Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w76 3/15 kur. 138-140
  • Sababu Gani Kuwa Mkaribishaji?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Sababu Gani Kuwa Mkaribishaji?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1976
  • Habari Zinazolingana
  • Ukaribishaji Wageni​—Sifa Inayovutia na Inayohitajika Sana!
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2018
  • “Fuateni Mwendo wa Ukaribishaji-Wageni”
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1996
  • “Mkaribishane”
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2005
  • Shiriki “Mambo Mema” kwa Kuwa Mkaribishaji-Wageni (Mt. 12:35a)
    Huduma Yetu ya Ufalme—2014
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1976
w76 3/15 kur. 138-140

Sababu Gani Kuwa Mkaribishaji?

“HAKUNA mgeni aliyelala nje, mlango wangu ulikuwa wazi daima kwa msafiri.” (Ayu. 31:32, Jerusalem Bible) Ukaribishaji wa namna hii ulioonyeshwa na Ayubu ulikuwa ishara ya kuwatambulisha watumishi waliojitoa wa Mungu katika nyakati za kale.

Kuonyesha ukaribishaji kulikuwa hasa ni kuitikia kwa upendo uhitaji wa mgeni wa msaada na makao. Karne nyingi zilizopita wasafiri kwa jumla walitua katika kijiji au mji na kwenda kwenye njia kuu. Hii ilitoa wasaa kwa wenyeji kumkaribisha mgeni akae nao kwa usiku huo.

Habari ya Biblia kuhusu Mlawi mmoja wakati wa kipindi cha Waamuzi katika Israeli inaonyesha jambo hili. Njiani kutoka Bethlehemu, yeye, mtumishi wake na suria wake walielekea Gibea ya Benyamini ili walale. Twasoma: “Basi wakaingia ndani wakaketi katika njia kuu ya mji, wala hakuna mtu aliyewapeleka nyumbani wakakae usiku kucha.”​—Amu. 19:1, 2, 14, 15, NW.

Tabia ya namna hii isiyo ya ukaribishaji ilikuwa ya ajabu sana katika mji wa Kiisraeli maana haikuwa ya kawaida. Yule Mlawi alikuwa ameepukana na mji wo wote usio wa Kiisraeli, akidhani kuwa angepokewa vizuri zaidi na Waisraeli. (Amu. 19:11, 12) Walakini, mwishowe mzee mmoja mwanamume asiye wa kabila la Benyamini akaonyesha ukaribishaji, akisema: “Na iwe amani kwako; lakini na haya yaliyokupungukia na yawe juu yangu mimi; lakini usilale njiani.”​—Amu. 19:16-20.

Kule kukataa kwa, watu wa Gibea kuonyesha ukaribishaji kwa wageni kulikuwa ni uthibitisho wa upungufu mkubwa wa adili. Kwa uchoyo walifuatia shughuli zao wakikataa kutwaa wasaa wa kuonyesha fadhili.

Wingi wa choyo yao ulionekana hata zaidi baada ya yule mzee mwanamume kuwapokea nyumbani kwake wale wasafiri. Umati wa wanaume waliizunguka nyumba hiyo, wakidai yule Mlawi aletwe kwao wamfanye ufisadi. Walakini, yule mzee mwanamume hakuwakubalia madai yao. Hata hivyo hali ilizidi kuwa hivyo hata suria wa yule Mlawi akapewa mikononi mwao. Walimtenda mabaya usiku kucha hata akafa.​—Amu. 19:22-28.

Karne fulani huko nyuma roho kama hiyo ilikuwako katika Sodoma. Jioni moja wageni wawili wazuri waliingia Sodoma. Akiisha kuwaona, Lutu aliwakaribisha nyumbani kwake, akawasihi wasilale katika njia kuu. Wale wageni wakakubali, lakini kabla hawajaweza kwenda kulala, umati uliizunguka nyumba ya Lutu, “tangu mvulana hata mzee.” Wakamlilia Lutu awatolee wale wageni wawili wawafanye ufisadi, lakini alikataa kwa nguvu. (Mwa. 19:1-11) Huu ulikuwa ushuhuda wa haki iliyosababisha kuokoka kwa Lutu uharibifu ambao Yehova alileta juu ya Sodoma na miji mingine mitatu ya jirani.​—Kum. 29:23; 2 Pet. 2:6-9.

Bila yeye mwenyewe kujua, Lutu alikuwa amewaingiza malaika nyumbani mwake. Mfano wake, na mifano mingine ya namna ile ya ukaribishaji, inaonyeshwa katika Waebrania 13:2 kama jambo la kutia Wakristo moyo. Twasoma: “Msisahau kuwafadhili wageni; maana kwa njia hii wengine wamewakaribisha malaika pasipo kujua.”

Hakika, roho ya fadhili na ukarimu unaoongoza kwenye ukaribishaji wa kweli ni jambo la thamani. Kukosekana kwake, kama kulivyoonyeshwa na wenyeji wa Gibea na Sodoma, kunaweza kuongeza matendo ya choyo ipitayo kadiri. Ndivyo ilivyo kwa maana upendo wa kweli kwa wengine unamfanya mtu atende kwa ajili ya faida zao na kumzuia asivunje haki zao. Mtume Paulo alionyesha jambo hili aliposema: “Ampendaye mwenzake ameitimiza sheria. Maana kule kusema, Usizini, Usiue, Usiibe, Usitamani; na ikiwapo amri nyingine yo yote, inajumlishwa katika neno hili, ya kwamba, Mpende jirani yako kama nafsi yako. Pendo halimfanyii jirani neno baya.”​—Rum. 13:8-10.

Tukisitawisha na kudumisha moyo wa upendo unaotokeza wonyesho halisi wa ukaribishaji ndipo tu tunapoweza kupata kibali ya Mungu. Ndivyo ilivyo maana upendo kwa Mungu na kwa wengine ndio msingi wenyewe wa ibada ya kweli. Yesu Kristo alisema: “Hivyo watu wote watatambua ya kuwa ninyi mmekuwa wanafunzi wangu, mkiwa na upendo ninyi kwa ninyi.”​—Yohana 13:35.

Kama katika siku za kale, kati ya watu wa Mungu leo pana wasaa mwingi kuwa wa kwanza katika kuonyesha ukaribishaji. Ziko nyakati ambapo misiba yenye kusababishwa na vitu vya asili (matetemeko ya ardhi, dhoruba, tufani n.k.), maradhi au mengine kama haya yanaingiza waamini wenzetu katika uhitaji. Ni vizuri namna gani wakati ndugu na dada zao wa kiroho wanapofanya wawezavyo kusaidia! Halafu, pia, kunaweza kuwa na nyakati za kuonyesha ukaribishaji wetu kwa wazee wenye kusafiri, kwa kuwapa chakula na/au mahali pa kukaa, tukiwasaidia gharama fulani. Tena, ndani ya kundi mna wasaa mwingi wa kushiriki chakula, ushirika wa wenzetu waaminio na mambo mengine kama hayo. Kuonyesha ukarimu wa namna hii kwaweza kufanya tutiane moyo na kujengana.

Ukionyeshwa ukaribishaji, utakumbuka nini? Ni hekima kuwa mwangalifu usiingie katika shtaka lo lote la kujinufaisha mwenyewe kwa ye yote na kwa njia hiyo kuwa namna ya ‘kimelea kati ya watu.’ Mtume Paulo na wafanya kazi wenzake waliweka mfano mzuri kwa jambo hili. Mtume aliwakumbusha wazee wa kundi la Efeso: “Ninyi wenyewe mnajua ya kuwa mikono yangu hii imetumika kwa mahitaji yangu na ya wale waliokuwa pamoja nami.” (Matendo 20:34) Hii haimaanishi kuwa Paulo na wenzake walikataa misaada yote ya ukaribishaji. Kwamba walikubali ukaribishaji wa kweli ni wazi kutokana na yaliyotukia katika Filipi. Katika mji huo Lidia na nyumba yake walikubali Ukristo kwa moyo. Hapo baadaye akamsihi Paulo na wenzi wake: “Kama mmeniona kuwa mwaminifu kwa [Yehova], ingieni nyumbani mwangu mkakae.” Ukaribishaji wa moyoni wa namna hii usingeweza kukataliwa. Mwandikaji wa Matendo, Luka daktari, anaongeza. “Akatushurutisha.”​—Matendo 16:14, 15.

Mtu anapokubali ukaribishaji wa mwingine anajiweka chini ya lazima ya kuwa mgeni mwenye shukrani. Yesu Kristo alivuta akili kwenye jambo hili alipowaambia wafuasi wake: “Basi, kaeni katika nyumba iyo hiyo, mkila na kunywa vya kwao . . . Msihame-hame kutoka nyumba hii kwenda hii.” (Luka 10:7) Katika kusema alivyosema, Yesu alikuwa akionyesha wazi kuwa wafuasi wake wasingeondoka nyumbani mwa aliyewakaribisha bila shukrani na kwenda mahali pengine ambapo mwenye nyumba angeweza kuwapa starehe zaidi na chakula kizuri zaidi. Tukichukua kanuni ya onyo la upole la Yesu, tunaweza kuona kuwa ingekuwa siyo fadhili kufutilia mbali mwaliko ati kwa sababu baadaye kitu fulani kilicho bora katika hali ya vitu vya kimwili kimetolewa kwetu.

Kwa kuona ambayo Biblia inasema, tunapaswa sote tuwe wakarimu kwa sababu ya upendo mkubwa kwa Yehova na kwa wanadamu wenzetu. Hata kama tuna kidogo, hatujaondolewa kule kuonyesha moyo wa ukaribishaji​—⁠kufikiria hali ya wengine. Na wakati ukaribishaji wa kweli uonyeshwapo kwetu, tunapaswa kuukubali kwa shukrani kama wonyesho wa upendo.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki