka sana jambo hili la kuokolewa. Wao wanachukizwa na majivuno na tamaa ya kupata mali ya wale wanadini ambao wanajidai kuwafundisha jinsi ya kuokolewa. Wengine wanashtushwa na misisimuko isiyo ya kiakili ya hisia za moyoni ambazo ni tabia ya dini za kievanjeli zinazokazia wazo la wokovu. Mwandikaji wa jarida Mwingereza Philip Howard alisema kwamba hawa wanaojiita waevanjeli ati “huchochea misisimuko ya watu ya hisia za moyoni na kuwafanya watie sahihi katika hundi zao za pesa badala ya kuvuta fikira za wasikilizaji wao.”—Linganisha 2 Petro 2:2.

Bado wengine wanagutushwa na mabadiliko ambayo nyakati fulani hutokea katika watu mmoja mmoja wanaoamini kwamba wamepata ono la “kuokolewa.” Katika kitabu chao Snapping, Flo Conway na Jim Siegelman wanazungumzia maono mengi ya kidini—kutia na “kuokolewa”—ambayo yalivuma sana miongo michache iliyopita. Wanaandika juu ya “upande usio na mafaa” wa maono haya na kusema kwamba watu “wanaingizwa ghafula” katika mabadiliko ya nyutu ambayo yanakosa kuwapa utimizo na elimu iliyoahidiwa bali wanakuja kuzinduka kuwa wamedanganywa, wanafunga akili zao zisitake kupokea mawazo mapya, na kutoweza kukabili uhalisi wa maisha. Watungaji hao wanaongeza hivi: “Tunaweza kuueleza mwendo huo kuwa ule wa kufunga akili, wa kutofikiri.”

Haikuwa hivyo Wakristo wa karne ya kwanza walipookolewa. Mlinda-gereza Mfilipi ‘hakufunga akili zake’ wakati mtume Paulo alipojibu swali lake, “Ni lazima mimi nifanye nini nipate kuokoka?” Na Paulo na Sila hawakurukia ‘kuchochea hisia zake za moyoni’ na kumsihi awape mchango mkubwa wa kifedha. Bali, ‘walimwambia neno la Yehova.’ Kwa kusababu na mwanamume huyo, walimsaidia apate ufahamu ulio waziwazi wa maandalizi ya Mungu kwa ajili ya wokovu.—Matendo 16:32.

“Mwamini Bwana Yesu”

Wale wamisionari Wakristo walifungua akili za mlinda-gereza yule zipate ukweli wa msingi juu ya wokovu. Ulikuwa ukweli ule ule ambao mtume Petro alieleza wakati kundi la Kikristo lilipoanzishwa mara ya kwanza. Petro alielekeza kwenye daraka kuu la Yesu Kristo kwa habari ya wokovu, akimwita “Wakili Mkuu wa uhai.” Mtume huyo alisema hivi pia: “Hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.” (Matendo 3:15, NW; 4:12) Paulo na Sila walimwelekeza mlinda-gereza Mfilipi kwa Wakili huyo huyo wa wokovu waliposema: “Mwamini Bwana Yesu, nawe utaokoka.”—Matendo 16:31.

Ingawa hivyo, inamaanisha nini kumwamini Bwana Yesu? Kwa nini hakuna jina jingine isipokuwa lile la Yesu ambalo kwalo tunaweza kuokolewa? Je! hatimaye kila mtu atafikia wokovu? Je! mitume waliamini lile wazo la kusema “ukiisha okolewa, umeokolewa daima”? Haya ni maswali ya maana kwa sababu, ijapokuwa ni hakika kwamba maneno na matendo ya wanadini wengi wa ki-siku-hizi yameelekea kupunguza uzito wa neno hilo, tungali tunahitaji wokovu. Sisi sote tunahitaji jibu lenye kutosheleza, lililo la kiakili kwa swali hili: “Ni lazima mimi nifanye nini nipate kuokoka?”

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki