Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • lmd somo la 4
  • Unyenyekevu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Unyenyekevu
  • Wapende Watu—Fanya Wanafunzi
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Paulo Alifanya Nini?
  • Tunajifunza Nini Kutoka kwa Paulo?
  • Mwige Paulo
  • Kwa Nini Kujivika Unyenyekevu?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1991
  • Yehova Anawathamini Watumishi Wake Wanyenyekevu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2019
  • Vielelezo vya Unyenyekevu vya Kuiga
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1993
  • Sitawisha Unyenyekevu wa Kweli
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2005
Pata Habari Zaidi
Wapende Watu—Fanya Wanafunzi
lmd somo la 4

KUANZISHA MAZUNGUMZO

Mtume Paulo akiwa amefungwa mnyororo pamoja na mlinzi, anazungumza kwa heshima na Mfalme Agripa, Gavana Festo, na Bernike.

Matendo 26:​2, 3

SOMO LA 4

Unyenyekevu

Kanuni: “Kwa unyenyekevu mwaone wengine kuwa bora kuliko ninyi.”—Flp. 2:3.

Paulo Alifanya Nini?

Mtume Paulo akiwa amefungwa mnyororo pamoja na mlinzi, anazungumza kwa heshima na Mfalme Agripa, Gavana Festo, na Bernike.

VIDEO: Paulo Anamhubiria Mfalme Agripa

1. Tazama VIDEO, au soma Matendo 26:​2, 3. Kisha fikiria maswali yafuatayo:

  1. Paulo alionyeshaje unyenyekevu kwa jinsi alivyozungumza na Mfalme Agripa?

  2. Paulo alimkaziaje fikira Yehova na Maandiko? —Ona Matendo 26:22.

Tunajifunza Nini Kutoka kwa Paulo?

2. Tukizungumza kwa unyenyekevu na heshima, ujumbe wetu utavutia zaidi.

Mwige Paulo

3. Zungumza kwa heshima. Epuka mtazamo wa kujionyesha kwamba unajua kila kitu na mtu unayezungumza naye hajui chochote.

4. Onyesha wazi kwamba msingi wa kweli unazofundisha ni Biblia. Neno la Mungu lina mawazo yanayogusa mioyo ya watu. Tunapolitumia, tunajenga imani yao katika msingi unaofaa.

5. Endelea kuwa mpole. Usijaribu kuendelea kuthibitisha kwamba uko sahihi. Hatutaki kubishana na watu. Onyesha unyenyekevu kwa kuwa mtulivu na kutambua wakati wa kuondoka. (Met. 17:14; Tito 3:2) Ukizungumza kwa upole, huenda mtu huyo akasikiliza ujumbe wetu wakati ujao.

SOMA PIA

Rom. 12:​16-18; 1 Kor. 8:1; 2 Kor. 3:5

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki