WIMBO NA. 117
Sifa ya Wema
Makala Iliyochapishwa
1. Yehova Mungu wa Wema,
Twaona wema wako.
Wewe ni mtakatifu,
Njia zako ni njema.
Watuonyesha fadhili
Tusizozistahili.
Unastahili ibada,
Ndiwe twatumikia.
2. Watu wako waonyesha,
Sifa ya wema wako,
Katika mwenendo wao,
Na wanapohubiri.
Mafundisho yako mema,
Yawachochea wengi.
Twakuomba roho yako,
Tuwe wema daima.
3. Ubariki wema wetu,
Kwa ndugu zetu wote.
Tuonyeshe watu wote,
Fadhili zako Mungu.
Familia, Kutaniko,
Mijini, vijijini.
Bariki juhudi zetu,
Tuwe wema milele.
(Ona pia Zab. 103:10; Marko 10:18; Gal. 5:22; Efe. 5:9.)