WIMBO NA. 68
Kupanda Mbegu ya Ufalme
Makala Iliyochapishwa
1. Njo’ni kwenye kazi ya Bwana,
Tiini mwito wa Kristo.
Yu tayari kuwaongoza,
Msikilizeni yeye.
Mbegu ya kweli inazo nguvu,
Za kukua mioyoni.
Hivyo tieni bidii shambani;
Timizeni kazi ya Bwana.
2. Mafanikio mpatayo,
Yawategemea ninyi.
Wasaidieni wengine,
Wapende kweli na haki.
Wasaidieni kuishinda,
Mikazo na changamoto.
Nanyi mtapata shangwe mwonapo,
Ongezeko siku kwa siku.
(Ona pia Mt. 13:19-23; 22:37.)