Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w74 4/15 kur. 188-190
  • Sababu kwa Nini Waweza Kuamini Katika Ufufuo

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Sababu kwa Nini Waweza Kuamini Katika Ufufuo
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1974
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • NINI KITAKACHOFUFULIWA?
  • Ufufuo—wa Nani, na Wapi?
    Unaweza Kuishi Milele Katika Paradiso Duniani
  • Tumaini la Ufufuo Ni Hakika!
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2000
  • Ufufuo wa Yesu​—Kwa Nini Ni Muhimu Kwetu?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2014
  • Tumaini la Ufufuo Lina Nguvu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2000
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1974
w74 4/15 kur. 188-190

Sababu kwa Nini Waweza Kuamini Katika Ufufuo

MAMILIONI leo hayaamini katika ufufuo. Wengine hata wanajivunia kutokuwa kama watu ambao, kulingana na makadirio yao, ni wajinga vya kutosha kuweza kuamini katika jambo lisilo na maana kama kufufuliwa kwa wafu. Lakini je! kutokuamini kwao kunafanya iwe vyepesi zaidi kwao kupambana na tumaini la kufa? Je! kunawapunguzia huzuni wakati wapendwa wao wanapokufa? Je! wasingekuwa afadhali zaidi kama wangekuwa na tumaini hakika la kuishi tena na kuwaona wapendwa waliokufa wakiishi tena? Je! tumaini hilo hakika lawezekana?

Kwa mtu anayeamini kwamba Mungu yuko, si vigumu kuamini katika ufufuo. Ni jambo la busara kwake kuazimia kwamba Yeye aliyeuanzisha uhai wa kibinadamu hapo kwanza vile vile ni mwenye hekima vya kutosha kuweza kuwafufua wafu, kuwaumba tena wanadamu waliokufa. Yeye huyu, Yehova Mungu, ameahidi ufufuo au kuumba kupya naye akahakikisha kwamba ahadi zake zinategemeka.

Karne nyingi zilizopita, kwa habari ya Ibrahimu na Sara, Yehova Mungu alifanya mwujiza unaolingana na ufufuo. Haukuwapo uwezekano wo wote wa kibinadamu kwa Sara kuweza kuzaa mwana, kwa maana alikwisha kuacha kuingia mwezini. (Mwa. 18:11) Naye Ibrahimu alikuwa tasa asiweze kupata watoto. Na hali lisilowezekana kwa kibinadamu lilitukia. Yehova Mungu alizirudisha nguvu za uzazi za Ibrahimu na Sara, kwa njia hiyo akiuhifadhi ukoo wa Ibrahimu kupitia kwa mke wake mpendwa Sara. Juu ya mwujiza huu, barua iliyoongozwa na roho ya Mungu kwa Waebrania yasema: “Kwa imani hata Sara mwenyewe alipokea uwezo wa kuwa na mimba, alipokuwa amepita wakati wake; kwa kuwa alimhesabu yeye aliyeahidi kuwa mwaminifu. Na kwa ajili ya hayo wakazaliwa na mtu mmoja, naye alikuwa kama mfu, watu wengi kama nyota za mbinguni kwa wingi wao.”​—Ebr. 11:11, 12.

Jambo la ajabu mno kama kurudishwa kwa nguvu za uzazi za Ibrahimu na Sara kulivyokuwa, Yehova Mungu alifanya miujiza hata mingine inayotoa mifano yenye kutia imani nguvu juu ya uwezo wake wa kufufua. Yeye aliwapa wengine wa watumishi wake waliojitoa uwezo wa kufanya ufufuo wenyewe. Nabii Eliya alimfufua mwana wa pekee wa mjane katika Sarepta. (1 Fal. 17:21-23) Mrithi wake nabii Elisha alimfufua mwana wa pekee wa mwanamke aliyejulikana sana, aliyekuwa mkaribishaji mwema katika Shunami. (2 Fal. 4:8, 32-37) Yesu Kristo alimfufua binti yake Yairo, afisa-msimamizi wa sinagogi; mwana wa pekee wa mjane katika Naini, na rafiki yake mpendwa Lazaro, aliyekuwa mfu kwa siku nne. (Marko 5:22, 35, 41-43; Luka 7:11-17; Yohana 11:38-45) Katika Yafa, mtume Petro alimfufua Dorkasi (Tabitha) kutoka kwa wafu. (Matendo 9:36-42) Naye mtume Paulo alimfufua Eutiko ilipotokea ajali ya mauti.​—Matendo 20:7-12.

Ufufuo ulio wa ajabu zaidi, hata hivyo, ulikuwa ule wa Yesu Kristo. Ufufuo huo ulitoa uhakika ulio na nguvu zaidi kwamba kutakuwako ufufuo wa wafu. Kama vile mtume Paulo alivyowaambia wale waliokusanyika penye Areopago katika Athene, Ugiriki: “[Mungu] ameweka siku atakayowahukumu walimwengu kwa haki, kwa mtu yule aliyemchagua; naye amewapa watu wote uthabiti wa mambo haya kwa kumfufua katika wafu.”​—Matendo 17:31.

Ufufuo wa Bwana Yesu Kristo ulihakikishwa kwa historia na mashahidi wengi walioshuhudia kwa macho. Wakati mmoja aliwatokea wanafunzi zaidi ya 500, wengi wao ambao walikuwa wangali hai wakati mtume Paulo alipoiandika barua yake ya kwanza kwa Wakorintho. Ufufuo wa Yesu Kristo ulikuwa hakika sana kwamba Paulo angeweza kuandika hivi katika barua hii: “Lakini kama hakuna kiyama [ufufuo] ya wafu, Kristo naye hakufufuka; tena kama Kristo hakufufuka, basi, kuhubiri kwetu ni bure na imani yenu ni bure. Naam, na sisi tumeonekana kuwa mashahidi wa uongo wa Mungu; kwa maana tulimshuhudia Mungu ya kuwa alimfufua Kristo, ambaye hakumfufua, ikiwa wafu hawafufuliwi.”​—1 Kor. 15:13-15.

Wakristo wa karne ya kwanza, kama vile mtume Paulo, walijua kwa hakika kwamba Yesu alikuwa amefufuliwa. Wao walikuwa na nia ya kupambana na shida za namna zote, hata kifo chenyewe, wakiamini kabisa kwamba wangethawabishwa katika ufufuo.

NINI KITAKACHOFUFULIWA?

Ufufuo wa Yesu Kristo wafunua kwamba kufufuliwa kwa wafu hakumaanishi kufufuliwa kwa mwili ule ule. Yesu hakufufuliwa kwenye maisha ya kibinadamu bali kwenye maisha ya kiroho. Petro wa Kwanza 3:18, NW, anatuambia: “Basi, hata Kristo alikufa mara moja tu kuhusu dhambi, mtu mwenye haki kwa wasio haki, ili apate kuongoza ninyi kwa Mungu, yeye akiuawa katika mwili, lakini akifanywa hai katika roho.” Wakati wa ufufuo wake Yesu alipokea mwili, si wa nyama na damu, bali uliofaa kwa maisha ya kimbinguni.​—1 Kor. 15:40, 44-50.

Ili aonekane na wanafunzi wake kufuata ufufuo wake, Yesu Kristo alijivika mwili wa nyama pamoja na mavazi yaliyofaa, sawa na malaika walivyokuwa wamefanya mapema zaidi walipowatokea wanadamu. Hii yaeleza sababu gani wanafunzi wa Yesu hawakumjua sikuzote kwa mara ya kwanza na sababu gani Yesu angeweza kutokea na kutoweka kwa ghafula. (Luka 24:15-31; Yohana 20:13-16, 26) Vile vile na ikumbukwe kwamba Yesu hakuzikwa pamoja na mavazi bali alifungwa na vitambaa vizuri vya kitani. Alipokwisha kufufuliwa vitambaa hivyo vilibaki kaburini. Kwa hiyo kama vile Yesu alivyopaswa kufanyiza mavazi yanayoonekana, ndivyo alivyojivika mwili wa nyama ulioweza kuonekana na wanafunzi wake.​—Luka 23:53; Yohana 19:40; 20:6, 7.

Hii huenda ikatokeza maulizo, Namna gani juu ya wale ambao, tofauti na Yesu Kristo, watafufuliwa kwenye maisha ya kidunia? Je! miili yao itakuwa ile ile kama ilivyokuwa wakati wa kufa? Sivyo, hiyo isingekuwa busara, kwa maana ingemaanisha watafufuliwa katika hali ya kuelekea kufa. Wale waliofufuliwa wakati uliopita hawakurudishwa wakiwa katika hali ya ugonjwa iliyowafanya wafe. Wajapokuwa hawakuwa wakamilifu wakati wa ufufuo wao, walikuwa nao mwili mzima, ulio timamu.

Kwa wazi sana mwili ule ule, wenye chembe zile zile tu, usingeweza kufufuliwa. Kwa utaratibu wa kuoza mwili wa kibinadamu unageuzwa kuwa sehemu nyingine zinazoweza kumezwa na mimea. Huenda watu wakaila mimea hii. Kama matokeo, sehemu zilizomfanyiza mtu yule wa kwanza zaweza kuja kuwa ndani ya watu wengine. Kwa wazi chembe zile zile haziwezi kuwamo ndani ya mtu yule wa kwanza na ndani ya wengine wote wakati wa ufufuo.

Lakini, Yehova Mungu aweza kumfanya upya mtu yule yule katika ufufuo. Sisi tuko tulivyo kwa sababu ya utu wetu, maono na ukuzi wa akili, siyo kwa sababu ya vitu vinavyoonekana vinavyofanyiza miili yetu. Karibu miaka saba iliyopita chembe zilizoufanyiza mwili wako zilikuwa tofauti na vile zilivyo leo. Mahali pake pamechukuliwa na nyingine. Kwa hiyo mageuzi ya polepole yanayofanyizwa kwa karibu miaka saba ya maisha yako yaweza kufanyizwa wakati ule ule wa ufufuo.

Ijapokuwa hili laweza kusikika kama jambo lisiloaminika sana, hata hivyo si tofauti sana na linalotukia wakati wa kutungwa kwa mimba ya kibinadamu. Ile chembe ndogo inayofanyizwa shahawa na yai viunganapo inao uwezo wa kuwa mtu aliye tofauti na mtu mwingine ye yote aliyepata kuishi. Ndani ya chembe hii, kwa sababu hiyo, mna mfano wa namna ambavyo mtu atakayetoka katika hiyo atakavyokuwa. Mfano huu unakuwa sehemu ya mwili wa mwanadamu anayekua. Kwa hiyo je!, si jambo la busara kwa vile Muumba wa mwanadamu aweza kufufua au kuumba upya mwili ukiwa na utu na kumbukumbu la maisha la mtu aliyekufa?

Hivyo ufufuo au kuumbwa upya kwa kweli kunategemea kumbukumbu la Mungu la mfano wa maisha wa wanadamu. Hata wanadamu wasiokamilika wanaweza kuhifadhi na kufanya upya tamasha zinazoonekana na zinazosikika kwa njia ya tepu (kama zinazoonekana katika televisheni). Ni namna gani ambavyo uwezo wa Mungu wa kuweka kumbukumbu ulivyo mkubwa zaidi, kwa maana yeye anaziita nyota zote zisizohesabika kwa majina yake! (Zab. 147:4) Kwa sababu ya kumbukumbu lake kamili la mifano ya maisha na kusudi lake la kuwafufua wafu, Yehova Mungu angeweza kuwahesabu wanaume waaminifu kama vile Ibrahimu, Isaka na Yakobo kama walio hai.​—Luka 20:37, 38.

Kwa kweli kuna sababu tele za kuamini katika ufufuo au kuumbwa kupya kwa wafu. Imani katika ufufuo ina msingi wa ahadi za Mungu zinazotegemeka, ufufuo uliohakikishwa kwa historia wakati uliopita na tumaini katika uwezo wa Mungu wa kuhifadhi na kufanya upya mifano ya maisha kwa njia iliyo sawasawa.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki