Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • it uku. 724
  • Raba

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Raba
  • Ufahamu wa Kina wa Maandiko
  • Habari Zinazolingana
  • Waamoni—Watu Waliorudisha Uhasama kwa Fadhili
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1995
  • Kitabu Cha Biblia Namba 10—2 Samueli
    “Kila Andiko, Lenye Pumzi ya Mungu, Lafaa”
Ufahamu wa Kina wa Maandiko
it uku. 724

RABA

(Raba) [Nyingi; Tele].

1. Jiji lililokuwa ukingoni kabisa upande wa Magharibi mwa ufalme wa kale wa Amoni baada ya eneo hilo kuchukuliwa na Waamori. Raba ndio jiji pekee la ufalme wa Waamoni ambalo linatajwa kwa jina katika masimulizi ya Biblia, hivyo inawaziwa kwamba lilikuwa jiji kuu. Lilikuwa kilomita 37 Mashariki mwa Yordani. Jiji hilo lilikuwa karibu na kijito kilichojiunga na Mto Yaboki na hivyo lilinufaika na rutuba ya eneo hilo. Pia, lilikuwa jiji muhimu kibiashara kwa kuwa lilikuwa katikati ya Damasko na Arabia.

“Jiji la Waamoni la Raba” (Rab·bathʹ benehʹ ʽAm·mohnʹ) linatajwa kwa mara ya kwanza katika Biblia kuwa mahali ambapo jeneza la chuma la Ogu, mfalme wa Bashani, lilikuwa. (Kum 3:11) Waisraeli walipokuja katika Nchi ya Ahadi, kabila la Gadi lilipewa nchi ya Waamori (inaonekana mwanzoni ilikuwa ya Waamoni) “hadi Aroeri, mbele ya [labda Kask. Mash. mwa] Raba.”​—Yos 13:25.

Lilitekwa na Daudi. Jiji hilo linatajwa tena kulipotokea vita vilivyosababishwa na Mfalme Hanuni alipowatendea vibaya wajumbe wa Daudi. (2Sa 10:1-19; 1Nya 19:1-19) Yoabu na vikosi vyake walipigana na Wasiria waliokuwa wamekodiwa na Waamoni, huku Waisraeli wakiongozwa na Abishai wakawashambulia Waamoni “kwenye lango la jiji,” inaelekea ni Raba. (1Nya 19:9) Wasiria waliposhindwa, Waamoni walikimbilia jijini. Majira ya kuchipua yaliyofuata, Yoabu na jeshi lake wakalizingira jiji la Raba. Ni wakati wa kampeni hiyo ambapo Daudi alifanya dhambi na Bath-sheba huko Yerusalemu. Mfalme alimtuma Uria, mume wa Bath-sheba arudi vitani, na kulingana na maagizo ya Daudi, Uria aliwekwa katika mstari wa mbele vitani. Baadhi ya Waamoni waliposhambulia kutoka Raba, vita vilifanya Uria akaribie ukuta na ikawa rahisi kuuawa na wapiga mishale waliokuwa juu ya ukuta.​—2Sa 11:1-25; 1Nya 20:1.

Baada ya muda, Yoabu alifanikiwa katika vita vyake dhidi ya Raba kufikia hatua ya kuliteka “jiji lenye maji.” (2Sa 12:27) Kwa kuwa Yoabu alimweleza Daudi hali ilivyokuwa ili mfalme aje na kukamilisha ushindi na apokee sifa kwa kuliteka jiji la Raba, inaonekana Yoabu aliteka sehemu fulani tu ya jiji hilo. Huenda maneno “jiji lenye maji” yalirejelea sehemu fulani iliyo kwenye ukingo wa mto, tofauti na sehemu nyingine za jiji, au huenda aliteka vyanzo vikuu vya maji vya jiji hilo.​—2Sa 12:26-28.

Daudi alikuja na kukamilisha ushindi wake juu ya jiji la Raba, na “alichukua pia nyara nyingi sana kutoka katika jiji hilo.” (2Sa 12:29-31; 1Nya 20:2, 3) Baadaye, Waamoni wakawa huru tena. Katika karne ya tisa K.W.K., Amosi alitabiri hukumu juu ya Waamoni na akataja kihususa kwamba Raba lingeteketezwa. (Amo 1:13, 14) Yeremia na Ezekieli waliwasilisha jumbe dhidi ya Raba. Kama inavyoonyeshwa chini ya kichwa WAAMONI, inaonekana unabii huo ulitimizwa katika siku za Nebukadneza.​—Yer 49:2, 3; Eze 21:19-23; 25:5.

Katika karne ya tatu K.W.K., Ptolemy Philadelphus alijenga upya jiji la Raba na kuliita Filadelfia. Baadaye lilitiwa ndani miongoni mwa majiji ya Dekapoli na inaonekana lilikuwa jiji imara na lenye ufanisi mkubwa. Jiji la kisasa la ʽAmman limejengwa hapo, na bado kuna magofu mengi ya kale, kutia ndani ukumbi mkubwa wa maonyesho, lakini mengi ya magofu hayo ni ya siku za Waroma.

2. Moja ya majiji ambayo kabila la Yuda lilipewa wakati wa kugawa maeneo. Haijulikani kihususa mahali lilipokuwa. Kwenye Yoshua 15:60 limeorodheshwa pamoja na Kiriath-yearimu ambalo lilikuwa katika nchi yenye milima ya Yuda, kilomita 13 Magh. Kask. Magh mwa Yerusalemu.

[Picha katika ukurasa wa 724]

Magofu katika jiji la ʽAmman, mahali ambapo Raba la kale la Amoni lilikuwa, na baadaye Filadelfia ya Dekapoli

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki