Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w77 11/1 uku. 503
  • Je! Unakumbuka?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je! Unakumbuka?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1977
  • Habari Zinazolingana
  • “Mkumbuke . . . Muumba Wako Mkuu Katika Siku za Ujana Wako”
    Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo (2016)
  • Matunda Matamu ya Bure Kutoka Msituni
    Amkeni!—2007
  • Mng’ao wa Bluu wa Beri aina ya Pollia
    Amkeni!—2017
  • Mkumbuke Muumba Wako Mtukufu!
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1999
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1977
w77 11/1 uku. 503

Je! Unakumbuka?

Je! umeyasoma matoleo ya karibuni ya Mnara wa Mlinzi kwa uangalifu? Ikiwa umefanya hivyo, bila shaka utayakumbuka mambo haya:

● Kwa kuwa Yesu Kristo atamrudishia Baba yake ufalme mwishoni mwa utawala wake wa miaka elfu, tutayaelewaje maneno ya Biblia yanayosema utawala wake “hauna mwisho”?

Ufalme wa Kimasihi hautakomeshwa kwa nguvu, nayo matunda ya mambo mema uliyoyatimiza yatadumu milele.​—M 7/15/77, uku. 331.

● Kwa sababu gani ni jambo la maana watu wenye vyeo vya usimamizi hasa wawe wasikilizaji bora?

Kusikiliza mashauri mazuri ya wengine kunaweza kuzuia mtu asifanye makosa makubwa. Kusikiliza maneno ya wengine kunaweza kuamsha akili za mtu, kumpa ufahamu ajue maoni yao hasa na kumwezesha achukue hatua zinazohitajiwa ili kuzuia matatizo madogo yasiwe makubwa.​—M 9/15/77, uku. 418.

● Katika Mithali 13:20, “wapumbavu” tusiopaswa kushirikiana nao ni akina nani?

Si watu wasio na maarifa tu, bali ni watu wasiotaka kufuata adili nzuri, watu wasiomcha Mungu.​—M 9/1/77, uku. 403.

● Wakristo ‘wanaonyeshanaje heshima’?​—Rum. 12:10, tafsiri ya Kiingereza ya New World.

Wanaweza kufanya hivyo kwa kuheshimu sana waamini wenzao, bila kuwachukua vivi hivi tu, bali kufikiria maneno na maoni yao kwa unyofu na kwa moyo wa kupenda.​—M 9/15/77, uku. 426.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki