Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w77 11/1 kur. 503-504
  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1977
  • Habari Zinazolingana
  • Jinsi Kugeuka Umbo kwa Kristo Kwakuathiri Wewe
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1991
  • Yesu Ajapo Katika Utukufu wa Ufalme
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1997
  • Kugeuka Sura​—Wamwona Yesu Katika Utukufu
    Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
  • Kusudi la Kugeuka (kwa Yesu)
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1975
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1977
w77 11/1 kur. 503-504

Maswali Kutoka kwa Wasomaji

● Yesu alikuwa na maana gani alipowaambia mitume wake kwamba wengine wao wangemwona akija katika ufalme wake kabla hawajafa?

Leo, katika sehemu ya kaskazini ya mbali ya Golan Heights ndiko kiliko kijiji cha Baniyas ambapo ndipo ilipokuwa Filipi Kaisaria ya kale, ambapo Yesu alikuwa aliposema jambo lililohusu jinsi angegeuka sura baada ya siku kadha.

Yesu alisema: “Amin, nawaambieni, Pana watu katika hawa wasimamao hapa, ambao hawataonja mauti kabisa, hata watakapomwona Mwana wa Adamu akija katika ufalme wake.”​—Mt. 16:28.

Utimizo wa unabii wa Biblia siku zetu unaonyesha kwamba kuwapo kwa Yesu katika mamlaka ya Ufalme kulianza mwaka 1914 W.K. (Mt. 24:3-14; 25:31-33) Ni wazi kwamba Mathayo 16:28 haitaji tukio hilo, kwa maana hapo Yesu alisema jambo ambalo lingetukia kabla mitume hawajafa wote. Basi hilo lilikuwa tukio gani?

Maandiko ya Kiebrania yalikuwa yametabiri kwamba Masihi angekuwa mfalme wa milele. (Mwa. 49:10; 2 Sam. 7:12-16; Isa. 9:6, 7) Njozi ya Danieli hasa iliwapa Wayahudi sababu ya kutazamia utawala wa Masihi uwe mtukufu, wenye mamlaka na fahari. (Dan. 2:44; 7:13, 14) Lakini ni nani hasa angekuwa mfalme wa Kimasihi, na je! angetawala akiwa katika kiti cha enzi cha kidunia? Hata wanafunzi wa Yesu waliokubali kwamba ndiye Masihi wangeweza kufaidika kwa kuhakikishiwa kwamba angetawala akiwa mbinguni, akiwa na mamlaka na utukufu.​—Mt. 16:16-22; Matendo 1:6.

Kwa hiyo, muda unaopungua mwaka mmoja kabla Yesu hajafa, alieleza kwamba wengine wa mitume ‘wangemwona Mwana wa Adamu akija katika ufalme wake,’ au, kama Marko alivyosema, ‘wangeuona ufalme wa Mungu umekuja kwa nguvu.’ (Mt. 16:28; Marko 9:1) Baada ya Yesu kutoka kati yao, wanafunzi wangeweza kupata nguvu kwa sababu ya kujionea mapema kuwapo kwake kwa wakati ujao katika mamlaka ya Ufalme.

Lakini maneno ya Yesu katika Mathayo 16:28 yalitimizwaje? Mara nyingi maana ya mstari inaonyeshwa na maneno yanayouzunguka. Katika habari hii, masimulizi yote matatu ya Injili yanayohusu ahadi ya Yesu juu ya kumwona katika ufalme wake yanaeleza wazi kugeuka kwa sura yake.

Karibu juma moja baada ya Yesu kusema aliyosema katika Mathayo 16:28, alichukua baadhi ya mitume (Petro, Yakobo na Yohana) akawapeleka juu ya mlima mrefu, labda Mlima Hermoni. Akiwa huko aligeuzwa sura akaonekana katika njozi akiwa pamoja na Musa na Eliya. Halafu Mungu akasema: “Huyu ni Mwanangu, mteule wangu, msikieni yeye.”​—Luka 9:28-35; Mt. 17:1-5; Marko 9:2-6.

Kugeuka sura kwa Yesu kulikuwa njozi iliyomwonyesha akiwa katika mamlaka ya Ufalme na utukufu wa mbinguni, kama Petro alivyohakikisha baadaye. Akitaja kugeuka huko, Petro alieleza kwamba kwa njia hiyo wao walikuwa ‘wameuona wenyewe ukuu wake.’ Aliendelea kusema kwamba wakati Yesu alipogeuka sura “alipata kwa Mungu Baba heshima na utukufu.” (2 Pet. 1:16-18) Kwa hiyo, inaonekana kwamba wakati Yesu aliposema kwamba kabla hajafa baadhi ya mitume wangemwona katika ufalme wake, alikuwa akitaja tamasha ya kugeuka sura ambayo baadhi yao waliiona muda mfupi baadaye.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki