Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w75 2/15 kur. 81-87
  • Je! Wewe U Mwenye Rehema Kadiri Gani?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je! Wewe U Mwenye Rehema Kadiri Gani?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1975
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • UAMINIFU KWA KANUNI ZA HAKI WALETA KIBALI
  • WIVU WAZAA CHUKI YA UUAJI
  • YUSUFU ATEGEMEZWA KWA REHEMA YA YEHOVA
  • TOBA LA KWELI LATOA NAFASI YA REHEMA
  • KUSIMAMA HUKUMUNI KWA KUMBUKUMBU LA REHEMA
  • Njaa Yenye Kuleta Kifo Katika Wakati wa Utele
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1987
  • “Je, Mimi Niko Mahali pa Mungu?”
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2015
  • Yehova Hakumsahau Yosefu Kamwe
    Masomo Unayoweza Kujifunza Katika Biblia
  • “Tafadhali Sikilizeni Ndoto Hii”
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2014
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1975
w75 2/15 kur. 81-87

Je! Wewe U Mwenye Rehema Kadiri Gani?

1. Kwa sababu gani hakuna udhuru wa kuwa na ukatili ulioenea pote kwa kizazi kilichopo?

KATIKA hizi siku za kutovumilia na choyo, mtu mwenye kutenda kwa rehema ni baraka yenye burudisho. Yasemekana hivi juu ya Mungu wa kweli: “[Yehova] ana fadhili, ni mwingi wa huruma, si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema, [Yehova] ni mwema kwa watu wote, na rehema zake zi juu ya kazi zake zote.” (Zab. 145:8, 9) Naye Yesu alituonya kwa upole ‘tuendelee kuwa wenye rehema, sawa na Baba yenu alivyo mwenye rehema.’ (Luka 6:36, NW) Basi ni namna gani hali zisizovumilika zinazoletwa na shuku zisizohesabika, uadui na ukatili wa watu na mataifa zinavyokishtaki kizazi kilichopo!

2. Rehema ya Mungu inawafikia nani peke yao, na kwa sababu gani?

2 Mithali 28:27 yasema: “Mwenye kuwagawia maskini hatahitaji kitu; bali afichaye macho yake atakuwa na laana nyingi.” Ni wazi kutokana na hili kwamba rehema ya Mungu haitawafikia wale ‘wanaoficha macho yao.’ Mungu si wa kuchukuliwa na fikira. Kuzoea rehema kwake sikuzote kunapatana na sifa zake nyingine na kanuni zenye haki, kutoa na haki na utakatifu. (Hos. 2:19) Ye yote anayeitumia rehema ya Mungu vibaya, akidhani kwamba Mungu ataendelea kumrehemu bila kujali anafanya nini, atakatishwa tumaini kwa uchungu. Mtu anayeonyesha dharau ya makusudi kwa njia zenye haki za Mungu kwa matendo yake na mwendo wa maisha anamkosea Mungu, naye Mungu wa kweli kwa haki ‘atazuia kwa hasira rehema zake.’​—Zab. 77:9; Rum. 2:4-11.

3. Ni maulizo gani yawezayo kutusaidia tuamue sifa yetu wenyewe ya rehema?

3 Ndugu wa mama-mzazi mmoja na Yesu Yakobo alitoa onyo la kufaa na, wakati ule ule, akatia moyo alipoandika hivi: “Kwa maana yeye asiyezoea rehema atapata hukumu yake bila rehema. Rehema yashangilia hukumu kwa ushindi.” (Yak. 2:13, NW) Je! wewe u mwenye rehema kadiri gani? Je! ni vyepesi kwako kusahau makosa ambayo huenda ukatendwa? au unaona ni vigumu kuyasahau mambo hayo? Je! unayaona sana mahitaji ya walio karibu yako? au lazima fikira zako zikazwe kwenye mambo haya sikuzote? Je! unaelekea kuona shuku juu ya makusudi ya wengine? au unaweza kujua na kukubali unyofu na uaminifu? Je! unaelekea kuwafikiria zaidi wale walio na vyeo vikubwa au wenye ujuzi hasa kwa njia fulani? au waweza kupata furaha ya kweli katika sifa za kiroho tu? Kama ukijipima na maulizo haya, je! utaonekana kuwa usiye na rehema? Matokeo ni ya lazima, kwa maana, kama sisi mmoja mmoja twapendezwa au sivyo, hukumu ya Yehova italetwa juu yetu mmoja mmoja kama vile ambavyo ameonyesha kupitia kwa Yakobo, na ni mtu mwenye kuzoea rehema peke yake atakayeonyeshwa rehema akiletwa hukumuni.

4. Mtu mwenye rehema aweza kutambuliwaje?

4 Mtu mwenye rehema ni yeye asiyeweka kinyongo moyoni, mwenye nia ya kuzuia laana na adhabu hali ziruhusupo, mwenye ukarimu katika kutoa kwa kimwili na kiroho pia, mwenye kuwakumbuka wenye shida na apendezwaye nao kwa bidii, asiyeonyesha upendeleo au kutumia ulimi wake kwa kiburi au wivu, anayefanya matendo yake ya ukarimu na kugawa zawadi zake za rehema kwa unyofu na unyenyekevu bila majivuno, asiyekuwa bingwa sana katika shughuli zake na wenzake hata wanakuwa kama sehemu tu za “mashine ya tengenezo.” Kujitoa kwake kwa ukarimu, hata zaidi kuliko mali zake, hakutapita bila kuthawabishwa​—kwa kweli bila kuthawabishwa na Yehova. Neno la Mungu lasema: “Amhurumiaye maskini humkopesha [Yehova]; naye atamlipa kwa tendo lake jema.” Naye Yesu aliongeza hivi juu ya mithali hiyo: “Heri wenye rehema; maana hao watapata rehema.”​—Mit. 19:17; Mt. 5:7.

UAMINIFU KWA KANUNI ZA HAKI WALETA KIBALI

5. Yusufu alikuwa nani, na kwa sababu gani yeye hasa alikuwa mpendwa wa baba yake?

5 Mfano wa kutokeza wa mtu aliyeiga rehema ya Yehova ni Yusufu mjukuu wa Ibrahimu na mwana wa Yakobo au Israeli. Yusufu alizaliwa Shamu, akiwa mwana wa kwanza kati ya wana wawili wa Yakobo kupitia kwa mkewe mpendwa Raheli. (Mwa. 30:22-24; 35:24) Kwa kuwa Yakobo alikuwa na umri wa miaka 91 Yusufu alikuwa mwana wa uzee wake akapata kupendwa zaidi kuliko kaka zake. Wakati Yusufu alipokuwa mwenye umri wa miaka sita hivi, Yakobo aliondoka Padani-aramu alikokuwa amekwenda kutafuta mke kati ya watu wake mwenyewe na kurudia Kanaani pamoja na jamaa yake yote. (Mwa. 31:17, 18, 41) Alikaa kwa muda katika Sukothi, Shekemu na Betheli. Baadaye, walipokuwa wakielekea Bethlehemu kutoka Betheli, mama ya Yusufu, Raheli, alikufa akimzaa mwanawe wa pili Benyamini; hivyo Benyamini ndiye aliyekuwa ndugu wa pekee hasa wa Yusufu, wana wengine wa Yakobo wakiwa ndugu za baba-mzazi mmoja na Yusufu, waliozaliwa na Yakobo kwa Lea, dada ya Raheli, na kwa Zilpa na Bilha, wajakazi wawili wa Lea na Raheli.​—Mwa. 33:17-19; 35:1, 5, 6, 16-19.

6. (a) Yusufu alimletea baba yake habari gani juu ya ndugu za baba-mzazi mmoja naye, na kwa sababu gani hili halikuwa tendo la ukatili? (b) Ni kwa njia gani Simeoni na Lawi walivyokuwa wamejionyesha wenyewe kuwa wasio na huruma wakati mmoja mapema?

6 Ndugu kumi za Yusufu wa baba-mzazi mmoja hawakuonyesha uaminifu ule ule kwa kanuni za haki aliouonyesha Yusufu tangu umri mdogo. Alipokuwa mwenye umri wa miaka kumi na saba alikuwa akichunga kondoo pamoja na wana wa Yakobo na Bilha na Zilpa. Ingawa alikuwa mdogo kuliko ndugu zake, Yusufu alionyesha bidii zaidi kwa faida za baba yake kuliko hawa ndugu za baba-mzazi mmoja naye na kuleta habari mbaya kwa baba yake ipasavyo. (Mwa. 37:2) Hakuwa akitenda kikatili kwa kufanya hivyo, kwa sababu ndugu hawa walikuwa wakifuata mwendo wenye kosa naye Yakobo alistahili kujulishwa. Pengine uaminifu huu kwa kanuni za haki ulishiriki kumfanya Yakobo ampende Yusufu. Lakini, badala ya ndugu za Yusufu kufaidika kutokana na mfano wa Yusufu, walionyesha nia yenye wivu na roho ile ile ya ukatili kwake iliyokuwa imewafanya wawachinje ovyo ovyo watu wa Shekemu wakiongozwa na Simeoni na Lawi, watu ambao walikuwa wakijaribu kuanza uhusiano wa kirafiki nao na wasiokuwa na ulinzi wakati huo. Ijapokuwa walidai kuchinja kwao Washekemu kulikuwa kwa haki, baba yao Yakobo aliwaambia Simeoni na Lawi hivi, viongozi wa shambulio: “Mmenitaabisha, kunifanya ninuke vibaya kati ya watu wa nchi hii,” na miaka mingi baadaye Yakobo aliitaja ghadhabu ya Simeoni na Lawi kama yenye kulaaniwa, “kwa maana ilikuwa kali, na hasira yao, maana ilikuwa haina huruma.” (Mwa. 34:1-31; 49:7) Kwa sababu ya kukosa kwao huruma, walipoona kwamba baba yao alimpenda Yusufu zaidi kuliko ndugu zake wote na kumshonea kanzu ndefu yenye mistari (pengine inayofanana na zile zinazovaliwa na watu wenye vyeo), “hawakuweza kusema naye kwa amani.”​—Mwa. 37:3, 4.

7. Yusufu aliota ndoto gani. naye baba yake na ndugu za baba-mzazi mmoja naye waliitikiaje?

7 Baadaye Yusufu aliota ndoto akawapasha ndugu zake habari. Katika ndoto yake ndugu wote walikuwa wakifunga miganda shambani katikati wakati mganda wake uliposimama wima nayo miganda ya ndugu za baba-mzazi mmoja naye ikauzunguka na kuuinamia mganda wake. Kwa sababu hiyo ndugu zake wakaanza kumwambia: “Je! kweli wewe utatumiliki sisi?” nao wakapata sababu zaidi ya kumchukia. Masimulizi yanaendelea: “Akaota tena ndoto nyingine, akawaambia ndugu zake, akasema, Angalieni, nimeota ndoto nyingine; na tazama, jua na mwezi na nyota kumi na moja zikaniinamia. Akawaambia baba yake na ndugu zake; baba yake akamkemea akamwambia, Ni ndoto gani hii uliyoiota? Je! mimi na mama yako na ndugu zako tutakuja tukusujudie hata nchi? Ndugu zake wakamhusudu; bali baba yake akalihifadhi neno hili.” Kwa wazi Yakobo alijua kwamba huenda ndoto hizo zikawa na maana. Ingawa huenda ikaelekea kwamba Yusufu alikuwa akionyesha nia ya ukuu juu ya ndugu zake, kwa kweli yeye alikuwa akisimulia tu yale ambayo Yehova alikuwa amemfunulia, hali iliyowapa ndugu zake nafasi zaidi ya kuonyesha hali yao ya moyoni.​—Mwa. 37:5-11.

WIVU WAZAA CHUKI YA UUAJI

8. Yusufu alipataje kuwa mbali na nyumbani pamoja na ndugu zake za baba-mzazi mmoja naye, nao ndugu zake walilionaje jambo hili?

8 Sasa ndugu zake za baba-mzazi mmoja naye wakaenda kulisha kundi la baba yao katika ujirani wa Shekemu Yakobo alipokuwa akikaa Hebroni. Yakobo akahangaikia hali yao, pengine akiukumbuka ukatili uliokuwa umechochewa juu yake na wanawe katika ujirani walipokuwa wakiondoka Shamu. Ijapokuwa ulikuwa mgawo usiopendeza kwake bila shaka kwa sababu ya ukatili wa ndugu za baba-mzazi mmoja naye, Yusufu hakusita kwenda kwa ajili ya Yakobo akaone kama walikuwa salama salimini na kama kundi lilikuwa salama salimini. Mwishowe aliwapata Dothani, lakini, kabla hajaweza kuwakaribia, walimwona kwa mbali wakaanza kupanga kumwua.​—Mwa. 37:12-20.

9. Reubeni alipanga kufanya nini, lakini ni nini lililotukia mwishowe kwa Yusufu mikononi mwa ndugu zake?

9 Reubeni, mzaliwa wa kwanza wa Yakobo, alijaribu kumkomboa na mikono yao, ‘ili akamrudishe kwa baba yake,’ kwa sababu ya kuhangaikia madaraka yake mwenyewe juu ya Yusufu kama mzaliwa wa kwanza. (Mwa. 37:22-30) Yaelekea Reubeni hakuwako wakati msafara wa Waishmaeli ulipopita karibu ukielekea Misri kutoka Gileadi. Yuda akashauri kwamba Yusufu auzwe kwao badala ya wao kumwua na kuifunika damu yake. Ndugu wakakubali na, ingawa Yusufu aliomba rehema, walimwuza kwa Waishmaeli kwa vipande 20 vya fedha. Halafu wakaichukua kanzu ndefu ya Yusufu, waliyokuwa wamemnyang’anya, wakachinja mbuzi dume wakaichovya kanzu damuni. Baadaye ilipoonyeshwa kwa Yakobo, alisadiki kwamba mnyama-mwitu alikuwa amemnyafua mwanawe, na kwa hiyo akahuzunika sana hata akakataa asifarijiwe. Mwishowe wafanya biashara walimleta Yusufu Misri akauzwa kama mtumwa kwa Potifa, mkuu wa walinzi wa Farao.​—Mwa. 37:21-36.

10. Huu ni mfano kwetu leo kwa njia gani, na ni faida gani ambayo Yusufu angeipata kutokana na taabu zake?

10 Chuki hii yenye uuaji waliyokuwa wameionyesha ndugu za baba-mzazi mmoja Yusufu kwa jeuri hivyo na ukosefu wao wa ukatili wa kutomfikiria baba yao ni onyo kwa wo wote leo ambao huenda wakaweka kinyongo moyoni juu ya ndugu zao wa kiroho katika kundi la Kikristo. Yesu alisema hivi: “Kila amwoneaye ndugu yake hasira itampasa hukumu.” (Mt. 5:22) Lakini Yusufu alikuwa akitayarishwa akawe baraka kuu kwa watu wake, nayo taabu aliyoipata ilikusudiwa kumtakasa kwa ajili ya daraka kubwa hili.

YUSUFU ATEGEMEZWA KWA REHEMA YA YEHOVA

11. Yusufu alitendaje juu ya machungu yaliyompata, lakini ni majaribu gani zaidi ambayo yalimngoja?

11 Yusufu hakuacha kamwe machungu yaliyompata yamchahishe na kumwondoa kwa Mungu wa kweli. Bali, yeye alizidi kuutegemea uwezo wenye kuokoa na kuhifadhi wa Yehova, na kwa sababu hiyo matendo yote ya mikono yake yakabarikiwa. Baadaye bidii yake katika utumishi wa Potifa ilimkweza kwenye cheo cha msimamizi katika nyumba ya Potifa. Mke wa Potifa alijaribu mara nyingi akashindwa kumtongoza Yusufu, aliyeendelea kuwa imara katika uamuzi wake kutomtenda Mungu wake dhambi. Alipotatanishwa katika jitihada zake, sasa mke wa Potifa alimshtaki Yusufu kwa uongo juu ya kujaribu kumnajisi naye Yusufu akatupwa gerezani, Potifa alipoiamini hadithi yake.​—Mwa. 39:1-20.

12. (a) Yusufu alitendewaje gerezani, kulitukia nini kati yake na watumishi wawili wa Farao na hii ilimtiaje moyo? (b) Ni hali gani zilizofanya Yusufu afunguliwe gerezani?

12 Kwa muda fulani Yusufu alitendwa kikatili gerezani. (Zab. 105:17, 18) Walakini, bidii yake na kumtegemea Yehova vilithawabishwa tena kwa madaraka zaidi, nao mwenendo wake mwema akiwa chini ya hali mbaya ulifanya awekwe cheo cha kutumainiwa asimamie wafungwa wengine. Mwishowe, watumishi wawili wa Farao walipata kuwamo, mkuu wa wanyweshaji na mkuu wa waokaji. Baadaye, kila mmoja wao aliota ndoto na asubuhi yake wakawa wamevunjika moyo maana hakuwako mtu wa kuwafasiria ndoto zao. Akijua shida yao na kwa kumpa Yehova Mungu sifa ifaayo, Yusufu aliwafasiria ndoto zao ikatukia sawa na alivyowafunulia. Mkuu wa wanyweshaji alipewa tena kibali ya Farao kati ya siku tatu, mkuu wa waokaji akaangikwa katika kipindi kile kile. Bila shaka kwa kutiwa moyo na kibali ya Yehova kwake kwa kumpa tafsiri na bila shaka kwa kuridhika kuwa chanzo cha ndoto zake mwenyewe kilikuwa cha kimungu, Yusufu alimsihi mkuu wa wanyweshaji akaseme na Farao kwa ajili ya Yusufu, naye akakubali kufanya hivyo. Lakini mnyweshaji, alipotoka gerezani, alisahau mpaka baadaye miaka miwili Farao mwenyewe alipoota ndoto ambazo hakuweza kuzielewa. Wachawi wote wa Misri waliposhindwa kufasiri ndoto za Farao, mnyweshaji aliyakumbuka yaliyotukia kati yake na Yusufu akayasimulia kwa Farao. Mara Yusufu akatolewa gerezani akazifasiri ndoto za Farao.​—Mwa. 39:21–41:14.

13. Ni nini iliyokuwa tafsiri ya ndoto ya Farao, naye Yusufu alithawabishwaje na Yehova kwa uvumilivu wake wakati wa majaribu?

13 Sasa kumbukumbu la uvumilivu alilokuwa amekuza Yusufu na nia yenye huruma aliyokuwa ameidumisha wakati wa majaribu yake vilipaswa vithawabishwe. Akimpa Yehova sifa kwa mara nyingine, Yusufu alizifasiri ndoto mbili za Farao, akimweleza kwamba ingekuwako miaka saba ya shibe ikifuatwa na miaka saba ya njaa. Kisha Yusufu akamwarifu Farao kwamba Yehova alikuwa amempa yeye jibu la amani na kueleza namna ambavyo Farao angeweza kujitayarisha kwa miaka ya njaa wakati wa miaka ya shibe. Farao alimwona Yusufu mwenyewe kama msimamizi wa chakula afaaye ambaye angehitajiwa na kumweka kwenye cheo hiki, akimfanya awe wa pili katika ufalme na kumpa mamlaka yote kusimamia kazi ya kuweka akibani nafaka ya kujikinga na miaka ya njaa. Waliweka nyingi sana hata mwishowe wakaacha kuihesabu. Yusufu alipewa mke pia, Asenathi, binti ya Potifera, kuhani wa Oni, aliyemzalia wana wawili, Manase na Efraimu.​—Mwa. 41:15-52.

TOBA LA KWELI LATOA NAFASI YA REHEMA

14. Ni nafasi gani iliyojitokeza kwa Yusufu katika cheo chake kikubwa, nayo rehema yake ilijaribiwaje vikali sana sana?

14 Sasa Yusufu alikuwa katika cheo cha kuonewa kijicho kweli kweli. Maisha za watu wa Misri, kutia na maisha za Potifa na mkewe, zilikuwamo mikononi mwake. Lakini haikuwako hatari kwa ye yote kati yao. Yusufu alikuwa amekwisha jihakikisha kuwa mtu mwenye kusamehe na mwenye rehema, si mtu wa kutaka kulipiza kisasi au mkorofi. Hata hivyo, rehema yake ingejaribiwa vikali sana. Hii ilitukia njaa ilipokuwa imeenea katika dunia yote na watu wa dunia yote wakaja Misri wakitafuta nafaka. Siku moja, Yusufu alipokuwa akiangalia kazi zake na kutoa chakula kwa mataifa yenye kufa njaa kwa huruma na kuwatolea Wamisri vile vile, ndugu kumi za baba-mzazi mmoja naye walijitokeza mbele yake wakaanguka kifudi-fudi. Mara Yusufu akazikumbuka ndoto alizokuwa ameota juu yao na, ingawa aliwatambua, alijifanya asiyejulikana kwao na kusema nao kupitia kwa mkalimani tu. Angewatendeaje? Baada ya zaidi ya miaka 20, wakati wao wa hukumu ulikuwa umefika. Kwa kuwa walikuwa wametenda bila rehema walistahili kuhukumiwa bila rehema naye Yusufu asingeweza kuitumia vibaya hukumu ya Yehova, kwa kuwa alikuwa akitenda kama wakili wa Yehova. Hata hivyo, Yusufu hakuwa mtu wa kujilipiza kisasi, na ingalimpasa atoe hesabu kwa Mungu kwa sababu ya mwendo wake wa tendo kwao. Kwa hiyo, akiwa na hekima kutoka juu, aliwatia jaribuni.​—Mwa. 41:53–42:8.

15. (a) Yusufu aliwatendeaje ndugu za baba-mzazi mmoja naye, na kwa kusudi gani? (b) Ndugu zake za baba-mzazi mmoja naye walitendaje kwa sababu ya tukio hili?

15 Akitenda kikatili kwao, aliwashtaki juu ya kuwa wapelelezi, nao walipojidai kutokuwa na hatia na kusimulia kwake kwamba wote walikuwa wana wa mtu mmoja na kwamba ndugu mwingine alikuwa angali nyumbani, alimfunga Simeoni machoni pao akawaambia atakaa amefungwa mpaka watakaporudi wakiwa na ndugu yao mwingine. Kwa majonzi, ndugu zake walionyesha nia ya kutubu kabisa, wakaukubali msiba huu kama hukumu ya kulipiza kisasi kutoka kwa Mungu, “kwa kuwa” kama walivyosemezana, “tuliona shida ya [nafsi ya Yusufu], alipotusihi, wala hatukusikia.” Yusufu alipowasikia alihuzunika sana mwenyewe akatoka walipo akitoa machozi, ingawa wao hawakujua hivyo. Walakini, kujaribiwa kwao hakukuwa kumekwisha. Lazima kusiwepo na shaka lo lote juu ya toba lao. Akijaza vyombo vyao nafaka, Yusufu aliagiza fedha yao irudishwe katika magunia yao kwa siri, akawaambia warudi nyumbani, akamweka Simeoni kifungoni.​—Mwa. 42:9-28.

16. (a) Benyamini alishukaje Misri mwishowe, naye Yusufu alitendaje alipomwona? (b) Yusufu aliwatiisha ndugu zake wa baba-mzazi mmoja naye kwenye jaribu gani la mwisho, nayo matokeo yakawaje?

16 Mwishowe nafaka yao ilikwisha ikawa lazima warudie Misri. Lakini walikuwa wamekwisha onywa wasiuone uso wa msimamizi wa chakula wa Misri ndugu yao asipokuwa nao. Kwa kuogopa kumpoteza mwana wa pekee aliyebaki wa mkewe mpendwa Raheli kama alivyokuwa amempoteza Yusufu, Yakobo alizidi kukataa kumwacha aende, mpaka mwishowe akawa hana jingine la kufanya. Yuda aliahidi kuwa mlinzi wake. Walipotokea mbele ya Yusufu naye akamwona ndugu yake mwenyewe hasa Benyamini akiwa nao Yusufu hakuweza kujizuia. Kwa kuwa mawazo yake ya ndani yalisisimka kwa sababu ya ndugu yake, aliingia katika chumba cha ndani akatiririsha machozi. Ndipo alipowatia ndugu za baba-mzazi mmoja naye katika jaribu la mwisho. Kwa werevu alifanya ionekane kwamba Benyamini alikuwa ameiba kikombe cha fedha chenye thamani nyingi na kuamuru Benyamini aachwe nyuma kama mtumwa wake huku wengine wakirudi nyumbani kwao na kwa baba yao. Kwa majonzi na huzuni ya kujua kwamba hasara ya mpendwa wake Benyamini ingezishusha mvi za baba yao kaburini, walimsihi Yusufu awarudishie Benyamini kwa ajili ya baba yao na, mwishowe, Yuda alipojitoa achukuliwe badala ya Benyamini, Yusufu hakuweza kuvumilia tena naye akajifunua kwa ndugu zake akitiririsha machozi, akisema: “Mimi ni Yusufu, ndugu yenu, ambaye mliniuza kwenda Misri. Basi sasa, msihuzunike, wala msiudhike nafsi zenu, kwa kuniuza huku; maana Mungu alinipeleka mbele yenu kuhifadhi maisha.” Alipoagizwa na Farao, Yusufu ndipo alipopanga Yakobo baba yake aje Misri pamoja na nyumba yake yote, nayo sehemu ya nchi ya Misri iliyokuwa bora zaidi ikawa yao.​—Mwa. 42:29–47:31.

KUSIMAMA HUKUMUNI KWA KUMBUKUMBU LA REHEMA

17. (a) Ni nini kinachotilia mkazo kadiri na sifa ya rehema ya Yusufu, nasi twawezaje kuwa na hakika kwa kufaa kwamba rehema ilikuwa sifa aliyoionyesha Yusufu sikuzote? (h) Sisi wenyewe twawezaje kufaidika kutokana na mifano ya Yusufu, Yesu na Stefano?

17 Kadiri na sifa ya rehema ya Yusufu vinatiliwa mkazo na hali ambazo chini yake ilionyeshwa. Yusufu hakufikiria kulipiza kisasi alipokuwa na uwezo wa kufanya hivyo, alipotendwa kikatili hata kwa njia ya uuaji na ndugu zake, aliposhtakiwa kwa ukorofi na kwa uongo na mke wa Potifa, alipotiwa gerezani kwa ukali na udhalimu na Potifa, aliposahauliwa bila huruma na bila shukrani na mkuu wa wanyweshaji ambaye alikuwa amemfariji kwa huruma. Bali, kwa upendo na huruma nyingi ya unyofu aliyaangalia mahitaji yao yote, akionyesha kupendezwa kwenye huruma na nyumba yote ya baba yake na watu wote wa taifa la Misri. Kwa kweli sifa hii ya rehema haikuwa jambo ambalo Yusufu alilipata baada tu ya kukwezwa kwenye cheo cha ukubwa na uwezo. Bali, rehema aliyomwonyesha Yehova wakati wa majaribu yake, ni ushuhuda wa nia yenye kusamehe na yenye rehema ambayo bila shaka Yusufu aliidumisha mpaka mwisho. Hii inaelekea kuwa hakika kabisa kutokana na kanuni aliyoitaja Yesu: “Heri wenye rehema; maana hao watapata rehema.” (Mt. 5:7) Inalingana sana na nia ya Yesu mwenyewe juu ya mti wa mateso alipokuwa karibu kufa akasema hivi: “Baba, uwasamehe, kwa kuwa hawajui watendalo,” na kama ile ya Stefano alipokuwa akipigwa kwa mawe mpaka kufa akapaza sauti: “[Yehova], usiwahesabia dhambi hii.” (Luka 23:34; Matendo 7:60) Nia yenye rehema iliyoonyeshwa mara hizi zote ilithawabishwa na Yehova.

18. Kwa sababu gani imetupasa tupendezue sana na kuzoea rehema?

18 Kwa hiyo, je! haielekei kuwa wazi mapendezi yetu yamepaswa kuwa nini katika kuzoea rehema? Paulo anatuhakikishia kwamba “kila mtu miongoni mwetu atatoa habari zake mwenyewe mbele za Mungu.” (Rum. 14:12) Lo! inaridhisha namna gani kujua kwamba “rehema inafurahia hukumu kwa shangwe”! Kama ni katika wakati wa hatari uliopo, au katika Siku ya Hukumu inayokuja kasi (2 Pet. 3:7), namna hali yetu itakavyokuwa katika kutoa hesabu yetu wenyewe mbele za Mungu na Mwamuzi wake aliyewekwa, Yesu Kristo, itategemea, kati ya mambo mengi kumbukumbu la rehema litakaloonyeshwa na rehema yetu. Kufuata amri ya Yesu ya kupenda kwa uthabiti, chini ya hali zote, kutasaidia kulijaza kumbukumbu hilo na, wakati ule ule, kushiriki kuleta sifa kwa Yehova na amani ya kundi.

​—Kutoka The Watchtower, Aug. 15, 1974.

[Picha katika ukurasa wa 83]

Yajapokuwa maombi ya Yusufu ya rehema, ndugu zake walimwuza kwa Waishmaeli kwa vipande ishirini vya fedha

[Picha katika ukurasa wa 85]

Ijapokuwa ndugu za Yusufu walikuwa wamemtenda kikatili, yeye hakujilipiza kisasi bali aliwahurumia ndugu zake wenye kutubu na kuangalia mahitaji yao yote

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki