Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w76 9/1 kur. 391-392
  • ‘Sema Moyoni Mwako’

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • ‘Sema Moyoni Mwako’
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1976
  • Habari Zinazolingana
  • “Busara Yako na Ibarikiwe!”
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2017
  • Abigaili na Daudi
    Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia
  • Alitenda kwa Busara
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2009
  • Alitenda kwa Busara
    Igeni Imani Yao
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1976
w76 9/1 kur. 391-392

‘Sema Moyoni Mwako’

NYAKATI nyingine maneno na matendo ya wengine yaweza kukasirisha sana mtu. Wewe unapokasirishwa hivyo, wapaswa kufanya nini? Biblia inapendekeza hivi: “Ufadhaike, lakini usitende dhambi. Sema moyoni mwako, juu ya kitanda chako, nawe unyamae.”​—Zab. 4:4, NW.

Kuna hekima halisi katika shauri hilo. Huenda mtu akawa amekasirika kwa haki. Lakini wakati huo hasa ndipo anapohitaji kujiweza. Kuna hatari ya kupiga kwa ghafula mtu aliyemkasirisha, alipize kisasi na hivyo atende dhambi juu yake. Hiyo yaweza kuleta ugomvi mkali sana. Wakati watu wanapokuwa wamefadhaika sana mara nyingi wanafanya mambo wanayosikitikia sana baadaye. Siku hizi ni kawaida sana kusikia habari za watu walioumiza sana au walioua watu wa ukoo wao na rafiki zao walipokuwa na hamaki (hasira ya ghafula). Naam, shauri ni lenye hekima linalosema mtu atulize kufadhaika kwake saa za usiku zenye utulivu.

Yatupasa tufikirie matokeo ya mambo tunayosema au kutenda ili tusifanye mambo haraka haraka bila kufikiri. Wakati mmoja mtumishi wa Mungu Daudi aliposhindwa kufanya hivyo akamhamakia Nabali, alikaribia kuwa na hatia ya damu. Ilikuwa hivi:

Daudi na watu wake walikuwa wametumikia kama ukuta wa kulinda kundi la wanyama wa Nabali. Baadaye, Daudi alituma wajumbe kwa Nabali kwa sababu ya fadhili walizokuwa wamemtendea, wakamtakie mema na kumwomba msaada wa vitu vya kimwili. Nabali alidharau mambo yenye faida aliyotendewa na Daudi na watu wake, naye akawakemea wajumbe hao. Alipopashwa habari, Daudi aliamua kumwua Nabali pamoja na wanaume wote wa nyumba yake. Lakini mke wa Nabali Abigaili alichukua chakula haraka, akamwendea Daudi na kumwomba sana asitoe adhabu kwa mamlaka yake mwenyewe.​—1 Sam. 25:5-31.

Maneno yake yaliugusa moyo wa Daudi, akasema hivi: “Na ahimidiwe [Yehova], Mungu wa Israeli, ambaye amekuleta hivi leo kunilaki; na ibarikiwe busara yako, na ubarikiwe wewe, uliyenizuia hivi leo nisimwage damu, wala kujilipiza kisasi kwa mkono wangu mwenyewe.”​—1 Sam. 25:32, 33.

Kama ilivyokuwa kwa Daudi, sikuzote si vyepesi kuzuia hasira. Lakini, linakuwa jambo lenye kusaidia mtu asipojifikiria kwa uzito mno akihangaikia mno jina lake. Kuna mfano mzuri wa jambo hilo unaohusu Mfalme Sauli. Aliopochaguliwa kwanza awe mfalme wa Israeli, alikuwa mtu mwenye adabu na mnyenyekevu. Kabla ya kutiwa mafuta awe mfalme alimwambia nabii Samweli hivi: “Je! mimi si Mbenyamini, mtu wa kabla iliyo ndogo kuliko kabila zote za Israeli​—na jamaa yangu nayo si ndogo kuliko jamaa zote za kabila ya Benyamini?” (1 Sam. 9:21) Nia hii ya adabu ilimsaidia baadaye asifanye mambo haraka haraka wakati watu fulani walipomnenea kwa dharau. Maandiko yasema hivi: “Wengine wasiofaa kitu wakasema, Huyu je! atatuokoaje? Nao wakamdharau, wasimletee zawadi. [“Lakini yeye akatulia,” Common Bible]”​—1 Sam. 10:27.

Jambo la maana pia katika kutuliza fadhaa ni kukumbuka uhusiano wako na Muumba. Yehova Mungu hapendelei wale wanaofurahia msiba wa adui, kwa maana kufurahi kwaonyesha roho ya kulipa kisasi. Tunaonywa hivi katika Mithali 24:17, 18: “Usifurahi, adui yako aangukapo; wala moyo wako usishangilie ajikwaapo; [Yehova] asije akaliona hilo, likamkasirisha.”

Mtu aweza kuhatirisha uhusiano wake na Yehova Mungu kwa kuacha fadhaa yake iongezeke kiasi cha kuweka uchungu mwingi moyoni juu ya mtu fulani. Akifanya hivyo, atakuwa akidai kwamba ni haki yake kufanya jambo ambalo Mungu amejiwekea mwenyewe. “Kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena [Yehova].” (Rum. 12:19) Ndiyo sababu Mithali 24:29 yashauri hivi: “Usiseme, Nitamtenda kama. alivyonitenda mimi; nitamlipa mtu huyo sawasawa na tendo lake.” Mtu ajiamuliaye kutumia nguvu ambayo si haki yake kufanya jambo hilo aweza kupoteza nafasi ya kupokea rehema ya Yehova Mungu anapohukumiwa naye.

Kukosa kujiweza kwaweza pia kupotezea mtu heshima yake. Mithali ya Biblia yasema hivi: “Ghadhabu ya mpumbavu hujulika mara; bali mtu mwerevu husitiri aibu.” (Mit. 12:16) Mtu anayehangaika kupita kiasi anapoudhiwa kisha anatenda haraka haraka hujifanya aonekane mpumbavu na wengine. Lakini mwenye hekima hupuza maneno na matendo yenye kukasirisha. Kwa kuzuia ulimi na matendo yake, hafanyi matata kwa sababu ya kutoheshimiwa. Anaacha ionekane kana kwamba hakutendewa jambo lisilo la heshima. Mtu huyo huendeleza heshima yake na vilevile amani yake ya akili, wala hajishushii heshima kwa kuropoka-ropoka maneno yenye aibu.

Tena, mwenye kujiweza hujipatia ushindi wa adili. Ndivyo ilivyokuwa kwa habari ya Yesu Kristo. Yeye angeweza kuwaambia wanafunzi wake hivi: “Jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu.” (Yohana 16:33) Ingawa Yesu alikabiliwa na matisho na matusi, yeye hakufuata njia mbovu za ulimwengu. Mtume Petro aliandika hivi juu yake: “Yeye alipotukanwa, hakurudisha matukano; alipoteswa, hakuogofya; bali alijikabidhi kwake yeye ahukumuye kwa haki.” (1 Pet. 2:23) Kwa kuwa ulimwengu haukufaulu kumfanya Yesu alipize kisasi, yeye aliushinda. Ni jambo lenye kufaa sisi tujipatie ushindi kama huo.

Nyakati nyingine hata watu wanaotukasirisha wanaweza kufaidika tukitulia. Matokeo mema ambayo fadhili yaweza kuwa nayo kwao yakaziwa katika Mithali 25:21, 22: “Adui yako akiwa ana njaa, mpe chakula; tena akiwa ana kiu, mpe maji ya kunywa; maana utatia makaa ya moto kichwani pake; na [Yehova] atakupa thawabu.” Kwa sababu ya kutendewa kwa fadhili, huenda mtu aliyekasirisha mwingine bure akaaibika na kuanza kufikiria maneno na matendo yake kwa uzito. Hiyo huenda ikambadili na kutokeza sifa bora zake. Hata isipokuwa hivyo, mtu mwenye kuendelea kujiweza na kutolipa kisasi aweza kumtegemea Muumba amthawabishe.

Kwa kweli, sisi tu wenye hekima ‘tukisema mioyoni mwetu’ na kuendelea kujiweza. Kwa kusudi hilo, yatufaa tusitawishe adabu na unyenyekevu. Yatupasa pia tujiangalie tusiwe wenye haraka haraka katika usemi na matendo yetu. Kwa njia hiyo tutaepuka kuhatirisha hali yetu mbele za Yehova Mungu, tena tutahifadhi heshima yetu, na kupata ushindi wa adili, na hata huenda tukasaidia wenye kutuchokoza wabadili njia zao ziwe bora.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki