Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w74 5/1 kur. 195-197
  • Je! Mungu wa Upendo Angeweza Kutesa Nafsi?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je! Mungu wa Upendo Angeweza Kutesa Nafsi?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1974
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • MUNGU HAZUII ADHABU
  • Alijifunza Kuwa Mwenye Rehema
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2009
  • Alijifunza Kuwa Mwenye Rehema
    Igeni Imani Yao
  • Yona Ajifunza Juu ya Rehema ya Yehova
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1996
  • Kitabu Cha Biblia Namba 32—Yona
    “Kila Andiko, Lenye Pumzi ya Mungu, Lafaa”
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1974
w74 5/1 kur. 195-197

Je! Mungu wa Upendo Angeweza Kutesa Nafsi?

SIFA iliyo kuu ya Muumba wa mwanadamu ni upendo. Yeye ndiye aliye mfano bora wa upendo. Ndiyo sababu Biblia inasema: “Mungu ni upendo.” (1 Yohana 4:16) Juu ya Mungu huyu mwenye upendo, mtunga zaburi Daudi aliimba: “Kuwa chini ya hasira yake ni kwa kitambo, kuwa chini ya nia njema yake ni kwa muda wa maisha yote.”​—Zab. 30:5, NW.

Kadiri ya upendo wa Mungu kwa wanadamu i wazi kutokana na maoni yake juu ya wale wanaoziasi sheria zake. Yajapokuwa matendo yao ‘yanamwudhi’ na kumtia uchungu,’ yeye hawaki kwa hasira mara ile ile. (Zab. 78:38-41, NW) Yeye anatoa nafasi kwao kwa rehema wazigeuze njia zao, kwa maana yeye hafurahii kufikiliza hukumu mbaya juu yao. Kupitia kwa nabii wake Ezekieli aliwaambia Israeli waasi: “Sikufurahii kufa kwake mtu mwovu; bali aghairi mtu mwovu, na kuiacha njia yake mbaya, akaishi. Ghairini, ghairini, mkaache njia zenu mbaya; mbona mnataka kufa, Enyi nyumba ya Israeli?” (Eze. 33:11) Akiuona uhai kama wenye ubora mwingi, Yehova Mungu anahakikisha kwamba wale wanaozivunja sheria zake za haki wanapewa onyo.

Mfano mmoja ni Ninawi, mji mkuu wa Ashuru ya kale. Kama habari zinavyoonyeshwa katika Biblia, wakaaji wa mji huo walipata kuwa waovu sana kwamba Yehova akakusudia kuwaharibu. Hata hivyo, aliwapa nafasi ya kuyaacha maovu yao. Kwa upendo wake usio na mpaka na rehema alimpeleka nabii Yona kwao. “Baada ya siku arobaini Ninawi utaangamizwa,” ndilo lililokuwa tangazo lenye kushtua la nabii wa Yehova.​—Yona 3:4.

Waninawi walijua kwamba walikuwa wamejifanyia kumbukumbu baya. Dhamiri yao waliyopewa na Mungu iliwalaumu. Wajapokuwa hawakuwa waabudu wa Yehova Mungu, hata hivyo waliiogopa miungu. Kwa hiyo walipomsikia mgeni, ambaye hakuonekana kupendezwa nao, akiutangaza uharibifu wao unaokuja kwa ujasiri, Waninawi walishtuka sana. Mji mzima, pamoja na mfalme, ulitubu kwa kujivika magunia na kujipaka majivu.

Kwa rehema Mungu wa upendo aliwaachilia Waninawi wenye kutubu wasipatwe na mabaya ambayo nabii wake alikuwa ametangaza juu yao. Yona alishangaa sana. Kwa kweli, alikasirika. Aliuacha mji na kujijengea kibanda upande wa mashariki ya Ninawi. Huko akakaa akingoja aone kitakachoupata mji.​—Yona 4:1-5.

Ili Yona apate kuufahamu unyofu wa kuachiliwa kwa Waninawi wenye kutubu na Mungu, Yehova alichagua kumfundisha kwa njia ya somo lenye maana yenyewe. Akafanya mtango umee kwa mwujiza na kumtolea Yona uvuli mzuri katika kibanda chake. Nyumaye, Yehova akaweka buu liutafune mmea huu, likiunyausha. Kwa kunyimwa uvuli wa mmea, Yona aliwekwa chini ya upepo wa mashariki wenye kuunguza nalo jua lenye joto jingi likimpiga kichwani. Bila shaka alianza kushangaa sababu gani mmea ulinyauka, zaidi kwa kuwa ulikuwa umekuwa baraka kubwa kwake. Ajapokuwa Yona hakuwa wala ameupanda wala kuutunza, aliusikitikia mmea; ilielekea kuwa vibaya kwamba ulinyauka mapema sana.​—Yona 4:6-10.

Hata hivyo, Yehova Mungu alikuwa nayo sababu kubwa zaidi ya kuusikitikia Ninawi. Ubora wa wakaaji wake na wanyama wa kufugwa ulikuwa mwingi zaidi kuliko ule wa mtango mmoja. Akilitumia somo lenye maana yenyewe, Yehova alimwuliza Yona: “Na mimi, je! haikunipasa kuuhurumia Ninawi, mji ule mkubwa; ambao ndani yake wamo watu zaidi ya mia na ishirini elfu, wasioweza kupambanua katika mkono wao wa kulia na mkono wao wa kushoto; tena wamo wanyama wa kufugwa wengi sana?”​—Yona 4:11.

Je! ni jambo la busara kuazimia kwamba Mungu mwenye huruma hivyo kwa wanadamu angeweza kuwatesa wengine wao kufuata kifo chao, katika hell yenye moto kwa umilele wote? Ikiwa Yehova Mungu hakifurahii kifo cha waovu, awezaje kweli kufurahia kuona watu wakipatwa na maumivu makali zaidi sana kwa umilele wote?

Wakati Waisraeli walipokuwa wakijitia katika mazoea yenye uasi ya kutoa watoto kama dhabihu, Yehova alimwambia hivi nabii wake Yeremia: “Nao wamepajenga mahali palipoinuka pa Tofethi, palipo katika bonde la mwana wa Hinomu, ili kuwateketeza wana wao na binti zao motoni; jambo ambalo mimi sikuliagiza, wala halikuingia moyoni mwangu.” (Yer. 7:31) Ikiwa mazoea yenye kuchukiza ya kutoa watoto kama dhabihu yalikuwa kitu kisichowazika na Mungu wa upendo, angewezaje kweli kuwaza juu ya mateso ya milele kwa wanadamu wanaozivunja sheria zake?

MUNGU HAZUII ADHABU

Hii maana yake si kwamba Yehova Mungu ataachilia kutenda maovu bila ya kuadhibiwa, kwamba yeye anakaa kana kwamba haoni uvunjaji mbaya sana wa amri zake. Neno lake Yeye latangaza: “[Yehova] ni Mungu mwenye wivu, naye hujilipiza kisasi; [Yehova] hujilipiza kisasi, naye ni mwingi wa hasira; [Yehova] hujilipiza kisasi juu ya adui zake, huwawekea adui zake akiba ya hasira. [Yehova] si mwepesi wa hasira, ana uweza mwingi, wala hatamhesabia mtu mwovu kuwa hana hatia kamwe.” (Nah. 1:2, 3) “Yeye ni mwenye hekima moyoni, na mwenye uwezo katika nguvu; ni nani aliyejifanya kuwa mgumu juu yake, naye akafanikiwa?” (Ayubu 9:4) Hata wale wanaojidai kuwa watu wake lakini wakijifanya wenye hatia ya uasi hawatalindwa wasidhurike, ndiyo, wasiteseke.

Ikiwa mtu anajaribu kuficha dhambi yake, Mungu hatamwacha asipatwe na matokeo yenye kutesa ya dhamiri yenye hatia. Mtu aliyeona hivi alikuwa Daudi. Yeye aliandika: “Niliponyamaza mifupa yangu ilichakaa kwa kuugua kwangu mchana kutwa. Kwa maana mchana na usiku mkono wako ulinilemea. Jasho langu likakauka hata nikawa kama nchi kavu wakati wa kaskazi.”​—Zab. 32:3, 4.

Kunyamazisha dhamiri yenye hatia kulimchosha Daudi. Huzuni kuu kwa sababu ya alichokuwa amekifanya ilizifanya nguvu zake kuwa kama vile mti unavyoweza kupoteza unyevu wenye kutoa uhai mnamo joto kali sana la hari. Lakini, mateso yaliyompata Daudi yalitokeza matokeo mema. Yalimvuta aiungame dhambi yake na kurudisha ujamaa ufaao na Mungu wake.

Hata adhabu iliyo kali zaidi sana ambayo Yehova Mungu huenda akaweka watu chini yake ni yenye kusudi. Yaweza kuwafanya wawe bora. Yehova Mungu hamtaabishi ye yote kamwe kwa ajili ya kujipatia raha yake mwenyewe. Yeye hafurahii kuadhibu kama vile baba mwenye upendo asivyofurahia kuadhibu katika kushughulika na mtoto asiyetii. Akionyesha kusudi la kuadhibu kwake, Yehova alitangaza hivi kupitia kwa nabii wake Isaya:

“Je! mwenye kulima alima daima, ili apande? afunua daima madongoa ya nchi yake, na kuyavunja? Akiisha kuulainisha uso wa nchi yake, je! hamwagi huko na huko kunde, na kutupa-tupa jira, na kuitia ngano safu safu, na shayiri mahali pake palipochaguliwa, na kusemethi karibu na mipaka yake? Kwa maana Mungu wake anamwagiza vizuri na kumfundisha. Kwa maana kunde zile hazipurwi kwa chombo kikali, wala gurudumu la gari halipitishwi huko na huko juu ya jira ile, bali kunde zile hupurwa kwa fimbo, na jira ile kwa ufito. Ngano ya mkate husagwa; kwa maana haipuri sikuzote bila kukoma; na ingawa gurudumu la gari lake na farasi wake huitawanya ngano ile, haisagi. Hayo nayo yatoka kwa [Yehova] wa majeshi, mwenye shauri la ajabu, apitaye wote kwa hekima yake.”​—Isa. 28:24-29.

Kulima na kuvuna ni kwenye kikomo. Ugumu wa udongo ndio unaoamua kadiri ya kulima. Namna ya nafaka ndiyo inayoamua nguvu na uzito wa vyombo vilivyotumiwa kwa kutwanga. Vivyo hivyo, Yehova Mungu hawaadhibu wale wanaoiasi sheria yake kwa umilele. Yeye anawaadhibu zaidi awalainishe, awafanye wawe wenye kupokea mashauri yake zaidi na uongozi. Hii yaionyesha hekima ya Mungu katika kusafisha watu, kuondosha tabia zisizopendeza kwa njia ya tendo linalofaa zaidi sana kwa hali zilizoko.

Nyakati nyingine kile ambacho Yehova Mungu anaruhusu kiwajie watu mmoja mmoja chaweza kuwa mateso kweli kweli kwao. Huenda kikafunua njia zao mbaya kwa maumivu. (Linganisha Ufunuo 11:10.)

Wale wanaoshindwa kuyasikiliza mashtaka ambayo Yehova Mungu ameyatangaza katika kinywa cha watumishi wake wanapatwa na matokeo yenye kutesa ya ujumbe wenyewe. Wanazikosa baraka ambazo zingewajia kama wangetubu na kuzigeuza njia zao. Lakini, hata katika habari yao, mateso yanatimiliza kusudi fulani. Yafunua wazi kwamba wao hawastahili kuachiliwa hukumu ya Mungu isifikilizwe juu yao.

Lakini je! yaweza kusemwa kwamba mateso ya milele yangekuwa yenye kufaa? Kama Yehova Mungu angeweka wanadamu chini ya mateso ya milele, je! wenye kuteswa wangefaidika? Bila shaka sivyo. Hata kama wangetaka, wasingeweza kuwa watu walio bora wala kuitengeneza hali yao. Halafu, tena, Muumba asingefaidika hata kidogo kutokana na kuwatesa kwa umilele. Ingemlazimu tu kufanya jambo fulani asilotaka kulifanya, yaani, kutazama mateso ya sikuzote, mateso yasiyo na kusudi jema kwa ajili ya mtu anayepasishwa bila ya uwezekano wo wote wa kutulizwa. Nabii Habakuki aliandika hivi juu ya Mungu: “Wewe u safi mno machoni usiweze kutazama mabaya; wala kutazama taabu huwezi wewe.” (Hab. 1:13, NW) Mungu awezaje basi, kuitazama huzuni kuu ya wale walioiasi sheria yake kwa umilele wote?

Kwa kweli haiwaziki kwamba Mungu wa upendo angeweza kufanya jambo linalotofautiana kabisa na utu wake, njia na matendo.

Lakini, yaweza kuulizwa, Je! huu ndio ushuhuda wa pekee juu ya fundisho la mateso ya milele? Je! hakuna ushuhuda wa kuonyesha kwamba kitu fulani kinaokoka mwili unapokufa? Je! kuwako kwa mtu akiwa mwenye ufahamu hakuendelei nyuma ya kifo? Kwa hiyo je! kutakuwako mateso kwa kile ambacho kinaokoka mwili unapokufa? Ili upate jibu kwa maulizo haya, twakukaribisha ujifunze Biblia pamoja na mashahidi wa Yehova.

[Picha katika ukurasa wa 196]

Wakati Waisraeli walipojitia katika kutoa watoto kama dhabihu, Mungu alionyesha katazo lake, akisema hakuwa ameliagiza hili na kwamba ‘halikuingia moyoni mwake’

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki