Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w79 11/1 uku. 24
  • Maswali kutoka kwa Wasomaji

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Maswali kutoka kwa Wasomaji
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1979
  • Habari Zinazolingana
  • Mikaeli Yule Mwana-Mfalme Mkuu Asimama
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1987
  • Mtegemee Yehova Kama Samsoni Alivyofanya
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2023
  • Yule Malaika Mkuu Mikaeli Ni Nani?
    Maswali ya Biblia Yajibiwa
  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1975
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1979
w79 11/1 uku. 24

Maswali kutoka kwa Wasomaji

● Mtumishi wa Mungu Samsoni alikwenda mahali pa kahaba katika mji wa Gaza katika Filistia kwa sababu gani?

Habari hiyo juu ya Samsoni na malaya huyo katika mji wa Gaza katika Filistia inasomwa hivi: “Samsoni akaenda Gaza, akaona huko mwanamke kahaba [malaya], akaingia kwake.” (Amu. 16:1) Hakuna jambo lo lote katika habari hiyo linaloonyesha kwamba kusudi la kwenda Gaza lilikuwa kumwona mwanamke kahaba. Mahali pake, alipokuwa humo mjini, alimtambua mwanamke wa namna hiyo, na, kwa vile alivyokuwa katika eneo la Wafllisti adui, nyumba yake ndiyo iliyokuwa mahali peke yake angeweza kupata mahali pa kulala usiku huo. Kwamba kusudi lake lilikuwa kupata mahali pa kulala peke yake inaonyeshwa wazi na yale ambayo tunasoma baadaye: “Basi Samsoni akalala mpaka usiku wa manane, akaondoka katikati ya usiku.” (Amu. 16:3) Angalia kwamba habari hiyo haisemi kwamba yeye aliendelea kulala naye mpaka usiku katikati.

Walakini, huenda Wafilisti wakawa waliamua kwamba Samsoni alikuwa amemlipa kahaba huyo kusudi alale naye. Ikiwa ndivyo walivyoamua, wangekuwa na hakika kwamba wangemkamata asubuhi yake. Hilo, pia, lingetumikia kusudi la Samsoni la kuchukua hatua juu yao kwa kung’oa malango ya Gaza na kuuacha mji huo bila ulinzi.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki