Msingi wa Kumwamini Mungu
MOJAWAPO la maelezo yanayotolewa na kamusi moja juu ya imani ni “kusadiki sana jambo lisilo na uthibitisho bila mashaka.” Lakini, elezo hilo laeleza kwa usahihi zaidi kule kuamini bila ushuhuda. Kuamini bila ushuhuda si imani. Kule kumwamini Mungu Muumba kunakotakiwa na Biblia, ambako inatolea msingi, ni imani iliyo juu ya ushuhuda wa wazi na kuwaza kuzuri.
Inasemekana kwamba wanasayansi wanaamini kanuni za msingi zinazoongoza maarifa yao mbalimbali. Mkulima hulima akiwa na imani katika utaratibu wa majira. Mifano mingi ingeweza kutolewa kuonyesha kwamba wanadamu wanatumaini na kuamini kutegemeka na utaratibu wa majira na kawaida zinazouongoza ulimwengu wote. Kwa kweli, utaratibu huu peke yake wathibitisha kuwako kwa Muumba mwenye akili. Wataalamu wa nyota waliweza kujua kwamba kuna sayari fulani, na wakajua mahali pazo kabla hazijaonekana, kwa kupima mwendo wa jua, mwezi na nyota kupatana na kawaida hizo za asili. Hali kadhalika, wanasayansi fulani waliweza kujua kwamba kuna vitu fulani vya asili visivyoweza kugawanywa na kugeuzwa viwe vitu vya namna nyingine (elements), wakaeleza jinsi vinavyofanya kazi, kabla vitu hivyo vya asili havijavumbuliwa, kwa sababu waliona utaratibu wa kawaida zinazoviongoza. Basi, kwa nini wanasayansi, wakulima na wengine wasimtumaini na kumwamini Yeye aliyezifanya kawaida hizi za asili?
Biblia inapotumia neno hili “imani,” linaweza kusemwa kwamba lahusiana na mambo ya aina mbili: Kwanza, uhakika wa mambo yanayotumainiwa, mambo yasiyoonwa kwa sababu yako wakati ujao. Na, pili, kuamini kwamba kuna watu wa kiroho, wasioonwa kwa macho ya kibinadamu kwa sababu si wenye miili ya asili; yaani, kumwamini Mungu na kuziamini ahadi zake. Kwa hiyo tunasoma hivi katika Waebrania 11:1 (New English Bible): “Imani ni nini? Imani inayapa matumaini yetu maana, na hutufanya tuwe na hakika ya mambo yaliyoko tusiyoyaona.” Ndiyo sababu twaambiwa kwamba yawapasa Wakristo watembee kwa imani si kwa kuona.—2 Kor. 5:7.
Kuamini kwamba kuna Mungu kwaweza kuthibitishwa sana kwa kufikiria uwezo na hekima inayoonekana katika vitu vilivyoumbwa ambavyo huonekana, kutia na utaratibu na upatano wavyo. Watu wote wenye akili watakubali kwamba kila tokeo lina chanzo chake kinachofaa. Saa yathibitisha kwamba kuna fundi wa saa. Basi, tukitazama po pote ulimwenguni, tangu jicho la mdudu, ambalo ni gumu sana kufahamu, mpaka makundi makubwa ya nyota za anga ya juu, tunakata shauri kwamba bila shaka kuna Muumba mwenye nguvu na mwenye hekima, aliyevifanya vitu hivi.
Bado kuna watu wengi wasioamini kwamba kuna Mungu. Na kwa kuwa wengi wa watu hawa ni wanasayansi, wengine hukata shauri bila kufikiri kwamba ni jambo lisilopatana na sayansi kuamini kwamba kuna Mungu Muumba. Lakini sivyo, kama alivyosema mwalimu wa Chuo Kikuu cha Pennsylvania wakati mmoja. Alipokuwa akizungumza juu ya kusadikika kwa miujiza inayotajwa na Biblia, alisema kwamba uwezo wa Mungu ambao wanasayansi hawajakubali bado, ndio uliofanya hii. Aliendelea kusema kwamba, “wanasayansi wengi si Wakristo, lakini hiyo si kwa sababu ni wanasayansi. Wafanya biashara wengi wala waandikaji wa habari si Wakristo; hasa, watu wengi si Wakristo.”
Taarifa inayohusiana na haya ni ile iliyotokea miaka kadha iliyopita katika gazeti New York Journal-American. Ilieleza hivi: “Kwa miaka mingi, wanasayansi walionwa na watu wengi kuwa wasioamini kuwako kwa Mungu. Lakini leo, . . . wakati sayansi karibu imekuwa kawaida ya maisha, wazo hili haliko hivyo tena. Juma hii, watu wanane kati ya wanasayansi mashuhuri wa taifa waliombwa na waandishi wa gazeti N.Y. Journal-American watoe maoni yao juu ya ulizo hili: ‘Je! wanasayansi humwamini Mungu?’ Kwa majibu yao, wazo moja la msingi lafunuka waziwazi: Uwezo fulani wa Kimungu, usio wa kibinadamu, umeumba ulimwengu. Miaka iliyopita, wanasayansi walieleza maoni yao kwanza juu ya kisa hiki. Tangu wakati huo hakuna walioona sababu yo yote ya kubadili maoni yao.”
Wernher von Braun, mtaalamu wa roketi, ambaye ni mmojawapo wale wanane waliotajwa, alijibu hivi: “Kwa nini namwamini Mungu? Kwa urahisi, sababu kubwa ni hii: Bila shaka dunia yetu na ulimwengu wote ulioumbwa kwa utaratibu na kwa ukamilifu una Muumba, mbuni mkuu. Uumbaji huu wenye utaratibu na mkamilifu sana, wenye kusawazika sana na wenye fahari sana, ni mazao tu ya Mungu. Bila shaka kuna Muumba; hakuna njia nyingine.”
Dkt. William Swann, mwanasayansi mwingine kati ya wale wanane, mtaalamu mashuhuri wa elimu ya miale ya nuru ya anga za juu, alisema mamoja hivi: “Mwanasayansi hutaka kutofautisha uhakika na kukisia tu. Basi nikiutazama ulimwengu mzima, napata uhakika wa kwamba ulibuniwa kwa njia ya akili. Kwa kusema hivi ninamaanisha kwamba ulimwengu wote waonyesha vizuri sana uhusiano wa kazi zake na mipango yake mizuri kama ile ambayo mhandisi anajitahidi kutimiza katika shughuli zake ndogondogo.”
Vilevile, Dkt. Warren Weaver, ambaye ni mwanasayansi na mmojawapo wataalamu mashuhuri wa hesabu wa huko Amerika, alisema wakati mmoja katika gazeti mashuhuri la kila mwezi hivi: “Kila uvumbuzi mpya wa sayansi unafunua zaidi utaratibu ambao Mungu ameweka katika ulimwengu Wake wote. Mungu hupata heshima na uweza wakati sababu na utaratibu Wake zinapofunuliwa.”
Halafu kuna ushuhuda pia wa Sir Isaac Newton, ambaye ametajwa kuwa “mtaalamu mkuu kuliko wote waliopata kuonwa na ulimwengu.” Habari za maisha yake zilizochapwa hivi karibuni zilisema hivi, “Karibu uchunguzi wote aliofanya Newton ulikuwa na kusudi la kumjua Mungu” nayo “elimu ya sayansi ilifuatwa iweze kufundisha wanadamu habari za Mungu.” Ushuhuda wote huo, unaoweza kuzidishwa zaidi ya mara elfu moja, wapatana na maneno ya mtume Paulo yaliyoongozwa na Mungu ya kwamba “mambo [ya Mungu] yasiyoonekana tangu kuumbwa ulimwengu yanaonekana, na kufahamika kwa kazi zake; yaani, uweza wake wa milele na Uungu wake; hata [watu wanaokana kwa maneno au kwa matendo kwamba hakuna Mungu] wasiwe na udhuru.”—Rum. 1:20.
UFUNUO WA KIMUNGU UNATAKIWA ILI KUMWAMINI MUNGU
Walakini, na tukumbuke kwamba kuamini vivi hivi tu kwamba kuna Mungu hakutoshi. Si sawa na kuwa na imani ya kweli na iliyo hai katika Mungu mwenyewe. Kwa mfano, matokeo ya kura yaliyochapwa mwishoni mwa mwaka 1976 yalionyesha kwamba watu wa Australia 76 kwa mia “humwamini Mungu.” Lakini je! kweli wanayaamini yale ambayo Mungu anasema na yale anayofanya, au wanaamini tu kwamba yeye yuko? Kama Yakobo, mwandikaji wa Biblia anavyosema, hata malaika wabaya, mashetani, huamini kwamba kuna Mungu—nao hutetemeka kwa hofu. Kwa wazi hawana imani katika Mungu. (Yak. 2:14, 19) Imani ya kweli katika Mungu si kuamini kwamba yuko tu, bali inahusu pia tumaini na kuwa na hakika kwamba Mungu ni mtu. Kama Biblia inavyosema: “Pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na [zaidi ya hayo] kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao” kwa bidii. (Ebr. 11:6) Imani haihusu akili tu, bali yahusu moyo pia, ndiyo, mwanadamu mzima.
Kwa wazi, ili kumwamini Mungu vizuri hatutakiwi tujifunze kinachoitwa “kitabu cha Maumbile tu.” Uumbaji waweza kushuhudia fahari, hekima na uweza wa Muumba, lakini hauwezi kujibu maulizo haya: Jina la Mungu ni nani? Kwa nini alituumba sisi, tena wakati gani? Kusudi la kuishi ni nini? Tumaini letu la mwisho ni nini? Tuna wajibu gani kwa Mungu na wanadamu wenzetu? Kwa nini ulimwengu umejaa fujo hivi? Mungu ataka tufanye nini ili tuje tuokoke msiba wa ulimwengu uliotabiriwa katika Neno lake na ambao wakaribia sana?
Ebu fikiri: Muumba alitupa uwezo wa kufikiri, wa kustaajabu, wa kutumia mawazo yetu na kuuliza maulizo kama haya. Bila shaka hangetutesa kwa kutuacha bila majibu, sivyo? Kwa kweli Mungu ametia katika mioyo na akili zetu kutamani maarifa, na aina fulani za maarifa anazoweza yeye peke yake kutoa. Je! si jambo la busara kukata shauri kwamba Mungu angetosheleza tamaa zetu za kujua mambo haya? Vilevile, yeye alituumba sisi tuwe na tamaa nyingine za asili—tamaa ya chakula na kinywaji, tamaa ya uzuri wa macho na wa kusikia, na kadhalika. Je! hakufanya mpango ili tuweze kutosheleza tamaa hizi kwa kujitahidi? Zaidi ya hayo, Muumba alitoa mahitaji yote ya wanyama. Je! hawapendi sana wanadamu? Ni jambo la busara kwamba angetutolea majibu—kupitia kwa ufunuo wa kimungu. Biblia ndio ufunuo huo wa kimungu, na tunapoichunguza tunaona kwamba kweli ndio ufunuo wa kimungu.
Biblia imetajwa kwa kufaa kuwa mwanga wa ustaarabu na wa uhuru. Sehemu zake kama Amri Kumi, Mahubiri ya Mlimani, na zaburi na mithali zake peke yake, zingetosha kuifanya kuwa bora. Kwa mfano, mara nyingi Amri Kumi zimefananishwa na Amri za Hammurabi, kama kwamba Amri hizo zilitungwa kwa mfano huo. Hiyo si kweli. Amri Kumi hizi zinakazia ibada ya Yehova Mungu; lakini Amri za Hammurabi, zinakazia mambo ya ulimwengu tu. Hata kuna tofauti kubwa katika kuzungumza mambo ya ulimwengu. Amri Kumi hazikatazi kuua tu, bali vilevile sehemu nyingine ya torati ya Musa huamuru adhabu ya kifo itolewe kwa uuaji wa kukusudia na kutofautisha uuaji wa kukusudia na uuaji usio wa kukusudia. (Hes. 35:9-34) Tofauti na hayo, kama Encyclopedia Britannica kinavyoeleza, katika Amri za Hammurabi, “maneno yaliyoachwa katika amri hizo ni yale ya uuaji wa kukusudia, na haijulikani jinsi uuaji huo ulivyotolewa adhabu wala waliopatiliza adhabu hiyo.” (Encyclopcedia Britannica, 1971, Vol. II, ukurasa wa 43) Angalia pia ile ya mwisho ya Amri Kumi, “Usitamani.” (Kut. 20:17) Torati hiyo ni ya namna ya pekee kwa kusimulia habari za sheria. Ni sheria inayoonyesha chanzo chenyewe cha uhalifu, lakini kufikilizwa kwayo kwategemea sana mtu mwenyewe!
Kwa busara, Biblia huanza na habari ya uumbaji. Labda itasemwa kwamba iliamsha hamu ya Albert Einstein, aliyesema wakati mmoja hivi: “Mimi nataka kujua jinsi Mungu alivyoumba ulimwengu huu. . . . Nataka kujua mawazo Yake.” Habari ya Biblia juu ya uumbaji inapatana na fikira za wanasayansi wengi leo, ijapokuwa uhakika huu hauthaminiwi na watu wengi.
Kulingana na habari hii, ebu sikia maneno ya mtaalamu mashuhuri Mwamerika wa elimu ya mawe, Wallace Pratt: “Kama mimi niliye mtaalamu wa elimu ya mawe ningeombwa nieleze kifupi mawazo yetu ya kisasa juu ya mwanzo wa dunia na jinsi uhai ulivyositawi juu yake mpaka kukawa na watu wenye kuishi mashambani na mifugo, kama makabila yaliyotajwa na Kitabu cha Mwanzo, ningeweza kuufuata sana usemi ule wa sura ya kwanza ya Mwanzo.” Na kwa habari ya muda wa zile siku za uumbaji zinazotajwa katika Mwanzo, mwanasayansi huyu anauliza kwa busara hivi: “Je! hatuhakikishwi kwamba, ‘siku moja kwa Muumba ni kama miaka elfu na miaka elfu ni kama siku moja?’” Je! mwandikaji wa habari ya Mwanzo angaliwezaje kupata habari na ufahamu huu bila kuongozwa na Mungu?
Zaidi ya hayo, waandikaji wa Biblia wanaonyesha unyofu unaothibitisha habari zao kuwa za kweli. Kwa njia hiyo hakuna mtu anayefaa kusema kwamba walificha makusudi yao. Ebu angalia yale ambayo Biblia inasema juu ya makosa hata ya watu mashuhuri wenye imani. Inasema juu ya kulewa kwa Nuhu; juu ya ngono za Yuda na mwanamke ambaye alidhani ni kahaba wa hekaluni; juu ya kukasirika kwa Musa; juu ya makosa ya Daudi, uzinzi wake pamoja na Bathsheba, ambao matokeo yake yakawa kifo cha mume wake; na juu ya kushindana kwa mitume wa Yesu. Bila shaka maandishi ya Biblia ni yenye unyofu wa kweli, kwa vile yanaeleza waziwazi, si mambo mema tu ya watu hawa waaminifu, bali na makosa yao pia.
Lo! jinsi tabia ya kibinadamu inavyoelezwa waziwazi katika Biblia! Kumekuwako mabadiliko kidogo sana kwa muda wa miaka elfu sita! Kwa mfano, karibu na mwanzo wa Maandishi ya Kimungu tunaona makosa ya kibinadamu ya wivu. Mwana wa Kwanza wa Adamu na Hawa amwua ndugu yake kwa sababu ya hasira kali yenye wivu. Baadaye wivu ule ule waongoza ndugu za Yusufu watake kumwua. Mfalme Sauli anamwonea Daudi wivu kwa sababu ya kufanikiwa kwake na kupendwa na watu wengi hata anataka kumwua. Maandishi ya Biblia ni ya kweli kwa vile yanazungumza matukio ya kweli katika maisha kama haya na mengine mengi.
Tena, kwa vile Biblia ni ufunuo ambao Mungu amewapa wanadamu, twaweza kutazamia bila shaka kwamba ingeenezwa zaidi mahali pote kuliko kitabu cho chote—na katika lugha nyingi zaidi ili ipatikane na watu wengi zaidi wanaoishi duniani. Nasi twaona ndivyo ilivyo. Mwaka 1975 peke yake, theluthi ya nakala bilioni moja za Biblia nzima au sehemu zake zilienezwa, nayo Biblia yapatikana sasa ikiwa nzima au nusu yake katika lugha 1,575.
Walakini, sababu yetu kubwa zaidi ya kuikubali Biblia kuwa Ufunuo wa Kimungu ni kutimizwa kwa unabii wake mwingi sana. Habari nyingi za kuzaliwa kwa Yesu, shughuli zake hadharani na kufa kwake zilitabiriwa na manabii Waebrania. Kati ya hizi ni mahali pa kuzaliwa kwake, juu ya wakati ambapo angeonekana kama Masihi na kazi yake ya hadhara ya muda wa miaka mitatu na nusu, jinsi alivyopokewa, na vilevile habari za kufa na kufufuliwa kwake.a Na ifahamike kwamba kama vile kuwa na imani katika Mungu kunavyomaanisha kuwa na imani katika Neno lake, Biblia, vivyo hivyo kuwa na imani katika Biblia kunamaanisha kuwa na imani katika Yesu Kristo kama Mwokozi wa wanadamu na Mfalme wa ufalme wa Mungu.
[Maelezo ya Chini]
[Blabu katika ukurasa wa 463]
‘Walakini, sababu yetu kubwa zaidi ya kuikubali Biblia kuwa Ufunuo wa Kimungu ni kutimizwa kwa unabii wake mwingi sana.’
[Chati katika ukurasa wa 460, 461]
(Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa)
Orodha hii ya vitu vya asili visivyoweza kugawanywa na kugeuzwa viwe vitu vya namna nyingine imetolewa katika inayoitwa Periodic Table of the Elements. Kwa sababu ya utaratibu wa vitu, wanasayansi waliweza kujua kwamba kuna vitu fulani vya asili visivyogawanyikana, wakaeleza jinsi vinavyofanya kazi, kabla vitu hivyo vya asili havijatofautishwa kimoja kimoja. Je! utaratibu huo wa vitu ulijitokeza wenyewe tu?
1 Hydrogen 1
2 Helium 2
3 Lithium 2-1
4 Beryllium 2-2
5 Boron 2-3
6 Carbon 2-4
7 Nitrogen 2-5
8 Oxygen 2-6
9 Fluorine 2-7
10 Neon 2-8
11 Sodium 2-8-1
12 Magnesium 2-8-2
13 Aluminum 2-8-3
14 Silicon 2-8-4
15 Phosphorus 2-8-5
16 Kibiriti 2-8-6
17 Chlorine 2-8-7
18 Argon 2-8-8
19 Potassium 2-8-8-1
20 Calcium 2-8-8-2
21 Scandium 2-8-9-2
22 Titanium 2-8-10-2
23 Vanadium 2-8-11-2
24 Chromium 2-8-13-1
25 Manganese 2-8-13-2
26 Chuma 2-8-14-2
27 Cobalt 2-8-15-2
28 Nickel 2-8-16-2
29 Shaba Nyekundu 2-8-18-1
30 Zinc 2-8-18-2
31 Gallium 2-8-18-3
32 Germanium 2-8-18-4
33 Arsenic 2-8-18-5
34 Selenium 2-8-18-6
35 Bromine 2-8-18-7
36 Krypton 2-8-18-8
37 Rubidium 2-8-18-8-1
38 Strontium 2-8-18-8-2
39 Yttrium 2-8-18-9-2
40 Zirconium 2-8-18-10-2
41 Niobium 2-8-18-12-1
42 Molybdenum 2-8-18-13-1
43 Technetium 2-8-18-13-2
44 Ruthenium 2-8-18-15-1
45 Rhodium 2-8-18-16-1
46 Palladium 2-8-18-18-0
47 Fedha 2-8-18-18-1
48 Cadmium 2-8-18-18-2
49 Indium 2-8-18-18-3
50 Bati 2-8-18-18-4
51 Antimony 2-8-18-18-5
52 Tellurium 2-8-18-18-6
53 Iodine 2-8-18-18-7
54 Xenon 2-8-18-18-8
55 Cesium 2-8-18-18-8-1
56 Barium 2-8-18-18-8-2
57 Lanthanum 2-8-18-18-9-2
58 Cerium 2-8-18-20-8-2
59 Praseodymium 2-8-18-21-8-2
60 Neodymium 2-8-18-22-8-2
61 Promethium 2-8-18-23-8-2
62 Samarium 2-8-18-24-8-2
63 Europium 2-8-18-25-8-2
64 Gadolinium 2-8-18-25-9-2
65 Terbium 2-8-18-27-8-2
66 Dysprosium 2-8-18-28-8-2
67 Holmium 2-8-18-29-8-2
68 Erbium 2-8-18-30-8-2
69 Thulium 2-8-18-31-8-2
70 Ytterbium 2-8-18-32-8-2
71 Lutetium 2-8-18-32-9-2
72 Hafnium 2-8-18-32-10-2
73 Tantalum 2-8-18-32-11-2
74 Tungsten 2-8-18-32-12-2
75 Rhenium 2-8-18-32-13-2
76 Osmium 2-8-18-32-14-2
77 Iridium 2-8-18-32-15-2
78 Platinum 2-8-18-32-17-1
79 Dhahabu 2-8-18-32-18-1
80 Mercury 2-8-18-32-18-2
81 Thallium 2-8-18-32-18-3
82 Risasi 2-8-18-32-18-4
83 Bismuth 2-8-18-32-18-5
84 Polonium 2-8-18-32-18-6
85 Astatine 2-8-18-32-18-7
86 Radon 2-8-18-32-18-8
87 Francium 2-8-18-32-18-8-1
88 Radium 2-8-18-32-18-8-2
89 Actinium 2-8-18-32-18-9-2
90 Thorium 2-8-18-32-18-10-2
91 Protactinium 2-8-18-32-20-9-2
92 Uranium 2-8-18-32-21-9-2
93 Neptunium 2-8-18-32-22-9-2
94 Plutonium 2-8-18-32-24-8-2
95 Americium 2-8-18-32-25-8-2
96 Curium 2-8-18-32-25-9-2
97 Berkelium 2-8-18-32-26-9-2
98 Californium 2-8-18-32-28-8-2
99 Einsteinium 2-8-18-32-29-8-2
100 Fermium 2-8-18-32-30-8-2
101 Mendelevium 2-8-18-32-31-8-2
102 Nobelium 2-8-18-32-32-8-2
103 Lawrencium 2-8-18-32-32-9-2
104 Rutherfordium
105 Hahnium
Atomic number 79
Dhahabu
Hesabu ya chembe za umeme katika kila nafasi, kuanzia nafasi iliyo karibu zaidi na sehemu ya katikati 2-8-18-32-18-1
[Picha katika ukurasa wa 459]
Hata Darwin alikubali hivi: “Kudhani kwamba jicho . . . labda lilijitengeneza lenyewe ni upuzi mwingi ajabu, mimi nasema wazi.”—“The Origin of Species,” uku. 190