Maswali Kutoka kwa Wasomaji
● Je! ni kosa Mkristo akitumia dawa za kupunguza maumivu, kwa kuwa Yesu alikataa divai iliyokuwa imechanganywa na dawa ya kupunguza maumivu alipokuwa ametundikwa juu ya mti wa mateso?
Si lazima; kwa wazi Yesu alifanya hivyo kwa sababu maalum (ya pekee).
Kabla tu ya kupigiliwa juu ya mti wa mateso kwa misumari Yesu alikataa kile ambacho Mathayo anaita “divai iliyochanganyika na nyongo.” Naye Marko anakieleza kuwa “mvinyo iliyotiwa manemane.” (Mt. 27:34; Marko 15:23) Mtoaji mmoja wa maelezo alisema hivi: “Manemane iliipa divai chungu ladha (utamu) nzuri zaidi nayo ilikuwa na matokeo ya kulevya yenye sumu. Huenda vitu hivyo viwili vikawa vilikuwa vimetiwa katika kinywaji hicho ambacho Yesu alionja akakikataa.”
Wakati huo Yesu alikuwa akifikia upeo wa mwendo wake wa ukamilifu. (Kum. 5:18, 19) Kwa hiyo, inafahamika wazi kwamba hangetaka kupoteza akili zake au kulewa. Alikuwa ameomba Baba yake akasema kwamba alikuwa na nia ya kupokea yale yaliyokuwa mbele yake. Kwa hiyo, Yesu alihitaji kuwa na ufahamu wake wote wakati huo. (Mt. 26:39; Yohana 10:17, 18) Kristo Yesu alihitajiwa kufahamu kabisa alilokuwa akifanya ili aweze kushika ukamilifu wake na kuwa mwaminifu mpaka mwisho.
Lakini namna gani juu ya Mkristo kukubali dawa za kupunguza maumivu anapoumwa au anapopasuliwa? Biblia inasema kwamba inafaa kumpa kileo mtu anayekaribia kufa, kumsaidia asahau huzuni yake, au labda maumivu yake. (Mit. 31:5) Kwa hiyo, ijapokuwa Maandiko yanalaumu kwa kufaa kulewa kwa kileo au kwa (dawa) za kulevya, hiyo haihusu kukataa dawa za kupunguza maumivu. Dawa kama hiyo ikiwa imetolewa na matabibu (waganga), inaweza kutumikia kusudi jema. Walakini, mtu anayehusika anapaswa kufikiria uwezekano wa kuwa mzoevu wa dawa kama hiyo ya kupunguza maumivu.