WIMBO NA. 45
Kutafakari kwa Moyo Wangu
Makala Iliyochapishwa
1. Mambo nitafakariyo;
Nayo mawazo ya moyo,—
Bwana, na yakupendeze,
Nitembee nawe Bwana.
Kila ninapolemewa,
Nikosapo usingizi,
Nikutafakari wewe,
Na mambo yaliyo mema.
2. Mambo safi na ya kweli,
Wema adili wowote,
Mambo yasemwayo vema—
Niyatafakari hayo
Mawazo yako ni bora!
Kamwe hayahesabiki.
Mungu nitatafakari,
Neno Lako sikuzote.
(Ona pia Zab. 49:3; 63:6; 139:17, 23; Flp. 4:7, 8; 1 Tim. 4:15.)