WIMBO NA. 104
Roho Takatifu—Zawadi Kutoka kwa Mungu
Makala Iliyochapishwa
1. Baba Yehova, mwenye rehema
Mioyo yetu waijua.
Tuondolee mahangaiko,
Tupe faraja ya roho yako.
2. Twakukosea mara kwa mara.
Tu wanadamu wenye dhambi.
Mungu twaomba: Tunakusihi,
Utuongoze kwa roho yako.
3. Tunapochoka, na kulemewa,
Roho yako yatuinua.
Tutakimbia, hatutachoka.
Tupe roho yako takatifu.
(Ona pia Zab. 51:11; Yoh. 14:26; Mdo. 9:31.)