Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w80 1/15 kur. 22-24
  • Mahubiri ya Mlimani

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mahubiri ya Mlimani
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1980
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • 1​—MTU AKITUKANWA AU KUUMIZWA
  • 2​—MTU ‘AKITAKA KUKUSHITAKI MAHAKMANI’
  • 3​—UTUMISHI WA LAZIMA KWA WAKILI WA SERIKALI YA KIBINADAMU
  • 4​—OMBI LA MSAADA WA KIMWILI
  • Inamaanisha Nini Kugeuza Shavu Lile Lingine?
    Amkeni!—2010
  • Kiwango cha Juu kwa Wafuasi Wake
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1986
  • Mahubiri Yenye Sifa Zaidi ya Yote Yaliyopata Kutolewa
    Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
  • Mahubiri Maarufu ya Mlimani
    Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1980
w80 1/15 kur. 22-24

Mahubiri ya Mlimani

“Msishindane na Mtu Mwovu”

BAADA ya kuzungumza juu ya viapo na nadhiri katika Mahubiri yake ya Mlimani, Yesu alizungumza juu ya namna ya kuwatendea watu ambao huenda wakawaumiza na kuwaudhi wengine. Yeye alianza kwa kutaja jambo ambalo wasikilizaji wake walikuwa wamejifunza kutokana na Torati ya Musa: “Mmesikia kwamba imenenwa, Jicho kwa jicho, na jino kwa jino.”​—Mt. 5:38; linganisha Kutoka 21:23-25; Mambo ya Walawi 24:19-21.

Wengine wameilaumu sheria hii kwamba ni kali mno. Hata hivyo, haikuhalalisha kujilipiza kisasi kama vile kisasi chenye sifa mbaya kati ya jamaa na jamaa cha nyakati za kisasa, kwa maana Maandiko ayo hayo ya Kiebrania vilevile yasema hivi: “Usiseme, Nitamtenda kama alivyonitenda mimi; nitamlipa mtu huyo sawasawa na tendo lake.” (Mit. 24:29) Sheria ya “jicho kwa jicho, na jino kwa jino” ingefikilizwa baada ya mtu kuletwa hukumuni “mbele za [Yehova], mbele ya makuhani na waamuzi watakaokuwapo siku hizo.”​—Kum. 19:15-21.

“Lakini mimi nawaambia,” akaendelea Yesu, “Msishindane na mtu mwovu.” (Mt. 5:39a) Tutalichukuaje jambo hili? Yesu aliwasaidia wasikilizaji wake kwa kutoa mifano minne ambayo ingewasaidia kumtendea ifaavyo “mtu mwovu,” yaani, mtu ambaye angewadhuru katika njia fulani.

1​—MTU AKITUKANWA AU KUUMIZWA

Kwanza Yesu aliwaeleza wasikilizaji wake jambo la kufanya wanapotukanwa au kumizwa: “Mtu akupigaye shavu la kuume, mgeuzie na la pili.”​—Mt. 5:39b.

Hii haimaanishi kwamba mtu anayepigwa kofi au anayepigwa ngumi alipaswa ajiachilie tu aendelee kupigwa bila kujikinga. Alipopigwa kofi usoni wakati wa kuhukumiwa kwake kusiko kwa haki mbele ya kuhani mkuu, Yesu alipinga kutendwa vibaya hivyo, akisema: “Kama nimesema vibaya, ushuhudie ule ubaya; bali kama nimesema vema, wanipigia nini?”​—Yohana 18:22, 23; linganisha Matendo 23:3.

Kupigwa kofi “shavu la kuume” kulikotajwa na Yesu kuliwakumbusha wasikilizaji wake, si kofi linaloleta maumivu bali sana sana la kutusi na kuaibisha. Maelezo juu ya Mathayo ya W. F. Albright na C. S. Mann yasema hivi: “Hapa Yesu anazungumza juu ya jambo linalotendeka katika Mashariki ya Karibu mpaka sasa​—kati ya mapigo yote ya mwili linalotusi zaidi ni lile la kupiga shavu la kulia kwa upande wa nyuma wa mkono.” Mapokeo ya Kiyahudi yaliweka faini ya zuz 400 (zinazolingana na dinari 400) kwa kofi kama hilo la kutusi la mtu kutumia upande wa nyuma wa mkono. Kiasi hiki kilikuwa zaidi ya malipo ya mwaka mzima kwa mfanya-kibarua mkulima.

Masimulizi ya Injili ya Luka, ambayo sana sana yaliandikiwa watu wasio Wayahudi, yanatumia maneno ya Yesu katika njia ya kawaida tu: “Akupigaye shavu moja, mgeuzie la pili.” (Luka 6:29a) Hii haihusu kofi la kutusi tu, bali mapigo ya jeuri. Katika mojawapo ya hali hizi, shauri la Yesu lilikuwa ‘kugeuza shavu la pili.’ Yeye alitaka wafuasi wake wawe tayari kuvumilia kutukanwa au kuumizwa bila kulipiza kisasi. Kwa njia hiyo wangekuwa wakimwiga Yesu mwenyewe, ambaye kwa habari yake mtume Petro aliandika hivi: “Yeye alipotukanwa, hakurudisha matukano; alipoteswa, hakuogofya; bali alijikabidhi kwake yeye ahukumuye kwa haki.”​—1 Pet. 2:23; linganisha Isaya 50:6.

2​—MTU ‘AKITAKA KUKUSHITAKI MAHAKMANI’

Kisha, Yesu alizungumza namna mtu anavyopaswa kufanya mtu ajaribupo kumnyang’anya kitu kisheria: “Na mtu atakaye kukushitaki [mahakmani] na kuitwaa kanzu yako, mwachie na joho pia.”​—Mt. 5:40.

Katika siku za kale, ilikuwa desturi watu kupeana vazi kama rehani ya kuhakikisha malipo ya deni. (Ayubu 22:6) Ikiwa mdaiwa alishindwa kulipa, mahakma ingaliweza kumpa mdai vazi hilo. (Mit. 13:13; 27:13) Walakini, sheria ya Mungu ilisema kwamba “joho” (vazi la nje) lililokuwa limetolewa kama rehani halingeweza kuchukuliwa wakati wa usiku, kwa kuwa huenda mdaiwa akawa angaliihitaji kama kitu cha kujifunika nacho alalapo.​—Kut. 22:26, 27; Kum. 24:12, 13.

Yesu aliwashauri wafuasi wake watoe bure “kanzu” ambayo huenda adui katika sheria alikuwa akiitaka; na iliwapasa kufanya hivyo mara tu ‘mtu atakapo kwenda mahakmani,’ kabla mashtaka mahakmani hayajaanza. Na zaidi ya hayo, wao wangefanya jambo jingine zaidi, ‘kumwachia na joho pia,’ ijapokuwa sheria ya Mungu haikudai jambo hilo.

Akikubaliana na shauri hili, mtume Paulo aliwaandikia Wakristo katika Korintho hivi: “Basi, imekuwa upungufu kwenu kabisa kwamba mnashitakiana ninyi kwa ninyi. Maana si afadhali kushutumiwa? Maana si afadhali kunyanga’nywa mali zenu?” (1 Kor. 6:7) Ndiyo, iliwapasa kuwa tayari kupatwa na hasara badala ya kuona sifa ya kundi ikiharibiwa mbele ya watu wote na mabishano fulani mahakmani.

Masimulizi ya Luka ya maneno ya Yesu yanatumika hata inapokuwa si jambo linalohusu mashtaka ya mahakmani: “Akunyang’anyaye joho yako, usimzuilie na kanzu.” (Luka 6:29b) Huenda Luka akawa alikuwa akifikiria watu wanaoshambuliwa barabarani na wanyang’anyi ambao waliwanyang’anya joho zao. Mahali pa kupigania kutwaliwa kwa mavazi ambayo pengine ni ya bei, wanafunzi wa Yesu wangefanya vema wakifanya zaidi ya yale yaliyodaiwa na kupeana ‘hata na kanzu.’ Huenda hii ikawa ingeokoa maisha zao wanaposhambuliwa na wahalifu hatari, au huenda kukawa kungekuwa na matokeo mengine yenye faida.​—Mit. 15:1; Mt. 5:16.

Walakini, Mwana wa Mungu hakumaanisha kwamba watu walipaswa kutoiendea sheria au kwamba iliwapasa wajiachilie waletewe umaskini na watu waovu. Twaona kwamba mtume Paulo alifahamu kwamba sivyo alivyomaanisha Yesu, kwa kuwa Paulo alikwenda mbele ya wakuu wa Kirumi katika jitihada zake za “kuitetea Injili na kuithibitisha” kisheria. (Flp. 1:7; linganisha Matendo 25:8-12.) Wakristo wanaweza kuchukulia watu au mamlaka za kilimwengu hatua za kisheria ili kudai mambo ambayo ni haki yao. Walakini, wanapofanya hivyo haiwapasi kutenda kwa ukali, bali kwa amani. Hata hivyo, katika maisha ya kila siku, Mkristo anapaswa kusitawisha maelekeo ya kutoshikilia haki zake.​—Rum. 12:​17-19.

3​—UTUMISHI WA LAZIMA KWA WAKILI WA SERIKALI YA KIBINADAMU

Kisha Yesu alisema hivi: “Na mtu atakayekulazimisha [utumikie] mwendo wa maili moja, nenda naye mbili.”​—Mt. 5:41.

Usemi ‘atakayekulazimisha utumikie’ unatafsiriwa kutokana na neno la Kigiriki angareuo, ambalo lilitokana na lugha ya Kiajemi. Hapo kwanza, neno hili lilihusu utendaji wa wajumbe waliokuwa wakitumikia watu wote, au matarishi, waliowekwa kwa mamlaka ya mfalme wa Uajemi. Matarishi hawa walikuwa na uwezo wa kulazimisha katika utumishi wao, wanaume, farasi, merikebu pamoja na vitu vinginevyo ambavyo vingesaidia kazi rasmi. (Linganisha Esta 3:13; 15; 8:10, 14.) Warumi waliutumia mpango huu. Wakati wa utumishi wa Yesu wa kidunia, wakuu wa serikali wangaliweza kulazimisha Wayahudi kubeba mizigo au kufanya kazi nyingine za kulazimishwa. (Mt. 27:32; Marko 15:21) Wayahudi waliuona utumishi huu wa lazima wa kutumikia watu wa Mataifa kuwa jambo la kuchukiza sana. Hata hivyo, Yesu aliwashauri wasikilizaji wake waufanye kwa uchangamfu. Kwa kweli, wakilazimishwa kwenda mwendo wa maili moja ya Kirumi (kama futi 5,000, au kilometres 1.5), iliwapasa wao wajitolee kwenda mara mbili ya mwendo huo.

4​—OMBI LA MSAADA WA KIMWILI

Kufuata hilo Yesu aliwashauri waonyeshe ukarimu katika kutoa msaada wa kimwili: “Akuombaye, mpe; naye atakaye kukopa kwako [pasipo faida] usimpe kisogo.”​—Mt. 5:42.

Wasikilizaji wa Yesu wangeweza kukumbuka kwamba sheria ya Mungu ilikataza Waisraeli kudai faida kwa mikopo waliyowatolea Wayahudi wenzao. (Kut. 22:25; Law. 25:37; Kum. 23:20) Na zaidi ya hayo, sheria hiyo iliongeza hivi: “Usifanye moyo wako kuwa mgumu, wala usimfumbie mkono wako nduguyo maskini; lakini mfumbulie mkono wako kwa [ukarimu], umkopeshe kwa kweli yatoshayo haja yake katika ahitajiayo.” (Kum. 15:7, 8) Akiwa Masihi na “Mtimizaji” wa sheria ya Mungu, Yesu alienda hata zaidi katika kupendekeza roho ya utoaji wa ukarimu.​—Mt. 5:17; Matendo 20:35.

Bila shaka shauri la Yesu hapa ni lenye ubora mwingi sana. Watu wanaochagua kuachana na heshima yao na hata vitu vyao vya thamani mahali pa kuvipigania, wanaofanya migawo isiyopendeza bila kunung’unika na wanaotoa mali zao kwa uchangamfu kusudi wasaidie wengine wanaohitaji sana wanawapendeza wanadamu wenzao na kupendwa na Mungu.​—2 Kor. 9:7.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki