WIMBO NA. 21
Endeleeni Kuutafuta Kwanza Ufalme
Makala Iliyochapishwa
1. Ufalme wa Kristo Yesu,
Utakaotawala,
Ni wenye thamani sana,
Mbele zake Yehova.
(KORASI)
Tafuta Ufalme kwanza,
Pia uadilifu.
Mwimbieni Mungu sifa,
Na kumtumikia.
2. Msihangaishwe sana,
Na chakula, mavazi.
Mungu ataturuzuku,
Tukiutanguliza.
(KORASI)
Tafuta Ufalme kwanza,
Pia uadilifu.
Mwimbieni Mungu sifa,
Na kumtumikia.
3. Ufalme utangazeni;
Saidieni watu,
Wamtumaini Mungu,
Na utawala wake.
(KORASI)
Tafuta Ufalme kwanza,
Pia uadilifu.
Mwimbieni Mungu sifa,
Na kumtumikia.
(Ona pia Zab. 27:14; Mt. 6:34; 10:11, 13; 1 Pet. 1:21.)