Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • lfb somo la 35 uku. 86-uku. 87 fu. 1
  • Hana Alisali ili Apate Mwana

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Hana Alisali ili Apate Mwana
  • Masomo Unayoweza Kujifunza Katika Biblia
  • Habari Zinazolingana
  • Alimweleza Mungu Mahangaiko Yake
    Igeni Imani Yao
  • Alimmwagia Mungu Mahangaiko Yake Kupitia Sala
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2010
  • Jinsi Hana Alivyopata Amani
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2007
  • Hannah—Mwanamke Aliyepata Faraja Katika Sala
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1981
Pata Habari Zaidi
Masomo Unayoweza Kujifunza Katika Biblia
lfb somo la 35 uku. 86-uku. 87 fu. 1
Hana akimkabidhi Samweli kwa Eli katika maskani

SOMO LA 35

Hana Alisali Ili Apate Mwana

Elkana alikuwa mwanaume Mwisraeli aliyekuwa na wake wawili, Hana na Penina, lakini Elkana alimpenda Hana zaidi. Penina alimdhihaki Hana wakati wote kwa sababu yeye alikuwa na watoto wengi na Hana hakuwa na mtoto hata mmoja. Kila mwaka, Elkana pamoja na familia yake walienda kuabudu katika maskani iliyokuwa Shilo. Siku moja, walipokuwa huko, alimwona mke wake mpendwa Hana akiwa amehuzunika sana. Alimwambia hivi: ‘Hana, tafadhali usilie. Mimi nipo. Ninakupenda.’

Baadaye, Hana alienda kusali. Akiwa analia, alisali kwa Yehova na kumwomba msaada. Alitoa ahadi hii: ‘Yehova, ikiwa utanipa mtoto wa kiume, nitamtoa akutumikie maisha yake yote.’

Kuhani Mkuu Eli anamwona Hana akisali huku akilia

Kuhani Mkuu Eli alimwona Hana akilia naye akafikiri kwamba Hana alikuwa amelewa. Hana akamjibu: ‘Hapana, Bwana wangu, mimi sijalewa. Nina tatizo zito nami ninamweleza Yehova kulihusu.’ Eli alitambua kwamba alikuwa amekosea, kwa hiyo akamwambia hivi: ‘Mungu na akutimizie ombi lako.’ Hana alihisi vizuri, kisha, akaenda zake. Ndani ya mwaka mmoja, alipata mwana naye akamwita jina lake Samweli. Hebu wazia jinsi Hana alivyofurahi kupata mwana!

Hana hakusahau ahadi aliyotoa kwa Yehova. Mara tu Samweli alipoacha kunyonya, alimpeleka ili akatumikie katika maskani. Hana alimwambia Eli hivi: ‘Huyu ndiye mvulana ambaye nilisali kumhusu. Ninamtoa amtumikie Yehova maisha yake yote.’ Kila mwaka, Elkana na Hana walimtembelea Samweli na kumletea koti lisilo na mikono. Yehova alimbariki Hana naye akapata wana wengine watatu na mabinti wawili.

“Endeleeni kuomba, nanyi mtapewa; endeleeni kutafuta, nanyi mtapata.”​—Mathayo 7:7

Maswali: Kwa nini Hana alikuwa mwenye huzuni? Yehova alimbariki Hana jinsi gani?

1 Samweli 1:1–2:11, 18-21

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki