Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w75 4/15 kur. 188-190
  • Kusudi la Kugeuka (kwa Yesu)

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kusudi la Kugeuka (kwa Yesu)
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1975
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • KUGEUKA
  • USHUHUDA WA UTUKUFU WA KRISTO UNAOKUJA
  • “LILE NENO LA UNABII LILILO IMARA ZAIDI”
  • Jinsi Kugeuka Umbo kwa Kristo Kwakuathiri Wewe
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1991
  • Kugeuka Sura​—Wamwona Yesu Katika Utukufu
    Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
  • Yesu Ajapo Katika Utukufu wa Ufalme
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1997
  • Mtazamo-Kimbele wa Utukufu wa Ufalme wa Kristo
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1988
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1975
w75 4/15 kur. 188-190

Kusudi la Kugeuka (kwa Yesu)

JE! WEWE waamini kwamba Kristo atatawala dunia kweli kama Mfalme? Ikiwa ndivyo, je! atatawala akiwa katika kiti cha enzi cha kidunia au cha kimbinguni? Au wadhani alikuwa mtu wa kutokeza tu, mwalimu?

Ni kwa kusudi la kutoa jibu la hakika, la kutegemeka kwa maulizo haya, na kuwa na watu wa kushuhudia kwa macho yao wenyewe kwa usahihi na bila wasiwasi juu ya uhakika wa utawala wake wa kimbinguni, kwamba njozi ya kugeuka ilipewa kwa mitume watatu, na masimulizi yake yakahifadhiwa katika maandishi.

Ili kuelewa kusudi la kugeuka, yatupasa turudie mazungumzo ambayo Yesu alikuwa nayo pamoja na wanafunzi wake siku chache tu mapema. Walikuwako wakati Mafarisayo na Masadukayo walipoomba ishara kwa mashaka​—⁠yaelekea wakitaka Yesu aje kwa kuonekana katika mawingu ya mbinguni. Lakini Yesu aliwaambia watu hao wachoyo na waovu kwamba wangepokea ishara ya kidunia tu​—⁠ishara ya nabii Yona.​—Mt. 16:4.

Muda fulani baadaye Yesu aliwauliza wanafunzi wake maoni ya watu kwa ujumla: “Watu hunena Mwana wa Adamu kuwa ni nani? Wakasema, Wengine hunena u Yohana Mbatizaji, wengine Eliya, wengine Yeremia au mmojawapo wa manabii.”​—Mt. 16:13, 14.

Baada ya kuhakikisha maoni ya watu, Yesu aliuliza: “Nanyi mwaninena mimi kuwa ni nani?” Simoni Petro akajibu: “Wewe ndiwe Kristo [Masihi], Mwana wa Mungu aliye hai.” Mungu ndiye aliyewafunulia mitume hili kwa sababu ya imani yao; lakini bado walihitaji kujua mengi zaidi juu ya Masihi, mambo aliyopaswa kufanya na utukufu ambao angepewa na Mungu. Kwa hiyo, Yesu akaanza kueleza kwamba yampasa aende Yerusalemu na kupatwa na mengi na kuuawa. Petro alijaribu kumsihi asiende kwa kusema: “Hasha, Bwana, hayo hayatakupata.” Itikio la Petro lilionyesha kwamba hakuelewa kabisa kwamba Yesu alipaswa afe kifo cha dhabihu, na kwamba angefufuliwa kwenye uzima wa Kimbinguni. Wala Petro hakuelewa kwamba Ufalme ungetawala kutoka mbinguni, ukianza muda mwingi baada ya kufa kwa mitume, wakati wa parousia ya Kristo, au kuwapo kusikoonekana katika utukufu na uwezo. Mara hiyo Yesu alimsahihisha Petro, akisema: “Huyawazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu.”​—Mt. 16:15-23.

Yesu alijua kwamba mitume wake walikuwa na maoni ya kibinadamu juu ya ufalme wake, wakidhani angetawala kutoka kiti cha enzi cha kidunia. Lakini ilikuwa lazima kwa watu hawa, ambao wangekuwa nguzo katika kundi la Kikristo, wawe mashahidi wa ukweli wa kuwapo kwake kwa kimbinguni kwa wakati ujao katika mamlaka ya Ufalme. (Gal. 2:9) Baada ya kifo chake na kufufuliwa, si wakati huo, ingewapasa kuuimarisha ukweli huu mkubwa, fundisho hili la maana, katika kundi. Kwa hiyo aliwaambia maneno haya ya kusifika:

“Mwana wa Adamu atakuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika zake . . . Amin, nawaambieni, Pana watu katika hawa wasimamao hapa, ambao hawataonja mauti kabisa, hata watakapomwona Mwana wa Adamu akija katika ufalme wake.”​—Mt. 16:24-28.

KUGEUKA

Siku chache baadaye maneno ya Kristo yalitimizwa. Alimchukua Petro, Yakobo na Yohana katika mlima mrefu sana. Hakuwa na haja ya kuchukua mitume wake wote. Mashahidi watatu walitosha, kama Torati ilivyohitaji. (Kum. 19:15; 2 Kor. 13:1) Masimulizi ya Luka ya tamasha ya kugeuka yasema hivi:

“Ikawa katika kusali kwake [Yesu] sura ya uso wake ikageuka, mavazi yake yakawa meupe, yakimeta-meta. Na tazama, watu wawili walikuwa wakizungumza naye, nao ni Musa na Eliya; walioonekana katika utukufu, wakanena habari za kufariki kwake [exodos, Kigiriki] atakakotimiza Yerusalemu. Petro na wale waliokuwa pamoja naye walikuwa wamelemewa na usingizi; lakini walipokwisha amka waliuona utukufu wake, na wale wawili waliosimama pamoja naye. Ikawa hao walipokuwa wakijitenga naye, Petro alimwambia Yesu, Bwana mkubwa, ni vizuri sisi kuwapo hapa; na tufanye vibanda vitatu; kimoja chako wewe, na kimoja cha Musa, na kimoja cha Eliya; hali hajui asemalo. Alipokuwa akisema hayo, lilitokea wingu likawatia uvuli, wakaogopa walipoingia katika wingu hilo. Sauti ikatoka katika wingu, ikisema, Huyu ni Mwanangu, mteule wangu, msikieni yeye. Na sauti hiyo ilipokwisha, Yesu alionekana yu peke yake.”​—Luka 9:29-36.

Bila shaka njozi hii ilitokea usiku, kwa maana walikuwa wakisinzia, nao hawakushuka kutoka mlimani mpaka kesho yake. Lakini walikuwa macho walipokuona kugeuka. Ebu uwazie mshangao wa mitume walipokuwa wakiiona sura ya Yesu iking’aa kama jua, na mavazi yake yakimeremeta kwa weupe! Muda mwingi mapema Musa aliweza kuficha utukufu wa uso wake kwa utaji, baada ya kurudi kutoka mlimani ambako Mungu alisema naye, lakini utukufu wa Kristo ulio mwingi zaidi kuliko huo uliifanya sura yake yote tukufu hata zaidi, yenye kumetameta.​—Kut. 34:29-35; linganisha 2 Wakorintho 3:7-11.

USHUHUDA WA UTUKUFU WA KRISTO UNAOKUJA

Hapa, mbele ya macho ya mitume, ulikuwapo ushuhuda wa kwamba kuwapo kwa Yesu katika mamlaka ya Ufalme kungekuwa kutukufu na kwa kimbinguni. Pia, mazungumzo ya Musa na Eliya wa njozi juu ya kufa kwa Yesu yalikuwa uhakikisho wa kwamba kifo chake cha aibu hakikuwa jambo lililopaswa kuepukwa, kama Petro alivyotaka. Katika njozi hii, Musa, aliyetumiwa na Mungu awape Israeli Torati, alilifananisha agano la Torati. Eliya aliwafananisha manabii wale wengine. Torati na manabii ilikuwa imemtabiri Kristo, maisha yake, mateso yake, dhabihu yake, utukufu wake. Yote yalielekeza kwenye Kristo. Kama vile mtume Paulo alivyosema: “Torati imekuwa kiongozi kutuleta kwa Kristo.” (Gal. 3:24; Rum. 10:4) Na, kwa habari ya manabii wengine, baadaye malaika alimwambia mtume Yohana hivi: “Ushuhuda wa Yesu ndio roho ya unabii.”​—Ufu. 19:10.

Pia, Kristo ni Kiongozi na Mkombozi, kama Musa alivyokuwa. Yeye ndiye Mpatanishi wa agano jipya, kama vile Musa alivyokuwa mpatanishi wa agano la Torati. (Gal. 3:19; Ebr. 9:15) Yehova alikuwa amemwambia Musa hivi: “Mimi nitawaondokeshea nabii miongoni mwa ndugu zao mfano wako wewe, nami nitatia maneno yangu kinywani mwake, naye atawaambia yote nitakayomwamuru. Hata itakuwa, mtu asiyesikiliza maneno yangu atakayosema yule kwa jina langu, nitalitaka kwake.”​—Kum. 18:18, 19; Matendo 3:22, 23, 26.

Kristo angeendesha kazi kama Eliya. Nabii Malaki alikuwa amekwisha andika ahadi ya Yehova: “Angalieni, nitawapelekea Eliya nabii, kabla haijaja siku ile ya [Yehova], iliyo kuu na kuogofya.” Eliya alikuwa amefanya kazi kubwa kuirudisha ibada safi. (1 Fal. 18:25-29, 40) Yohana Mbatizaji alifanya hivyo kwa Israeli. (Luka 1:17; Mt. 17:12, 13) Lakini, wakati wa kugeuka kwa Yesu, Yohana huyu alikuwa amekwisha kufa. Kwa hiyo kutokea kwa Eliya njozini kungeonyesha kwamba Kristo angeendesha kazi kubwa zaidi, kurudisha ibada safi daima. Hii ilipaswa itukie “kabla haijaja siku ile ya [Yehova], iliyo kuu na kuogofya,” itakayotokea wakati Mungu atakapofikiliza hukumu juu ya waabudu wa uongo na hii taratibu mbovu ya mambo.​—Mal. 4:5, 6.

Njozi ilikuwa hakika sana hata Petro akaanza kushiriki katika tamasha, kwa wazi akiwa ameshikwa sana na hofu na shukrani. Alipowaona wale wanaume wawili wa njozi “walipokuwa wakijitenga naye [Yesu],” yaelekea hakutaka waondoke. Kwa hiyo alisema juu ya kufanya vibanda, “hali hajui asemalo.”

Walakini, tukio hilo lilikuwa njozi, Musa na Eliya wakiwa wa njozi tu. (Mt. 17:9) Kwa maana Musa alikuwa amekwisha kufa na alikuwa angali katika kaburi lake. (Kum. 34:5, 6; linganisha Matendo 2:29.) Eliya alichukuliwa juu katika gari la moto mpaka angani, lakini si kuingia katika mbingu za Mungu. Kwa kweli, alihamishwa au akasafirishwa kwenye mgawo mwingine duniani. Kwa kweli, miaka mingi baadaye Eliya, akiwa angali hai, aliandika barua ya unabii kwa Yehoramu, mfalme wa Yuda. (2 Nya. (Sik.) 21:12) Baadaye Eliya alikufa, sawa na wanadamu wote. Wala yeye wala Musa hakufufuliwa kwenye uzima wa milele kabla ya Kristo, ambaye ndiye “mzaliwa wa kwanza wa waliokufa.” Yesu mwenyewe, alipokuwa duniani, alisema hivi: “Hakuna mtu aliyepaa mbinguni.”​—Ufu. 1:5; Yohana 3:13.

Petro alipokuwa akisema, wingu lilifanyika likawafunika. Hii ilikuwa ishara ya kuwapo kusikoonekana kwa Yehova. (Kut. 16:10; 1 Fal. 8:10) Halafu, katika mmojawapo wa nyakati ambazo sauti ya Yehova mwenyewe ilisikiwa, Yeye alitoa ushuhuda wake mwenyewe juu ya Umasihi wa Yesu, akisema: “Huyu ni Mwanangu, mteule wangu, msikieni yeye.”​—Luka 9:35.

“LILE NENO LA UNABII LILILO IMARA ZAIDI”

Lo! ni uhakikisho wenye kukata maneno na wa kuogofya namna gani waliopewa mitume hawa watatu wakati huo! Lo! ushuhuda wao juu ya Umasihi wa Kristo sasa ungekuwa wenye nguvu na wenye kusadikisha namna gani! Kwa kweli, ‘hawakuwa wameonja mauti’ kabla ya kuuona wonyesho huu wenye kutazamisha wa kuwapo kwa Kristo kwa wakati ujao katika utukufu wa Ufalme. Zaidi ya miaka 30 baadaye mtume Petro aliandika hivi:

“Maana hatukufuata hadithi zilizotungwa kwa werevu, tulipowajulisha ninyi nguvu zake Bwana wetu Yesu Kristo na [kuwapo kwake, parousia, kuwapo kusikoonekana katika mamlaka ya Ufalme]; bali tulikuwa tumeuona wenyewe ukuu wake. Maana alipata kwa Mungu Baba heshima na utukufu, hapo alipoletewa sauti iliyotoka katika utukufu mkuu, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye. Na sauti hiyo sisi tuliisikia ikitoka mbinguni tulipokuwa pamoja naye katika mlima ule mtakatifu. Nasi tuna lile neno la unabii lililo imara zaidi, ambalo, mkiliangalia, kama taa ing’aayo mahali penye giza, mwafanya vyema, mpaka kutakapopambazuka, na nyota ya asubuhi kuzuka mioyoni mwenu.”​—2 Pet. 1:16-19.

Yaelekea mtume Yohana, alikuwa akiikumbuka tamasha hii sana alipoandika hivi karibu miaka 66 baada ya njozi ya kugeuka kwa Yesu: “Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.”​—Yohana 1:14.

Leo “nyota ya asubuhi” ambayo Petro alisema juu yake imetokea. Yesu Kristo ametawazwa katika utukufu wa Ufalme mwishoni mwa Majira ya Mataifa katika mwaka wa 1914 C.E.! Ikiwa ‘tumeuangalia unabii mioyoni mwetu,’ neno la unabii linaimarishwa kwetu zaidi kuliko lilivyokuwa kwa mitume. Kristo ametimiza yaliyoandikwa juu yake kwa unabii katika Torati na katika Manabii. Sasa yeye anawaongoza watu wake kama alivyofanya Musa, dunia ya paradiso yenye haki ikiwa karibu tu mbele ya wale wanaomkubali yeye sasa na kufuata uongozi wake. Je! wewe unalichukua kwa uzito neno la unabii na neno la mashahidi wa kweli walioona kwa macho yao wenyewe utukufu wake? Je! unakuelewa kuwapo kwake kusikoonekana katika mamlaka ya Ufalme? Ikiwa ndivyo, una upendeleo mwingi sana sasa, nawe unalo tumaini zuri ajabu ambalo lingali mbele yako.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki