Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w81 8/1 uku. 3
  • Hannah—Mwanamke Aliyepata Faraja Katika Sala

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Hannah—Mwanamke Aliyepata Faraja Katika Sala
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1981
  • Habari Zinazolingana
  • Alimweleza Mungu Mahangaiko Yake
    Igeni Imani Yao
  • Jinsi Hana Alivyopata Amani
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2007
  • Alimmwagia Mungu Mahangaiko Yake Kupitia Sala
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2010
  • Hana Alisali ili Apate Mwana
    Masomo Unayoweza Kujifunza Katika Biblia
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1981
w81 8/1 uku. 3

Hannah—Mwanamke Aliyepata Faraja Katika Sala

Hana asiye na mtoto aliishi wakati ambapo wanawake waliona kutokuzaa kuwa laana kubwa sana. Maoni yao yalikuwa kama yale ya Raheli, ambaye kwa kukata tamaa alimwaambia Yakobo mumewe hivi, “Nipe wana kama sivyo, nitakufa mimi.” (Mwa. 30:1) Hana, pia, aliona kuwa utu uke wake haukutimizwa kwa kutokuwa na watoto. Uhakika wa kwamba alikuwa mmoja tu wa wake wawili wa Elkana uliongeza tatizo hilo. Hiyo ilikuwa hivyo sana sana kwa sababu kwa mke wake Penina, Elkana alikuwa amepata wana na binti.

Wakati Elkana na jamaa yake waliposafiri mpaka mahali patakatifu huko Shilo kuabudu, Penina alitumia nafasi hiyo kumchokoza Hana, akimfanyia mzaha kwa sababu ya kuwa tasa. Hana alilia asile sehemu yake ya chakula cha dhabihu. Ndipo mume wake alijaribu kumfariji akisema: “Hana, unalilia nini? Kwani huli chakula? Kwa nini moyo wako una huzuni? Je! Mimi si bora kwako kuliko watoto kumi? ”—1 Sam. 1:2-8.

Mwishowe, Hana aliweka mahangaiko yake yote kwa Yehova Mungu. Pindi moja akiwa Shilo, aliondoka mezani “akamwomba [Yehova], akalia sana.” (1 Sam. 1:9, 10) Kwa bidii sana Hana alisihi hivi: “Ee [Yehova] . . . ikiwa wewe utaliangalia teso la mjakazi wako, na kunikumbuka, wala usinisahau mimi mjakazi wako, na kunipa mimi mjakazi wako mtoto mume, ndipo mimi nitakapompa [Yehova] huyo mtoto siku zote za maisha yake wala wembe hautamfikilia kichwani kamwe.”—1 Sam. 1:11.

Kwa kuwa midomo yake ilionekana kana kwamba ananena, huku akieleza Yehova Mungu taabu yake ya moyoni, kuhani mkuu Eli kwa kosa alimdhania kuwa amelewa naye akamkaripia. Lakini kwa haraka Hana akasema: “Hasha! bwana wangu, mimi ni mwanamke mwenye roho ya huzuni; mimi sikunywa divai wala kileo, ila nimeimimina roho yangu mbele ya [Yehova]. Usimdhanie mjakazi wako kuwa ni mwanamke asiyefaa mtu; kwa kuwa katika wingi wa kuugua kwangu na kusikitika kwangu ndivyo nilivyonena hata sasa.”—1 Sam. 1:15, 16.

Akifahamu kosa lake Eli alimtakia baraka za Mungu, akasema: “Enenda kwa amani; na Mungu wa Israeli akujalie haja yako uliyomwomba.”—1 Sam. 1:17.

Sala ya Hana, kutia na maneno ya Eli yalimhusuje? Alipata faraja ya kweli. Hana akaanza kula chakula na “uso wake haukukunjamana tena.” (1 Sam. 1:18) Akiwa amemwachia Yehova Mungu jambo hilo, akawa bila huzuni nyingi ya moyoni. Hata alifahamu kwamba Aliye Juu Zaidi alipendezwa naye kama mtu, naye alimtumainia kwa uhakika apate msaada. Ingawa hakujua matokeo yangekuwa nini, Hana alifurahia amani ya ndani. Lazima awe alitambua kwamba ama kipindi cha kuwa bila mtoto kingekoma au Yehova Mungu angetimiza kwa njia fulani uhitaji wake wa kutokuwa na mtoto.

Bila shaka tumaini la Hana kwa Mungu Mwenye Nguvu Zote halikuwekwa mahali pasipofaa. Alizaa mvulana akamwita jina lake Samweli. Baada ya kumwachisha maziwa, Hana alimpeleka Samweli akatumikie katika patakatifu. (1 Sam. 1:19-28) Kwa kuwa Biblia inataja orodha ya miaka ya kuweka Walawi kwenye utumishi, “wenye miaka mitatu na zaidi,” inaweza kuwa kijana huyo alikuwa mwenye umri wa miaka mitatu wakati huo.—2 Nya. 31:16.

Akithamini fadhili za Yehova kwake, Hana alimtolea sala ya shukrani. Sala hiyo ilimtukuza Yehova kuwa Yeye halingani na mtu ye yote. Hana alisema: “Hakuna aliye mtakatifu kama [Yehova]; kwa maana hakuna ye yote ila wewe, wala hakuna mwamba kama Mungu wetu.” (1 Sam. 2:2) Kwa upande wake mwenyewe, Hana alikuwa ameona kwamba Mungu Mwenye Nguvu Zote ni kama mwamba ulio imara, yaani mwenye kutegemeka na imara. Tunaweza kumtegemea yeye kabisa.

Baraka zaidi zilikuwa mbele ya Hana. Wakati mmoja, alipokuja na mumewe huko Shilo, Eli aliwabariki wote wawili, akasema: “[Yehova] na akupe uzao kwa mwanamke huyu, badala ya azimio [Samweli] aliloazimia [Yehova].” (1 Sam. 2:20) Hana alikuwa na furaha ya kuona baraka hiyo ikitimizwa. Hatimaye akawa mama wa wana wengine watatu wa kiume na wawili wa kike. —1 Sam. 2:21.

Kama vile Hana alivyopata faraja katika sala, sisi pia tunaweza kupata msaada kwa kuweka mahangaiko yetu yote kwa Yehova Mungu. Atajibu maombi yote yanayopatana na makusudi yake. Kwa hivyo, tukimimina mioyo yetu kwa baba yetu wa kimbinguni, na tuwe, kama Hana, ‘wasiojihangaikia tena,’ tuwe na hakika kwamba yeye ataondoa mzigo wetu, vyo vyote utakavyokuwa, au atatuwezesha tuuvumilie.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki