WIMBO NA. 143
Endeleeni Kufanya Kazi, Kesheni, na Kusubiri
Makala Iliyochapishwa
1. Mweka majira, nyakati,
Anayeitwa Yehova—
Wakati wa kutetewa,
Uko karibu sana.
(KORASI)
Endeleeni kufanya kazi,
Kesheni na kusubiri,
Baraka za Ufalme.
2. Wakati umeshawekwa,
Mwana wake yu tayari.
Kwa ajili ya pigano,
Dhidi ya wapinzani.
(KORASI)
Endeleeni kufanya kazi,
Kesheni na kusubiri,
Baraka za Ufalme.
3. Japo sote twaugua,
Tunasubiri kwa hamu.
Ije siku ya Yehova,
Tuachiliwe huru.
(KORASI)
Endeleeni kufanya kazi,
Kesheni na kusubiri,
Baraka za Ufalme.
(Ona pia Mt. 25:13; Luka 12:36.)