“Kipaji cha Uso cha Kahaba”
KWA sababu ya ibada yake ya sanamu yenye aibu, Yerusalemu unasemekana kuwa na “kipaji cha uso cha kahaba.” (Yer. 3:3) Hii inamaanisha kwamba Yerusalemu ulikuwa kama mwanamke kahaba asiye na haya. Ilikuwa kama kwamba matendo yake ya uzinzi yalikuwa yameandikwa katika kipaji cha uso wake, yakionekana kwa wote.