Wimbo Na. 98
Kupanda Mbegu za Ufalme
Makala Iliyochapishwa
1. Njooni watumwa wa Mungu,
Muliojiweka wakfu.
Fanyeni kazi ya Bwanetu,
Fwateni hatua zake.
Mbegu zipandeni bila woga,
Moyoni penye rutuba.
Mungu asifiwe kwa kazi yenu;
Tieni bidii shambani.
2. Kati ya mbegu mupandazo,
Zaanguka miambani.
Japo zachipuka haraka,
Hazina mizizi hata.
Miiba na pupa huzisonga,
Waupenda ulimwengu.
Nyingine zitamea na kuzaa,
Katika udongo muzuri.
3. Na mafanikio shambani,
Yawategemea ninyi.
Onyesha subira, upendo,
Jueni mioyo yao.
Waondoleeni wasiwasi,
Fanyeni yote mwezayo.
Kwa shangwe twatumaini kuvuna,
Thelathini na hata mia.
(Ona pia Mt. 13:19-23; 22:37.)